Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kamwe usije thubutu kuuza eneo lako ,kwa mambo ya ndoa ,siku akija kukuudhi huyo mwanamke utajutiaMm nin 34 had sasa cjaoa na. Sijui nitaoa Lin mamb Ni mengi nafanya vibarua kupata pesa ila mungu asimame mwakani nioe nitauza hats kiwanja changu nipate hela za kuoa mnk wazaz hawnielewi kbsa. Hvy nitauuzakiwanja kimoja nipate pesa za kutoa mahar na Pete ipatikane ..kuhusu demu nafikiri kumtafuta .wingine mnk nilianee. Kwao wako vxr ila wanazarau hvyo ctamuezaa
Kijn pmbna watu kazkzn wanataka pesa sana wazaz Kama huna pesa watakuzarau
una mtoto?Bila shaka unatokea mkoa wa kigoma,nilienda kusoma diploma kila kijana alkuwa ameoa na wapo chuo na wameacha wake zao nyumban,mim nna miaka 30 lakin wazazi wangu hasa baba huwa wanasema mim bado Mdogo pale iktokea mtu kawauliza kwann sjaoa
Sina Mtoto,Niko makini kutumia kondom na kujua mienendo ya hedhi ya demu ninae kuwa nae,sometimes huwa nakuwa na mahusiano na wanawake wenye mimba ili nfaidi nyama nyama pasipo kuwa na shaka ya kutengeneza ujauztouna mtoto?
kwaiyo matarajio yako kupata mtoto ni mwaka gani???? maana mwenzio hapo anadai kuwa umri unamtupa mkono na hana familia (mke wala mtoto)Sina Mtoto,Niko makini kutumia kondom na kujua mienendo ya hedhi ya demu ninae kuwa nae,sometimes huwa nakuwa na mahusiano na wanawake wenye mimba ili nfaidi nyama nyama pasipo kuwa na shaka ya kutengeneza ujauzto
Mtoto nahtaj mmoja tu kwa ajili ya kuwaonesha wanazengo kuwa nko vzur,kwahyo nazan nikifika 40 ndo utakuwa wakat mzurkwaiyo matarajio yako kupata mtoto ni mwaka gani???? maana mwenzio hapo anadai kuwa umri unamtupa mkono na hana familia (mke wala mtoto)
Nakuunga mkono huo ndo uhalisia..Kama unampenzi Yuko chuo hakuna utachoambulia...jamaa angu pamoja na kumhudumia Dem wake na kumwambia siku akimsaliti atajiua lakini haikusaidia mpaka Sasa binti hataki mazoea nae keshakutana na mabishoo hakumbuki Tena..Ingekuwa mim ningempa mimba tu inshu ni mtoto ndoa c lazma saaana kwasisi wahangaikaji.Ni kweli mkuu lakini Kama umefika chuo utaelewa Nini namaanisha chuo Kuna stunts nyingi mnoooo ni Bora kumwambia ukweli ajiandae kisaikolojia
Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Safi sana mkuu. Tuzidi kupeana moyo katika safari hii ndefu ya maisha.Pole Mkuu... Sio yoote tunayopanga yatafanikiwa muda huo Huo. Endelea kufanya kazi kwa bidii huku ukimuomba Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi.
Hakuna kubwa kwa Mola
Kukiri sio Sababu people's change ni Bora kumueleza pia negative side ilivyo Ili apunguze expection karibia members wote tuliopo humu jf tuliwahi kuwa na wapenzi na waliwahi kuweka viapo kuwa Wana tupenda na hawato tuacha lakini kilicho kuja kutokea Kila mtu anajua mwenyewe [emoji16][emoji16]Nishapita huko naelewa sana mkuu. Demu kakiri anampenda jamaa na hajari hali yake kwasasa na jamaa nae kakiri kuwa anampemda demu. Demu ni lazima aende chuo hakuna alternative nyingine and the guy is psychological tortured because he is ain't in a position to change the situation sasa huu ni ujinga kuwaza kitu ambacho huwezi kukifanya kwasasa. Ndiomana namwambia ili aweze kuyaacomodate hayo yote aendelee kufanya vibarua vyake huku akitafuta ajira akifanikiwa hofu aliyonayo itapotea na mambo yataenda vizuri.
Eimeen [emoji120] huu ushauri mzuri sanaMiaka 30 bado mtoto sana
Bill gates alioa akiwa na miaka 40
Jitulize..achana na haraka..
Binti nenda nae hadi itakavyokuwa..
Usianze fanya maamuzi Kwa hofu
MKuu,unafikiria Sana mkuu.eti ulishwahi Kua namapenzi kisha akasafiri kwenda dar???!!!! comment fikirishi nachonganishi Sana hii.Ulishawahi pendana na mtu then akaenda dar[emoji23][emoji23][emoji23]
Ngoja nikusaidie kukufumbuwa macho, binti anataka harusi na hataki ndoa, Sasa chaguo ni lako na wewe unataka nini?Habarini ndugu zangu, naombeni niwape mkasa wangu kidogo ili walio nizidi umri na wenye busara wanishauri kwenye ili ninalopitia, maana nina ongozwa na mawazo sana na nashindwa kuiona kesho yangu ilio bora
Kwanza kabisa umri wangu ni miaka 30 kwa sasaivi, nimetokea katika familia ya ufukara mkubwa (ata elimu yangu ya o-level nilisomeshwa na wilaya kitengo cha elimu), nina mpenzi ambaye nimekaa nae kwenye mahusino miaka 5 sasaivi (nimetangulia kusema ivyo vitu viwili ili nielezee kinaga ubaga kinachonisibu)
Mpaka muda huu wa miaka iyo 30 sina familia (sina mtoto), rafiki zangu wengi wameoa, wana watoto na familia zao ila kwa upande wangu imekuwa tofauti kidogo, kwa huu umri nilionao napata ujumbe mwingi sana kutoka kwa marafiki na baadhi ya ndugu kuniuliza vipi nafikilia nini kuhusu kuwa na famili (nabaki na mawazo ndugu zangu)
Ndugu zangu muda mwingi katika maisha yangu nimeutumia shuleni, nilipomaliza form-four sikubahatika kuchafaulu kwenda advance level, ilinibidi kufanya vibarua vya hapa na pale na kuweza kufanikisha kupata pesa ya kusoma level ya certificate, baada ya kumaliza certificate nikaanza kupambana tena na vibarua vya hapa na pale kwa mwaka mzima na kupata pesa ya kusoma diploma, baada ya kumaliza diploma katumia tena mwaka mzima kupambana kufanya vibarua na kupata pesa ya kusoma degree (nashukuru mungu kwa level ya degree nilipata mkopo wa asilimia 96%) na zile pesa zilinsaidie kwenye mambo yangu mengine
Nilimaliza chuo level ya degree mwaka 2018 (mpaka ivi sasa bado natafuta ajira bila mafanikio yeyote yale)
Kwa sasa najifanyia vibarua vyovyote vinavyokuja mbele yangu, iwe ni kuchimba misingi ya nyuma, kukusanya kuni na kuuza kwa wakaanga samaki, kuchotea watu maji, na kadhalika (nk).
Nimeishia kupata ela ya kula tu, jamii, marafiki, ndugu wakiniambia kuhusu kuoa uwa wananiweka kwenye wakati mgumu sana nashindwa la kufanya.
MAHUSIANO.
Nina girfriend wangu nilikutana nae kipindi nasoma diploma mwaka wa mwisho yeye akiwa anasoma form 5 (PCB), akuweza kuendelea hakuweza kubahatika kwenda levele ya degree alienda kusoma diploma baada ya kumaliza from six, na alimaliza diploma mwaka jana mwezi wa 10.
mimi na uyu bnti tumepitia up and down nyingi sana, mwaka jana niliisi mwenzangu amebadilika baada ya kuona mawasiliano yetu hayapo kama kipindi cha nyuma, na nilikuwa nikimuuliza mwenzangu anakuwa mkali sana, ilinilazimu nimuache uku nikiwa na uchungu sana moyoni maana ni binti niliyempenda sana sana (kumbuka wakati nipo nae uyu binti muda wote huo ndugu zake nilikuwa nawaona kwenye picha tu akiwa-post), ila rafiki zake baadhi nilikuwa nawafahau, baada ya kuaamua kukaa pembeni (nilifuta mawasilino yake kabisa) baada week 3 alikuja kunitafuta, aliniomba msamaa kwa yaliotokea na nikamsamehe kabisa tukaendelea na mahusiano mpaka ivi sasa
mwaka huu mwezi wa saba aliniomba niende kwao nikaonanae na ndugu zake, nikamuone baba yake na mama yake (ndugu zangu nilipata kama woga flani ivi, maana sikutegemea awe na ughafla wa kuniambia vile) ni kweli nampenda aswaaa, alianza kunipa simu niongee na mzazi wake wa kike (mama yake) alisema ameshamuambia mama yake kuwa mimi ni rafiki yake
Kuna siku mama yake aliniambia ni lini nitakwenda kuwasalimia (maana wazazi wake wanakaa mkoa wa kaskazini), nilimpanga tarehe ya kwenda kuwasalimia, tarehe ikafika nikafika kwao, nilipokelewa vizuri sana sana sana, nilitambulishwa kwa ndugu zake wengi tu. sikuwahi kufika kwa yule binti ila baada ya kufika nikajionea mwenyewe, kwao ni watu wenye uwezo kifedha, kifupi wanajimuda aswaa, nikaanza kama kukosa confidence ivi.
Mwezi huu uyu binti anakwenda kusoma chuo kikuu, matokeo bado hayajatoka ya chuo (selection),
uyu binti tangu nimeenda kwao ni mtu ambaye ametokea sana kunipenda zaidi ya kipindi cha nyuma kabisaaa, kila ninachosema kwake anakuwa yupo tayari, ila issue inakuja kwenye mambo yafuatayo.
anakwenda kusoma chuo (hapa pananiogopesha kama penzi letu litaendelea kudumu)
kuhusu kumuoa yupo tayari kabisaa ila tatizo linakuja upande wangu sina kazi kabisa kwa sasa (nabagaiza sana sana) kwenye miangaiko yangu kupata ela ya kula
ila pia anaonyesha kuitaji japo sana sana sherehe, hapa napo pananipa mawazo
Mpaka sasaivi ni binti amekuwa akiniheshimu, akinisikiliza tunahishi vizuri sana pasipo shida yeyote ile, ni binti amabaye uwa ananitamkia maneno haya "Siitaji pesa wala kitu chochote kutoka kwako, ila nahitaji tuje kuishi maisha mazuri, pambana unavyojua ki-alali kikubwa tuje kuishi maisha mazuri" aya maneno yake uwa yanazunguka sana kichwani mwangu.
Kuna muda pia nawaza, nimuache nikatafute binti mwingine uko nyumbani kwetu nianze nae maisha kwa kuoana kwa kutoa maali tu kwao, nianzishe familia kuliko kuanza kusubiliana na uyu ambaye kwanza anataka sherehe (ananisikiliza kote ila kwenye kufunga ndoa ambayo sherehe akuna anaonekana kutokuwa tayari).
nampenda sana sana, ila kuna muda nakosa amani binafsi, umri unakimbia sana ndio kitu kinanipa mawazo pia.
samaani kwa uzi mrefu, mbarikiwe