Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Kusalimu kwa kusema"kidumu chama cha mapinduzi" inawezekana ila kwa kuwa ni raisi wa TZ , Jamhuri ya muungano ni salamu sahihi. Big up Mama.
 
Ni tatizo kwa wengine na sio lazima Kila unachokifikiri wewe kuwa sawa basi iwe Kwa kola mtu,

Lazima pia ujifunze kukubali fikra za wengine,

Nchi huru hii.

Na kwa taarifa yako tu , thread hii inawakilisha mawazo ya wengi tu, ingawa wengine hawataki kusema.

Ukweli unapotakiwa kusemwa usemwe.

Anza kwa kukubali wazo la mama la salamu mpya. Nchi huru hii.

Fanya sensa ya kutathimini wachangiaji wanashauri nini kwenye hoja yako.
Huwezi kusema wengi wakati huna data.
Hata wawili ni wengi. Data huongea zenyewe.
 
Mh. Rais Samia ,

Naamini unafahamu kabisa kuwa, Mwaka 2020 wakati tunampigia kampeni Dr. Magufuli, tulikupigia kampeni na wewe ukiwa mgombea mwenza.

Tuliwaamini nyote wawili kwamba ni watu sahihi kuliongoza Taifa letu.

Sasa wewe ni Rais wetu, hakuna ubishi katika hilo.

Sasa Mh. Rais napata ukakasi kidogo kwa kauli zako , Kila unapotusalimia,

Huyu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unayemtaja ni nani hasa,

Maana ninavyofahamu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayotokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Sasa hakuna mtu, kitu, watu, vitu kwa jina hilo.

Ingawa naelewa kwamba unataka usionekane kuwa unapendelea Dini yeyote,

Lakini Bado Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Haina hadhi ya kutajwa Kwa jina.

Sio sahihi kuipa hadhi hiyo.

Serikali Haina dini, lakini sisi raia tuna dini zetu, na hatumfahamu huyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh. Rais, salami hii, inatufikirisha mno sisi wengi,

Unaweza usiambiwe ILA Kuna haja ya kuachana nayo.

Wasalaaam,

Statesman,

Dar es Salaam.
Aaahh..we kijana suala dogo kama hilo linakushinda kulichambua!! Sasa u DC utauweza kweli..nasikitika kukwambia kwamba hautakuwepo kwenye mkeka!
 
Aaahh..we kijana suala dogo kama hilo linakushinda kulichambua!! Sasa u DC utauweza kweli..nasikitika kukwambia kwamba hautakuwepo kwenye mkeka!
Na ndio ajira zilizobakia Kwa sasa hakuna nyingine.
 
Nasisitiza, “Ni unafiki kusema Bwana Asifiwe, kama huamini Yesu ni mwana wa Mungu!” Naongeza pia, ukisha Sema Bwana Asifiwe, ukisema asalam aleykum, unakanusha ulichosema mwanzo and vise vesa!

Aliyekataa hizo salamu na kuibua hii ya JMT ndiye huyohuyo aliyekuwa akiwaongoza raia deile kusema ^Mwanga wa milele umwangaziee Ee Bwana, apumzike kwa amani^ Sijui unanielewa kweli!???
 
Nawasalimu kwa jina la "Marekani"

Nawasalimu kwa jina la "Indonesia"

Nawasalimu kwa jina la "Nigeria"

Nawasalimu kwa jina la "Uturuki"

Hapo vipi
 
Akili ndogo inahangaika na mambo ya kitoto.

Serikali ilichepusha 1.5 trillion shillings bila maelezo ya kueleweka. Watu walipiga kimya tu hapa... leo wanataka tujadili salamu
 
Nawasalimu kwa jina la "Marekani"

Nawasalimu kwa jina la "Indonesia"

Nawasalimu kwa jina la "Nigeria"

Nawasalimu kwa jina la "Uturuki"

Hapo vipi

Poa sana.
Hujui kuwa unaimarisha umuhimu wa jina husika kwa wahusika. "Kidumu chama cha mapinduzi" Hapo vipi?
 
Mkuu hii salamu Haina msingi wa kuitegemea.

Huyo Jamhuri hafahamiki ni nani.

Kwanini Rais anahofia kusalimia wananchi Kwa kuzitambua dini zao au tamaduni zao??

Kama anaona soni kusema Asalam Aleykum au Bwana Yesu Asifiwe basi aseme tu Habarini za saa hizi ma bibi na mabwana.

Huyo Jamhuri ndio nani??
Kikubwa Kayafa Hamnazo kafa hayo mengine ni madogo na yanavumilika
 
Rais ajitahidi tu kusema Bwana Yesu asifiwe, maana ukishakua kiongozi unakua kiongozi wa wote,

Ila kusema nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Kwa hapa nyumbani Tanzania hiyo sio salamu.
Miaka yote ya uongozi wake alikuwa akisema na kusalimia kawaida, sasa tangu ile Machi juzi amestuka nini!???
 
Akili ndogo inahangaika na mambo ya kitoto.

Serikali ilichepusha 1.5 trillion shillings bila maelezo ya kueleweka. Watu walipiga kimya tu hapa... leo wanataka tujadili salamu
Shangaa na wewe mkuu. Mleta mada alishindwa kuhoji vitu vinavyowagusa watanzania wakiwemo wazazi wake kule Isanga mwalugesha lakini leo hii anahoji salamu. Cha ajabu zaidi salamu haina tatizo lolote ila uelewa wake ndio wenye shida ila bado hilo halioni.
 
Kwa kifupi hii salamu siipendi hata kidogo. Kwanza imechakachua salamu yetu wakristo. Ingetungwa tofauti nisingekuwa na neno. Sisi yetu ni "Nakusalimu kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo", Sasa hii ya huyu mama imechakachua salamu yetu.
Itoshe tu kusema tunaabudishwa tusichokijua

mama D
 
Kikubwa Kayafa Hamnazo kafa hayo mengine ni madogo na yanavumilika
Mkuu ondoa neno "kuvumilika". Hii salamu haina shida yeyote, in fact ni salamu nzuri na yenye maana kubwa sana kwa watanzania wote. Haibagui dini, kabila, rangi wala ukoo zaidi inahamasisha uzalendo, kutuunganisha na kutukumbusha kuwa ardhi ya Tanzania ndio ardhi pekee tunayotakiwa kujivunia.
 
Mkuu hii salamu Haina msingi wa kuitegemea.

Huyo Jamhuri hafahamiki ni nani.

Kwanini Rais anahofia kusalimia wananchi Kwa kuzitambua dini zao au tamaduni zao??

Kama anaona soni kusema Asalam Aleykum au Bwana Yesu Asifiwe basi aseme tu Habarini za saa hizi ma bibi na mabwana.

Huyo Jamhuri ndio nani??
Ni nchi anayoiongoza
 
Unasalimiwa kwa jina la nchi yako unapoishi mjomba, mambo mengine siyo lazima u complicate ninyi ndio mnafanya maisha yaonekane magumu sana. Ni kuhooooji ni kuhooooji hata vitu visivyo haja ya kuhoji.
 
Huyu hajaanza kusikika leo au juzi

Ukitaka kumjua nenda kangowe au kaharibu
Mali yoyote ya serikali utamjuwa mkuu

Ova
 
Mbona hamlalamiki mtu akiapa " Naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nitaitumikia kwa moyo wangu wote..."

Hadi hapo humjui Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
 
Back
Top Bottom