Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Katika kitu cha busara alichofanya Raisi wetu ni kubuni salamu hii ambayo nitaomba iendelezwe kwa mustakabali wa diversity zetu.

1.Zamani tulikuwa tukiambiwa nchi haina dini lakini kiongozibanasimama na kuanza kusalimia salamu za dini mbalimbali nusu saa

2. Mwingine kwa makusudi , kwenye hadhira yenye watu wengi anasalimia salamu moja tu ambayo inatumika kwenye dini yake wakati kuna mkusanyiko wa watu wengi watu wakilalamika anajitetea kwa kutoa tafsiri ya maana ya salamu hiyo ya kigeni kuwa ni nzuri tuu

3.Hata akisalimia kwa salamu zote bado swali lilikuwa ninaulizwa kwa nini kaanza kutaja salamu ya dini yake? Haya mambo yalileta mkanganyiko mkubwa na kuonyesha kwamba tunadharauliana na kuna watu waliona dini zao ni subprime over others

4.Nashauri salamuu hii ya kizalendo itumike sehemu zote zenye hafla za kiseriksli na za kijamii na kwa watu wote wenye itikadi tofauti

5. Salamu za kidini zibaki kwenye nyumba za ibada husika au kwa watu wanaojuana wana imani moja wanapokutana

HONGERA SANA MH. RAISI WANGU KWA UBUNIFU HUU
 
Ya Kaisari mwachie Kaisari...,

Hizo Salamu zenu mkipeana huke mehakaluni, makanisani, masinagogi, kwenye mapango au mkiwa na mizimu yenu kwani haitoshi ?
 
Mh. Rais Samia ,

Naamini unafahamu kabisa kuwa, Mwaka 2020 wakati tunampigia kampeni Dr. Magufuli, tulikupigia kampeni na wewe ukiwa mgombea mwenza.

Tuliwaamini nyote wawili kwamba ni watu sahihi kuliongoza Taifa letu.

Sasa wewe ni Rais wetu, hakuna ubishi katika hilo.

Sasa Mh. Rais napata ukakasi kidogo kwa kauli zako , Kila unapotusalimia,

Huyu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unayemtaja ni nani hasa,

Maana ninavyofahamu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayotokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Sasa hakuna mtu, kitu, watu, vitu kwa jina hilo.

Ingawa naelewa kwamba unataka usionekane kuwa unapendelea Dini yeyote,

Lakini Bado Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Haina hadhi ya kutajwa Kwa jina.

Sio sahihi kuipa hadhi hiyo.

Serikali Haina dini, lakini sisi raia tuna dini zetu, na hatumfahamu huyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh. Rais, salami hii, inatufikirisha mno sisi wengi,

Unaweza usiambiwe ILA Kuna haja ya kuachana nayo.

Wasalaaam,

Statesman,

Dar es Salaam.

JMT ni Tanganyika full stop 🛑
 
Aliyekataa hizo salamu na kuibua hii ya JMT ndiye huyohuyo aliyekuwa akiwaongoza raia deile kusema ^Mwanga wa milele umwangaziee Ee Bwana, apumzike kwa amani^ Sijui unanielewa kweli!???
Kwani Mtu yeyote akisema, “mwanga wa milele umwagazie ee Bwana, apumzike kwa amani!” Ndiyo Bwana kweli atasikia na kufanya hivyo?!
 
Kwani Mtu yeyote akisema, “mwanga wa milele umwagazie ee Bwana, apumzike kwa amani!” Ndiyo Bwana kweli atasikia na kufanya hivyo?!
You got it!!! Kama ni suala la maneno tu na halina effect yoyote (and it's true), kwa nini aitumie, hata!??? Likewise, kama haina athari na ameitumia, kwa nini zile zingine asitumie!??? Hivi hiki si kitendo cha wazi cha ^madarasa mawili^ (double standard)!??? By the way, everybody knows what she has been actually using before she took over the reigns of government.
 
Una point hapo. Sasa Rais lazima kupenda na kuheshimu dini za wananchi wote. Basi anagalau abadilishe kidogo aseme ""Msifuni Yesu Kristu!"
Mmeanza kuwabagua wengine kidini eee?!!!

Sikutegemea SKY ECLAT mtu mwenye fikra TUNDUIZI akumbatie hayo masuala KOKO ya ubaguzi wa KIDINI......

Sijui sisi waafrika tuna matatizo gani ?!!! 🤣🤣

Yaani unaweza kukuta hata PROFESA lakini bado tu akawa na mihemko KOKO ya Mambo ya kidini na ubaguzi wa KIDINI kwa wengine.....PATHETIC.....

#NchiKwanzaKablaYaChochote
 
Spiritualy hii salamu sio salama, tunafahamu jina la jamhuri ya muungano wa tz lilipatikana baada ya kuchanganya udongo wa tanganyika na zanzibar kwenye chungu na kisha ukatupwa chini ya bahari ya hindi ukinuizwa manuizo ya kimiungu.

U never know,inaweza salamu hii ina inspiration ya marine evil spirit,hatujui consequences zake, lakini mwisho wake sio mzuri.

Bora salamu za dini zetu zitajwe,maana katika salamu hizo lazima yumo Mungu wa kweli anatajwa kati ya hao wasio wa kweli.
 
Binafsi hii salamu ndio ilitakiwa kutumika miaka yote. Ni salamu nzuri inayojumuisha watanzania wote wenye dini na wasio na dini. ... Kwa nyongeza tu ni unafiki kusema salamu aleikyumu wakati huamini kwenye uislamu hivyo hivyo ni unafiki kusema bwana Yesu asifiwe wakati huamini Yesu ni mwana wa Mungu.

Mama ni intelligent na wewe ni kilaza hivyo usimbishie.
Pia hapo anajaribu kuondosha migawanyiko iliyochochewa kwa makusudi na kundi fulani,hivyo wote waliobaguliwa na wasiobaguliwa watajisikia wote no wamoja na kazi iendelee.
 
Jambo dogo mnalikuza ilimradi tu kuonyesha udhaifu wa mama... sijui mnapata nini?
Jambo dogo sana. Mama muislam na hajisikii amani kuanza kusema Bwana asifiwe.

Ni salam yenye mantiki ya kukumbusha kuwa hapa kazi tu inao muendelezo ambao ni kazi iendelee.
 
Spiritualy hii salamu sio salama, tunafahamu jina la jamhuri ya muungano wa tz lilipatikana baada ya kuchanganya udongo wa tanganyika na zanzibar kwenye chungu na kisha ukatupwa chini ya bahari ya hindi ukinuizwa manuizo ya kimiungu.

U never know,inaweza salamu hii ina inspiration ya marine evil spirit,hatujui consequences zake, lakini mwisho wake sio mzuri.

Bora salamu za dini zetu zitajwe,maana katika salamu hizo lazima yumo Mungu wa kweli anatajwa kati ya hao wasio wa kweli.
Unao ushahidi upi kama hiyo miungu mingine haina ukweli ndani yake kwa hao wanaoiamini?. Ni bora kuachana na hii hulka ya kujiona tuna haki kuliko wengine.
 
Mh. Rais Samia ,

Naamini unafahamu kabisa kuwa, Mwaka 2020 wakati tunampigia kampeni Dr. Magufuli, tulikupigia kampeni na wewe ukiwa mgombea mwenza.

Tuliwaamini nyote wawili kwamba ni watu sahihi kuliongoza Taifa letu.

Sasa wewe ni Rais wetu, hakuna ubishi katika hilo.

Sasa Mh. Rais napata ukakasi kidogo kwa kauli zako , Kila unapotusalimia,

Huyu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unayemtaja ni nani hasa,

Maana ninavyofahamu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayotokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Sasa hakuna mtu, kitu, watu, vitu kwa jina hilo.

Ingawa naelewa kwamba unataka usionekane kuwa unapendelea Dini yeyote,

Lakini Bado Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Haina hadhi ya kutajwa Kwa jina.

Sio sahihi kuipa hadhi hiyo.

Serikali Haina dini, lakini sisi raia tuna dini zetu, na hatumfahamu huyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh. Rais, salami hii, inatufikirisha mno sisi wengi,

Unaweza usiambiwe ILA Kuna haja ya kuachana nayo.

Wasalaaam,

Statesman,

Dar es Salaam.
Kuna chochote unachopoteza?
 
Huyu nguchiro anasumbua watu tu,cjui hoja yake nn????nchi ili iwe nchi lazma iwe na watu
Hebu pitia tena wimbo huu:
Tanzania, Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote...
Jiulize ni nani huyu unayempenda.
Sasa rejea hii salam. Nawasalimia kwa jina la jamhuri....
Kuna tofauti gani kimsingi.
Hapa ni kuiweka nchi mbele kama ndio focus kwa kila jambo tunalofanya (kazi) ili kuleta ustawi wa nchi, watu wote.
JMT ni nchi, ni watu waishio humo na ndiyo tunayoijenga.
Tuangalie nia ya salam na sio tafsiri.
Kama tukichambua "hapa kazi tu" tungekuta makosa mfano, hata vibaka, changudoa, majambazi wanaweza kusema hapa kazi tu.
So, tuangalie nia na sio tafsiri za kukomoa!
 
Hadi kwa jambo hilo nalo mnajitoa ufahamu..aisee mataga tutaanza kuwazaba makofi sasa
 
Mama piga kazi ,mikumi tena ,kazi iendelee kwa jina la jahmuri ya muungano wa tanzania.
 
Back
Top Bottom