Jamhuri ya Bolivia ya Venezuela | República Bolivariana de Venezuela

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,143
Reaction score
6,560
| Jamhuri ya Bolivia ya Venezuela, Bolivarian Republic of Venezuela au República Bolivariana de Venezuela

Ni taifa linalopatikana bara la Amerika Kusini katika uwanda wa juu wa Caribbean, likiwa limepakana na Colombia - Magharibi, Brazil - Kusini Mashariki, Guyana - Mashariki, Trinidad na Tobago - Kaskazini Mashariki, Curaçao, Aruba, Leeward Antilles upande wa Kaskazini katika rasi ya Caribbean na bahari ya Caribbean.

Venezuela yenye ukubwa wa eneo zipatazo 912,050 Kilometers Square sawa na 352,144 Square Mile's, lugha rasmi ni Kihispaniora pia zikitambuliwa lugha nyingine 26. Huku lugha za Mandarin "KiChina", Kireno, KiItaliano na Kiarabu zikizungumzwa na idadi ya watu wengi.


Bendera ya Jamhuri ya Bolivia ya Venezuela

Pesa rasmi ikiwa Bolívar ya KiVenezuela - Bolívar 1 ni sawa na Centimos 100. Kauli kuu ya taifa hili (Motto) ni “Dios y Federación” | “Mungu na Shirikisho”.

Mji mkuu wa taifa hili ni Caracas, mji ulioendelea zaidi wenye kuhodhi masuala ya kiserikali. Jiji hili la Caracas ni moja ya majiji makubwa katika mwambao wa Amerika ya Kilatini. Miji mingine bora ni San Cristóbal, Maracaibo, Valencia, Cumaná, Maturin, Ciudad Bolívar, Maracay, Ciudad Guayana, Barquisimento na Barcelona kuifanya Venezuela moja ya nchi ya Amerika ya Kilatini kuwa na miji mingi iliyoendelea.


Jijini Caracas ©Miguel Fernandez

| Uhalisia wa hali ya Venezuela na siasa za kimataifa

Nchi hii bora iliyojengeka na yenye miundombinu ya kukata na shoka imepitia kipindi kigumu cha mdororo wa kiuchumi na kushuka thamani kwa Bolívar ya KiVenezuela chini ya Mh. Rais Nicolás Maduro aliyerithi mikoba ya Hugo Chávez, aliyewekewa vikwazo na mataifa ya "Magharibi".


Daraja la Ukubwa wa Rafael - Maracaibo

Kuwekewa vikwazo hivi vya kiuchumi kwa Venezuela kumepelekea hali isiyokuwa nzuri kwa raia wasiokuwa na hatia, chanzo kikuu cha vikwazo hivyo vinavyotafsiriwa kama mabavu, uonevu na ukoloni mamboleo usiokuwa na msingi ni kutokana na taifa kukataa kuibiwa rasilimali za Wavenezuela.

Hali hii ya mapitio na maumivu imewakumba Wavenezuela wengi kutokana na ukosefu wa ajira, rushwa na uhalifu kupelekea umaskini na raia wengi kuihama nchi.


Bandari ya Cross

Hivi karibu dunia imeshuhudia kituko cha aina yake baada ya kiongozi wa upinzani na kibaraka asiyekuwa na sera, Bw. Juan Guaído kusimama hadharani na kujitangaza rais akipatiwa kiburi na jeuri na mataifa ya Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya. Hali hiyo iliyozua gumzo ilizidi kupandisha joto duru za siasa za kimataifa baada ya rais Vladimir Putin wa Urusi kutozungumza chochote na kutuma ndege 6 na manowari 2 za kijeshi ndani ya Venezuela na kumuambia Nicolás Maduro "Wewe ndiye rais uliyechaguliwa".

Hali ilizidi kupamba moto baada ya Marekani kutaka mataifa yamtambue rais, hali iliyojibiwa na Uchina, Cuba, Uturuki, El Salvador, Saint Vincent na Grenadines, Misri, Syria, Sahrawi na Vietnam kwa kumuunga mkono Maduro.

Hali ikiwa si hali wengi wakitabiri kupinduliwa kwa Maduro, asubuhi yake rais wa Korea ya Kaskazini Mh. Bw Kim Jong Un maarufu kama "Kiduku" alirusha makombora mawili katika bahari ya Pacific kisha kuchagua upande wa Maduro.

Hali hiyo ilichochewa zaidi baada ya Bolivia kutuma kikosi cha wanajeshi kufanya msako na kuwakamata raia wa Marekani na Umoja wa Ulaya waliopatikana katika taifa hilo.

Vituko na vimbwanga vikizidi kuendelea Afrika ya Kusini ilichagua upande wa Maduro huku mataifa mengi ya Afrika yakiendeleza unafiki uliojificha.

Hali ilizidi kuvutia na zamu hii ikionekana kama sinema baada ya Marocco kupiga marufuku Juan Guaído kutosogelea mipaka ya taifa hilo.


Vijana wakisherehekea ©Jose Carlos

Panapofuka moshi basi tambua kuna moto, Uajemi iliingia makubaliano na ushirikiano na Venezuela. Hivi majuzi imefikisha meli ya mafuta katika rasi ya Maracaibo uliyosindikizwa na makomando wa Belarus na Bolivia na kupokelewa kwa ustadi, ndelemo na vifijo.

| Uchumi, Biashara, Kilimo, Utalii na Maendeleo

Taifa hili ndio lenye kuongoza kuwa na akiba ya mafuta ulimwenguni, taifa linalozalisha kahawa na kokoa ni nyumbani kwa viumbe 48 visivyopatikana sehemu yoyote duniani. Biashara za dhahabu, gesi asilia na petroli ni sehemu kubwa ya kutegemewa.


Mnyama Anteater © Maracaibo Vest

Maporomoko ya Angel Falls yenye urefu wa futi 3,212 sawa na mita 979 ndio yenye kuongoza. Maracaibo, Punto Fijo na ghuba ya Paria maeneo waliyowahi kuishi Amerigo Vespucci na Christopher Columbus ndio maeneo yenye kutembelewa na watalii wengi.


Margarita Island

| Elimu

Elimu ndani ya Venezuela ni iliyokuwa bora lakini isiyokuwa na thamani kutokana na ukosefu wa ajira na kiwango cha umaskini unaopelekea wahitimu wengi kuihama nchi. Wahitimu wengi wanakimbilia Ireland, Uhispania, Colombia, China na Mexico.

Vyuo baadhi vyenye kutoa elimu ya juu iliyokuwa bora ni Central University of Venezuela, University of Zulia, University of the Andes, Simón Bolívar University, University of East na Escuela de Cíne y Televisión de Venezuela.

| Michezo, Burudani, Muziki, Uandishi na Sanaa ya Uchoraji

Venezuela kimekuwa kituo cha burudani, sanaa, michezo na uandaaji filamu na matangazo mbalimbali. Michezo yenye wafuasi wengi ni baseball, mpira wa miguu na mpira wa kikapu. Venezuela hutambulishwa vyema kimataifa na timu ya taifa maarufu kama "Vinotinto" huku wachezaji kama Solomón Rondón “Don Don”, Juanpi, Sergio Córdova, Juan Arango, Pablo Camacho na Roberto Rosales wakipeperusha bendera ya Venezuela.

Mwendesha magari ya mbio za rangaranga Formula 1, Pastor Maldonado amekuwa mwakilishi wa taifa kimataifa.

Venezuela ni nyumbani kwa wachoraji nguli Arturo Michelona, Cristóbal Rojas, Carlos Cruz-Diez, Armando Reverón, Jesús Soto, Marisol na Yucef Merhi.

Waandishi wa aina yake kama Andés Eloy Blanco, Andrés Bello, Arturo Uslar Pietri, Fermin Toro na Teresa de la Parra.

Chimbuko la dansi ya "Calipso" ni Venezuela huku wanamuziki Chino y Nacho, Damy Ocean, Calle Ciega, Franco De Vita, Echoes na La Mar wakionekana mwiba kimataifa.

Kampuni za utayarishaji, uandaaji na uchakataji filamu 2 Wolves Production chini ya muongozaji Daniel Duran aliyetayarisha video nyingi za muziki zilizofikia watazamaji billioni ndani ya YouTube video hizo ni Sin Pijama, Ahora Dice, Se Acabó el Amor ilirekodiwa Sanzibar, Mayores, Picky na No Me Acuerdo.


Daniel Duran ©Cacho Diaz


Nuno Gomes

Compostela Films & Art chini ya Nuno Gomes kijana aliyeifanya kazi ya filamu kuonekana rahisi na Kike Audiovisuals chini ya kijana mchuja rangi Kike Aroyale Santander aliyenyuma ya muonekano bora wa matangazo ya kimataifa kama Pepsi, Coca-Cola, Hublot, Corona, Simolta Volta, BBVA, Petronas, Nestle, Ferrari na Adidas kwa uchache.

Hii ndio Jamhuri ya Bolivia ya Venezuela 🇻🇪
 
Shukran sana MKUU nimeupitia vyema kabisa Mungu akupe afya njema uzidi kutuletea habari moto moto

Ila hali ya VENEZUELA kwasasa ipoje maana one time nlisikia walikua nahali mbaya mnoooooo.....
Shukrani Mkuu,

Kwa sasa Venezuela hali inayo afadhari, biashara taratibu zinafanyika na Wavenezuela wanarudi kuwekeza.

Huduma muhimu zinaanza kurejea taratibu.
 
Kumbe hii nchi tajiri asee , wana rasirimali za kutosha
Hii nchi ilikuwa nzuri mno na bado ni nzuri...Sema mambo ya kuingiliwa kisiasa na Mataifa ya nje ndo yanaigharimu...Their oil..,Ina utajiri wa kutisha...Ni mojawapo wa nchi zilizo kwenye malengo yangu ya kuzitembelea Amerika ya Kusini...Kwanza jina lake tu,what a sweet name😋😋😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…