Write your reply...si utaje hapahapa huo ubaya wa washia?,na huyo mwandishi we fanya kupaste hapa paragraph chache kama amechemka ama anasema kweli tuone,kwanini ufanye siri?
Itikadi yao ya 5
YA NNE:
Kauli yao kuwa Qur-aan imebadilishwa:
Itikadi ya Kishia ni kuwa Qur-aan imebadilishwa, au bora tuseme mafundiho ya madhehebu ya Kishia yanaitakidi kuwa Qur-aan imebadilishwa.
Anasema Ibni Hazm kuwa:
‘Mashia Imamiyah wote wa zamani na wa sasa wanaamini kuwa Qur-aan imebadilishwa na kuongezwa yasiyokuwemo na kupunguzwa ndani yake mengi pamoja na kubadilishwa mengi. ‘
Haya ni maneno ya Ibni Hazm
Anasema Ni’imatullah al-Jazairiy:
‘Habari ni nyingi sana bali ni nyingi kupita kiasi (mutawaatir) zinazotuthibitishia kuwa Qur-aan imebadilishwa maneno yake, mada zake, na irabu yake.’
Al-Anwaar an-Nu’umaniyyah – Juzuu ya 2 ukurasa 357
Kauli hizi zimesemwa na wingi miongoni mwa maulamaa wa Kishia akiwemo Al-Huuru Al-’Aamiliy anayejulikana kuwa ni miongoni mwa maulamaa wakubwa.
Hebu tusikilize maulamaa wa Kishia wanasema nini juu ya Al-Huuru Al-’Aamiliy.
Anasema Al Khunsariy:
‘Al-Huuru Al-’Aamiliy alikuwa katika maulamaa wetu wakubwa sana waliotangulia na waliokuja baadaye na alikuwa bahari ya elimu’.
Ama Annuriy yeye anasema juu yake:
‘Al-Aamiliy alikuwa mfanya tahakiki, mwenye kuielewa vizuri elimu ya hadithi na mcha Mungu sana.’
Sasa hebu tumsikilize Al-Huuru Al-’Aamiliy mwenyewe anasema nini juu ya Qur-aan tukufu. Anasema Al-Huuru Al-’Aamiliy:
‘Juwa kuwa ukweli usio na shaka ndani yake kutokana na habari nyingi sana zilizotufikia ni kuwa hii Qur-aan tuliyonayo mikononi mwetu imebadilishwa kidogo baada ya kufa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na wale walioikusanya baada yake wakapunguza mengi kati ya maneno yake na aya zake.’
Maneno kama haya yalitamkwa pia na Al Qumy na Al-Kulayniy na wengi miongoni mwa maulamaa wa Kishia akiwemo Ahmed bin Abi Twaalib Al Tubrusiy.
Anaendelea kusema Al-Aamiliy:
‘Na itikadi hii kuwa Qur-aan imepunguzwa ni katika mambo ya lazima kuamini kila mwenye kufuata madhehebu ya Kishia.’
Yote haya yamo ndani ya kitabu cha ‘Mira-atul Anwar’ ukurasa wa 36, Na maana yake ni kuwa Al-Aamiliy anaitakidi kuwa kila mwenye kufuata madhehebu ya kishia lazima aamini kuwa baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Qur-aan imepunguzwa na kuongezwa yale yasiyokuwemo.
Anasema Yusuf Al Baharani:
‘Kutokana na wingi wa riwaya hizi, inawezekana hata kuzitilia shaka sheria zote za dini kwani habari zote hizi zimepokelewa kupitia njia hiyo hiyo moja, mashekhe na wapokeaji wote ndiyo hao hao. Ikiwa watu hawa wameweza kufanya khiana kubwa, basi vipi watashindwa kuifanya khiyana hii ndogo?’
Unakusudiwa hapa uimamu wa ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa amana hiyo ni kubwa zaidi kupita dini yenyewe.
Durar al Najafiyah – ukurasa 294
Ama Adnan al Baharani yeye anasema :
‘Habari hizi (za kubadilishwa Qur-aan) ni nyingi sana hata haina haja ya kuziandika baada ya kuwa na uhakika kuwa pande zote mbili wamebadilisha kwa kuongeza na kupunguza (anakusudia na wao Mashia pia wamebadilisha), na kwa vile hata Masahaba na Tabiina wanayajuwa hayo vizuri, bali ijmai ya kundi lenye haki linayakubali hayo.’
Anakusudia kuwa Shia ndilo kundi lenye haki na kwamba ni wajibu kwao kuwa na itikadi hiyo.
Shumus ad-Duriyah – 126
Anasema ‘Aliy bin Ahmad al-Kufiy:
‘Maulamaa wote wa riwaya na athar wamekubaliana kuwa Qur-aan hii iliyo mikononi mwa watu si kamili.’
Maneno haya haya yamesemwa na An-Nuur at-Twabrasiy katika kitabu chake maarufu sana kiitwacho ‘Faswlul Khitwaab’ – Ukurasa 27
Anasema An-Nuur at-Twabrasiy katika kitabu chake hicho maarufu kiitwacho ‘Faswlul Khitwaab fiy Tahriyfi Kitaab Rabbil Arbaab:
‘Miongoni mwa dalili kuwa Qur-aan imebadilishwa ni ule ufasaha wake mwingi katika baadhi ya aya na upuuzi ulio ndani ya baadhi ya aya.”
Katika kitabu chake hicho An-Nuur at-Twabrasiy ameziandika sura nyingi sana pamoja na aya anazodai kuwa zimeachwa au kubadilishwa, na hapa nitaandika baadhi chache ya sura na aya hizo:
Nitaanza na Sura maarufu waliyoipa jina la ‘Suratul wilayah’: anasema Attubrusiy kuwa sura hiyo ni kama ifuatavyo:
“ ﻳﺄﻳﻬﺎ ﺍﻟﺬﻳﻦ ﺁﻣﻨﻮﺍ ﺁﻣﻨﻮﺍ ﺑﺎﻟﻨﻮﺭﻳﻦ ﺃﻧﺰﻟﻨﺎﻫﻤﺎ ﻳﺘﻠﻮﺍﻧﻲ ﻋﻠﻴﻜﻢ ﺁﻳﺎﺗﻲ ﻭﻳﺤﺬﺭﺍﻧﻜﻢ ﻋﺬﺍﺏ ﻳﻮﻡ ﻋﻈﻴﻢ ﻧﻮﺭﺍ ﻓﻲ ﺑﻌﻀﻬﻤﺎ ﻣﻦ ﺑﻌﺾ ﻭﺃﻧﺎ ﺍﻟﺴﻤﻴﻊ ﺍﻟﻌﻠﻴﻢ ، ﺇﻥ ﺍﻟﺬﻳﻦ ﻳﻮﻓﻮﻥ ﺑﻌﻬﺪ ﺍﻟﻠﻪ ﻭﺭﺳﻮﻟﻪ ﻓﻲ ﺁﻳﺎﺕ ﻟﻬﻢ ﺟﻨﺎﺕ ﺍﻟﻨﻌﻴﻢ ﻭﺍﻟﺬﻳﻦ ﻛﻔﺮﻭﺍ ﻣﻦ ﺑﻌﺪ ﻣﺎ ﺁﻣﻨﻮﺍ ﺑﻨﻘﻀﻬﻢ ﻣﻴﺜﺎﻗﻬﻢ ﻭﻣﺎ ﻋﺎﻫﺪﻫﻢ ﺍﻟﺮﺳﻮﻝ ﻋﻠﻴﻪ ﻳﻘﺬﻓﻮﻥ ﻓﻲ ﺍﻟﺠﺤﻴﻢ ﻇﻠﻤﻮﺍ ﺃﻧﻔﺴﻬﻢ ﻭﻋﺼﻮﺍ ﻭﺻﻴﺔ ﺍﻟﺮﺳﻮﻝ ﺃﻭﻟﺌﻚ ﻳﺴﻘﻮﻥ ﻣﻦ ﺣﻤﻴﻢ”
’Yaa ayuha lladhiyna amanu aaminu binnurayni anzalnahuma yatluwaani ‘alaykum ayaatiy wa yuhadhiraanikum ‘adhaabi yawmin ‘adhiym nuuran fiy ba’adhihima min baadhin wa anaa ssamiy’ul ‘aliym. Inna lladhiyna yuwafuwna bi’ahdi Llaahi wa rasuwlihi fiy ayatin lahum jannatun na’iym walladhiyna kafaruw mim ba’adi ma aamanuw binaqdhihim miythaqhim wama ‘aahad-hum arrasuwlu ‘alayhi yuqdhafuwna fil jahiym. Dhalamuw anfusahum wa ‘asaw wasiyat rrasuwl ulaaika yusqawna min hamiym.’
Haya yamo ndani ya vitabu vyao mashuhuri kama hicho nilichotangulia kukitaja cha Nuri Al Tubrusi, na pia mwanachuoni wao mwengine aitwae Abi Shahar Ashub na wengi miongoni mwa maulamaa wa Kishia wameandika hayo.
Imepokelewa kuwa ‘Aliy bin ‘Abdillaah alipoisoma aya isemayo:
‘Kuntum khayra ummatin ukhrijat linnas.’ Na maana yake ni: ‘Nyinyi ni umma bora mliodhihirishiwa watu.’
Akasema Ja’afar Asw-Swaadiq: ‘Umma bora wanamuuwa Amiril muuminin na Al-Hasan na Al-Husayn alayhimu ssalaam?’
Na alipoulizwa: ‘Vipi niisome?’
Akajibu:
‘Isome hivi: ‘Kuntum khayra aimmatin’ . Na maana yake: Nyinyi ni maimamu bora.’
Hata suratul Inshiraah wanasema imeteremshwa kama ifutavyo:
‘Alam nashrah laka swadrak – wawadhaana ‘anka wizrak – alladhiy anqadha dhwaharak - warafaana laka dhikrak - bi ‘Aliyyin suhrak.”
Hizi ni baadhi chache sana ya aya na sura wanazoitakidi kuwa zimebadilishwa. Na Nuri Attubrusi huyu katika kitabu chake ameandika faharasi ya Qur-aan yote kuanzia Suratul Baqarah mpaka Suratul Ikhlas huku akizichambua aya anazosema kuwa zimebadilishwa.
Kilichobaki ni kumjuwa: nani huyu Nuri Attubrusiy aliyeandika kitabu akidai kuwa Qur-aan hii tuliyonayo imebadilishwa?
Anasema Abbas Al Qumiy mwandishi wa kitabu kiitwacho: ‘Alkuniya wal laqab:
‘An-Nuur at-Twabrasiyy ndiye Shekhe wa Waislamu – mwenye elimu ya Manabii na Mitume – mwenye kuaminika – aalim aliyekamilika.’
Ama Agha Barzak Al Taharani katika kumsifia An-Nuur at-Twabrasiy anasema:
‘Imamu wa maimamu wa elimu ya hadithi na ni katika maulamaa wakubwa wa kishia katika karne za mwisho na mkuu wa mashekhe wa kiislamu katika karne hii.’
Hivi ndivyo anavyosifiwa huyu aliyeandika kitabu akakiita: ‘Fasli l khitab fiy ithbat taharif kitab rabbi l arbab.
Na maana yake ni:
Kauli ya uamuzi juu ya kubadilishwa kwa kitabu cha Allaah.