Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
Demokrasia ni kitu kibaya sana kwa binadamu. Ni kama kujenga ukommunisti. Vinasound good na humane kwenye makaratasi, kiuhalisia ni vitu hatari kwa ustawi wa binadamu.Pamoja na kazi nzuri ya kufasiri kazi ya Plato, lakini huyo Plato alikuwa akielimisha zaidi kuhusu utawala wa kimabavu kutoka kwa kiongozi mwenye kuhodhi mamlaka (totaritarian) zote dhidi ya wale wanotawaliwa.
Na pia alikuwa akilalia zaidi kwa upande wa siasa za nchi za magharibi.
Lakini moja ya mambo ya muhimu kabisa kwa hayati Mwalimu Nyerere na kazi za Plato ni kufuata mawazo (ideas) ya Plato kwamba wajenga mfumo mzuri wa sheria na haki na usawa katika jamii unoiongoza na hapo ndo tumeona jinsi alivyoweza kuunda mifumo kadhaa chini ya uongozi wake kuanzia mahakama, bunge, ulinzi na usalama hadi kwenye mfumo wa chama kimoja ambao ulimwezesha kutawala kirahisi kwasababu alikuwa ana "access" ya kufahamu nani ni nani na nani kasema nini.
Na hilo ndo linotusumbua leo kwa haya tunoyaona yanotokea nchini kwa sasa.
Hivyo Plato sidhani kama alikuwa ni mtu sahihi wa kufuata na kuyatumia au kuyaiga kila aloyaandika kwani yapo ambayo leo hii yatatiza kuyafuata.
Kuna mmoja wa wakosoaji wazuri tu wa kazi za Plato aitwa Karl Popper alieandika kitabu chake kiitwacho "The Open Society and Its Enemies"alokiandika mwaka 1945. Popper amedai kwamba Maandishi ya Plato ni ya yale yaitwayo Dystopia yaani kinyume na Utopia kwamba Plato hakuwa akiamini katika demokrasia na ubinadamu kwani alikuwa aliamini katika kuhodhi madaraka na kuunda utawala ulowakandamiza wale watawaliwa.
Popper pia amemtofautisha Plato na Socrates kwamba Socrates ndiye aliefaa kuigwa kwa kazi zake za kuhoji khasa mawazo ya Plato.