Ok.
Tumalizie hiki kipande kidogo.... Cloning biological engineering ni teknolojia ya kurekebisha mifumo mbali mbali katika mwili wa kiumbe hai ili kiweze kuwiana na mazingira ya sayari husika. Hii ndiyo kazi tunayoiona katika masimulizi ya kitabu cha Mwanzo katika Biblia.
Anayetajwa pale kuwa Mungu tofauti na fungu la kwanza, siye hasa Mungu bali viumbe kutoka anga za mbali, yaani Jamii ya Lyran Humanoids. Viumbe hawa wenye ujuzi mkubwa wa teknolojia mbali mbali ndio waliootesha uhai hapa duniani kutokea sayari yao. Kilichofanyika pale sio uumbaji hasa wa viumbe wasiowahi kuwepo bali ni uoteshaji wa viumbe waliopo katika sayari nyingine ya mbali.
Michakato yote iliyofanyika pale ni jinsi ya kupangilia mambo katika mpango sawia unaowiana na sayari dunia. Majira na nyakati duniani , hali mbali mbali za hewa zingeweza kuwa ni tofauti kwa kiasi fulani na hivyo kuwa na athari kadhaa kwa viumbe hao endapo wangepandikizwa hapa duniani bila kupitia cloning biological engineering. Kwa hiyo cloning biological engineering ni teknolojia inayosaidia kiumbe hai kutoka sayari moja kufanya sayari rafiki kuwa sayari ya nyumbani.
Tafsiri ya baadaye ya kitabu cha Mwanzo ndiyo iliyobadilisha uelewa huu wa michakato iliyoendelea katika sura hiyo. Kwa mfano neno "Bara" katika lugha ya kiebrania yaani "kuumba " lina maana ya kutokeza kitu kipya kisichowahi kuwepo kabisa. Lakini neno la kiebrania "Asah" yaani "kufanya" maana yake ni kupangilia kitu kilichopo ili kiwe katika muundo unaohitajika. Maneno ya kiebrania kama Elohimu jina lenye wingi wa neno El, kuonesha viumbe wahusika kwamba walikuwa wengi Maneno kama, tufanye mtu kwa sura na mfano wetu - Mwanzo 1:26,na maneno, Mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya-Mwanzo 3:22, kauli inayoonesha kwamba walikuwa wengi na wenye kuhesabika mmoja mmoja. Maana wakasema amekuwa kama mmoja wetu.
Aidha binadamu akawa kama mmoja wao kwa kujua yaani ujuzi, kuonesha kwamba tofauti yao na binadamu ilikuwa katika ujuzi. Kwamba viumbe hawa walikuwa ni Wenye miili kama sisi kwa maana ile kauli iliyoahidi hukumu ya gharika kuu inasema, sitashindana na binadamu milele maana yeye naye ni nyama Mwanzo 6:33. Sasa angalia maneno , " Yeye naye ni nyama " kuonesha kwamba hata msemaji wa maneno hayo naye alikuwa ni nyama. Na kwa sababu ni nyama ndiyo maana viumbe hawa waliwahi kumtembelea Ibrahim akawachinjia wakala - Mwanzo 18:1-9. Tunaambiwa kwamba Yakobo alishindana na mmoja wa viumbe hawa mieleka na Yakobo ndiye aliyeshinda Mwanzo 32 :24 - 30.
Viumbe hawa pia kama viumbe walikuwa na mipaka, kwa mfano Adamu alipojificha kiumbe aliyemtembelea hangeweza kumuona kwa hiyo aliuliza Adamu uko wapi? Mwanzo 3:8-11. Je unakumbuka wanadamu walipojenga mnara viumbe hawa walisema na tushuke tuwachafulie msemo wasielewane maana pengine jengo lao hilo refu lingeweza kusababisha madhara makubwa endapo lingeanguka kwa sababu ya kuwepo kwa mapungufu katika ubora. - Mwanzo 11:7
Jimena njoo huku na
benie360