naomba kusahihisha ni ripoti ya jaji bomani na wal siyo jaji makani
Huyu Heyo anazeeka vibaya sana.Yaani huyu Sinclair ainunue hii report(maana na uhakika hajaipata bure bila kitu kidogo!) halafu wamuajibishe?Unachekesha wewe babu.Wakumuwajibisha ni huyo baba lao ambaye haishi jipya kila leo.Ni kero tupu kazi kujichekesha kwa wazungu na kuitikia 'yes sir'
Lakini ripoti si ya Rais... si anao uhuru wa kumpa yeyote amtakaye... hiyo ripoti haikuagizwa na Bunge hata sielewi kwanini wabunge wanakuja juu. Kama walikuwa wanataka si wangeunda kamati yao teule walipoombwa?
Kwanza awajibishe aliyemwezesha kabaila sinclair kupata hiyo ripoti na kufanya kazi iliyofanywa na kamati teule ya madini kuwa ya kujungujiko.
Si ajabu hata hotuba ya waziri wa madini sinclair anayo na anajua kinachoendela
Lakini ripoti si ya Rais... si anao uhuru wa kumpa yeyote amtakaye... hiyo ripoti haikuagizwa na Bunge hata sielewi kwanini wabunge wanakuja juu. Kama walikuwa wanataka si wangeunda kamati yao teule walipoombwa?
Tutegemee majibu ya mkato kama yale ya meremetaNi nani atakayejibu hoja ya Cheyo?? Waziri Mkuu, Mwanasheria mkuu au baadhi ya wajumbe walioko kwenye kamati ya Jaji Bomani??
Umefika wakati kwa Serikali kutoa tamko rasmi juu ya jinsi ripoti yake ilivyomfikia Bw. Sinclair kabla ya wahusika wengine muhimu nchini na hatua gani zimechukuliwa kuziba mapengo na kuwawajibisha wahusika. Ningefurahi kumsikia Waziri mkuu anasemaje kuhusiana na hili??
john cheyo, yule mbunge wa bariadi yuko bungeni anazungumza sasa hivi, anashangaa ripoti ya tume ya madini ya jaji makani kuwa kwenye web site ya mtu anayejiita rafiki wa kikwete. anataka achukuliwe hatua kama yule mauritius aliyefukuzwa na nyerere baada ya kusema ameiweka serikali mfukoni.....
Jamani hiyo ripoti siyo ya raisi bali ni ya taasisi.
Ikulu ni taasisi ya umma na si mali ya binafsi ya rais.
Rais ni kiongozi tu kwenye hiyo taasisi.
Kama ametoa siri za taasisi inabidi awajibishwe.
Tatizo ni huyu Mr Kisura jamani
Hivi mimi sielewi yeye anawafanyia nini Watanzania zaidi ya kujipendekeza kwa wazungu tu
alafu na mijibunge yetu inakaa kumsifia tuuuuu, wakati hakuna lolote analofanya la maana, itakuwaje report ambayo bunge haina mpaka leo hii, huyo sinclair tayari anayo, na hata hawaulizi na wala Kikwete aanaona sawa tuu
Hii nchi bwana inatia hasira sana tena sana ndugu zangu, maana kila kitu kimegoma, njia sahii ya nguvu ya hoja naona haina nguvu tena kwa sababu nguvu ya mafisadi na pesa a wizi ndivyo vilivyoshika nafasi katika nchi yetu
sasa sijui solution tutaitafuta vipi hapa