Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani huyu?

Mbona sioni watu wengi masokoni na sehemu nyingine mitaani wakisalimiana Tumsifu Yesu Kristu au Asalamaleku
Ndiyo maana Bi Mkubwa wako akashauriwa atumie salamu zingine mbadala kwa vile ziko nyingi tu. Unapopindisha lugha kama anavyofanya hapa kwenye salamu yake ya JMT, ni wazi huo ni mwelekeo wa kukufuru.
 
Hii salamu nzuri sana jwa sababu hizi.

1. itaondoa zile zinqzohusishwa kidini na kiutqmaduni fulani kama "Asalaam aleikum, bwana asifiwe".

2.Ni salamu moja inayomuunganisha kila Mtanzania anayeitqmbua na kuikubali n hi yake.

3. Inaonesha focus ni utaifa, si mtu binafsi kama Mfalme fulani, au chama tawala/ upinzani.Kwenye mikutano ya kitaifa mqthalan, kumsikia rais anasalimia kidumu chama cha Mapinduzi kunaweza kukera wapinzani. Lakini hii ni salamu ya Watanzania wote.Zaidi, katika zama hizi za mmomonyoko wa umoja wa kitaifa, salamu itawakumbusha Watanzania umoja wao katika Utanzania.

4.Ni salamu ya usawa.Yeyote anaweza kumsalimia yeyote, haina utata wa salamu kama Shikamoo ambayo mdogo anamsalimia mkubwa kuitoa inabidi uanze kupiga mahesabu.

5. Inakata mlolongo wa salamu ndefu na nyingi ambazo zinapoteza muda tu.
 
^We can easily forgive a child who is afraid of the darkness; the real tragedy of life is when men and women are afraid of the light.^ ~ Plato.
 
Mnaumia kwa vitu vidogo sana. Badala mlalamikie kuanzishwa kwa vyuo hata vya kujifunza kutengeneza pembejeo, manalilia salamu za makanisani na misikitini.

Mkisalimiana jumapili na ijumaa si inatosha
 
Si salamu mbaya.

But I’m a ‘keep it plain and simple’ kinda guy.

Kwangu ‘habari ya leo mabibi na mabwana’ naona inatosha kabisa.

Pia, yaweza kuwa modified kuendana na muda. Yaweza kuwa ‘habari za asubuhi, mchana, au jioni’.

Sijui ni lini tu tulienda huko kwenye mambo ya bwana asifiwe na asamaleko!

Halafu na yale mambo ya kutaja mlolongo wa viongozi wote waliopo!

Kupoteza muda tu.

Pia, ingependeza kuona [viongozi] wanaacha kurundikana wote sehemu moja.

Maana ipo yawezekana wote wakamezwa na li sink hole halafu taifa likakumbwa na sintofahamu.
 
Huwa najiuliza hivi salamu ya "CCM Oyeee! Ina maana inamaana gani?
 
Kwani ukiambiwa za asubuhi huyo za asubuhi atakuwa ndo Mungu?
 
Kwa kifupi hii salamu siipendi hata kidogo. Kwanza imechakachua salamu yetu wakristo. Ingetungwa tofauti nisingekuwa na neno. Sisi yetu ni "Nakusalimu kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo", Sasa hii ya huyu mama imechakachua salamu yetu.
Nimetamani kukupa like tatu kwa wakati mmoja.
 
Hamna dogo nyie akianza kusalimu kwa “ asalaam alleykum “ halafu “ tumsifu yesu kristo “ mtasema kwa nini anaanza kuwasalimu waislam.Bora atusalimu kwa Jamhuri na kazi iendelee.
 

Hiyo salama ya JMT haijakaa poa kabisa.
 
666
 
Hii ni kujaribu kukwepa kutamka neno Bwana kwa waprotestanti au Yesu Kristo kwa wakatoliki
 
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni watanzania wote kama taifa.
 
Ukisalimiwa salamu ya dini yako ndio unaona umeheshimiwa?
Asalimie kwa salamu za dini za Watanzania kama alivyofanya mtangulizi wake na hiyo iwe ndiyo sala ya kufungua mkutano. Hakuna haja ya kuwaita viongozi wa dini wasali tena. Tunapoteza muda kwani wanatoa hotuba badala ya sala fupi.
 
Labda hujasoma vizuri. Tumeshauri asalimie kwa kutumia salamu za dini kuu zote. Au maelezo ya nyongeza umeyachukulia kama ndiyo kitu chote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…