Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

"Nawasalimia Kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

Huyu ni nani???
Siyo jambo la msingi sana halina mantiki yoyote katika maisha halisi.
Nimekujibu kirahisi sababu ni jambo rahisi sana.
 
Maelezo yako naona kama yana siasa kwa mbali ndani yake

Hii hoja ni kweli kama mtu ataweka siasa kando

Maana ya salamu ni kujuliana hali na/au kutakiana heri

Salamu mara nyingi ni lazima inakuwa na pande mbili, mtoa salamu kuamkia na watolewa salamu kuitikia

Kiukweli hatuwezi kuhesabu kuwa mtu amesalimu watu kwa kusema "...nawasalimia kwa jina la..."

Wala kusema "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee" si salamu

Sasa kwa tafsiri nyepesi ni kwamba Mama hatoi salamu anaposimama kuhutubia bali anatumia kutamka kaulimbiu tu

Kuna vitu kama kibwagizo, kaulimbiu, misemo, methali na kadhalika ambazo nazo huwa na sehemu mbili hivyo hivyo lakini hatuiti kuwa ni salamu

Ni wazi inabidi ashauriwe aanze kusalimia watu sasa

Tukirudi kwa upande wa dini yake Mama mwenyewe (ya uislamu) ni dhahiri pia ni kosa kufanya chochote kwa jina tofauti na MwenyeziMungu (Allah)

Hii sijui imekaaje kwa upande wake ila kauli hiyo hutafsiriwa anakufuru

Naamini washauri wapo hadi (wanaohusika) kwenye maswala ya dini sasa sijui hawalioni hili!!?
 
Mkuu hii salamu Haina msingi wa kuitegemea.

Huyo Jamhuri hafahamiki ni nani...
Nina uhakika mnaoona hiyo salami haiko sawa mtakuwa wawili tu au watano kati ya was Tz m60. Sasa hapo ndio ujione NDEZI.

Mnahangaika sana kutafuta cha kumkosoa Mama hampati. Ipo siku mtasema kuvaa Mtandio sio sawa.
 
Nina uhakika mnaoona hiyo salami haiko sawa mtakuwa wawili tu au watano kati ya was Tz m60. Sasa hapo ndio ujione NDEZI.

Mnahangaika sana kutafuta cha kumkosoa Mama hampati. Ipo siku mtasema kuvaa Mtandio sio sawa.
Rais ajitahidi tu kusema Bwana Yesu asifiwe, maana ukishakua kiongozi unakua kiongozi wa wote,

Ila kusema nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Kwa hapa nyumbani Tanzania hiyo sio salamu.
 
Mbona unaangaika sana ila yawekana
wewe ndo yule aliyekua anajiita stroke


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mkuu sihangaiki,

Tunakumbushana tu, sote ni binadamu,

Wala usikasirike sana.

Naamini Rais Mwenyewe atakua amenielewa.

Namheshimu sana na kumpenda kiongozi wangu ndio maana nayasema haya.
 
Unajua madhara ya kuambiwa ^Badilisha hiki, badili na kile pia. Ona, badilisha hapa. Badilisha kila kitu kabisa. Hakikisha the so-called legacy inasahaulika,^ ndiyo haya ya kusafiri bila kujua aendako...
Kwa kifupi hii salamu siipendi hata kidogo. Kwanza imechakachua salamu yetu wakristo. Ingetungwa tofauti nisingekuwa na neno. Sisi yetu ni "Nakusalimu kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo", Sasa hii ya huyu mama imechakachua salamu yetu.
 
Vyovyote iwavyo hapa tunapitisha muda tu, siku iende.
Kama kweli hujui nini maana ya "Nawasalimu katika Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" utapata taabu sana.
Aliyekwenda kaenda.
 
Nchi ina hadhi ya mama, ndio inayozaa na kulea Watu Kwa kuwapa mahitaji Kama chakula, maji nk.
Baada ya mama yako kukuzaaa "anakutupa "Katika nchi, na nchi ndio inaamua uweje

Ndio maana tuna wivu nayo,leo hii nchi jirani ikitaka kumega hekta moja tu Kutoka kwetu hatutakubali, tutapigana Kufa kuilinda.
Kusema kwamba JMT si kitu chochote ni upogo wa fikra.
 
Binafsi sioni kama kuna tatzo maana tumezoea kuona kila utawala ukija na SLOGUN yake kama;

A) Ujamaa na Kujitegemea...

B) Ruksa...

C) Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe...

D) Maisha bora kwa kila mtanzania....

E) Hapa kazi tu...

........ na hapo katikati tumekosa kosa MAISHA NA BATA.[emoji23][emoji23][emoji23]..!!

F) Na sasa tunasalimiana ktk jina la jamuhuri ya muungano
Umeaniacha mkuu kwenye neno SLOGUN; umemaanisha nini?
 
Binafsi hii salamu ndio ilitakiwa kutumika miaka yote. Ni salamu nzuri inayojumuisha watanzania wote wenye dini na wasio na dini. ... Kwa nyongeza tu ni unafiki kusema salamu aleikyumu wakati huamini kwenye uislamu hivyo hivyo ni unafiki kusema bwana Yesu asifiwe wakati huamini Yesu ni mwana wa Mungu.

Mama ni intelligent na wewe ni kilaza hivyo usimbishie.
 
Umeongea pumba kishenzi. Binafsi hii salama ndio ilitakiwa kutumika miaka yote. Ni salamu nzuri inayojumuisha watanzania wote wenye dini na wasio na dini. ...Kwa nyongeza tu ni unafiki kusema salamu aleikyumu wakati huamini kwenye uislamu hivyo hivyo ni unafiki kusema bwana Yesu asifiwe wakati huamini Yesu ni mwana wa Mungu. Mama ni intelligent na wewe ni kilaza hivyo usimbishie.
Kuna watu wameshajiaminisha kuwa nchi hii kuna dini mbili pekee.

Kwasababu dini nyingine ni watu wakimya na hawapendi migogoro, wanawachukulia kama hawapo.
 
Back
Top Bottom