Jamii ya Kitanzania iache kulazimishana kuongea na watu, kama mtu huyo hapendi

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Kwa nini Watanzania wanapenda kulazimishana kuongea na watu

Unakuta mtu unapenda kukaa peke yako kimya bila kusumbua watu, unashangaa wanaanza kukuuliza mbona huongei na watu, na kuanza kukupangia kuwa unapaswa uanze kuongea na watu

Kuna muda unawasikia wanakusema kimyakimya eti huongei na watu, na sijui kwa nini wanadhani wakikusema hivyo basi wewe hautajua 🤦

Acheni kila mtu a enjoy maisha yake, tusipangiane namna ya kuishi. Unakuta mwingine eti anataka akusaidie kukuchangamsha uwe unaongea na watu. Aliyekuambia nataka msaada wako ni nani?

Mtu unakaa kimya usiwasumbue watu, lakini bado hata ukimya wako nao unawasumbua 🤔
 
Je ukitingwa sasa huto watafuta?,haijalishi uchumi wako ukoje na unajimudu kiasi gani ila kama wewe hutak kusumbuliwa na majilan asa kwa kujuliana hali,kusaidiana kwenye shida na raha basi usije sumbua na wewe
 
Huku sijui kama wahusika wapo kweli hao waliokusema
 
Sidhani.
 
Kuna video moja ya mmarekani mweusi aliyehamia Ghana niliona;

Anasema magharibi wana maendeleo makubwa ya kiuchumi ila afrika kuna maendeleo makubwa ya kijamii.

Watu wanahudumia wazazi waliozeeka, wanasaidia wapita njia, wanasemeshana japo hawafahamiani nk. Ukifikiria ni kweli.

Hao wanaokusemesha hawana nia mbaya wanataka ujumuike nao tu. Wewe jikaze hiyo ni kazi ndogo huwezi kushindwa.
 
Je ukitingwa sasa huto watafuta?,haijalishi uchumi wako ukoje na unajimudu kiasi gani ila kama wewe hutak kusumbuliwa na majilan asa kwa kujuliana hali,kusaidiana kwenye shida na raha basi usije sumbua na wewe
Unamsaidia mtu sababu mmezoeana au kisa ushikaji wa kupigishana stories huu ni unafiki, maana msaada wa kweli hauhitaji kujuana ndipo utoe msaada, kitendo cha mtu kukupa salamu hiyo inatosha msipende kuwafanya watu wafuate mienendo yenu ya maisha mwishoe mzoeane kipumbavu na muanze maugomvi yasiyo na tija
 
Watakuja wakudanganye ooh wewe ni introvert ni uongo kibao.

Punguza kupiga puli
Nakumbuka neno "Introvert" mara ya kwanza kuliona ilikuwa ni humu Jamii Forums, hata nilikuwa silijui.
Ila point kuu ni kwamba kama mtu ni mkimya acha aishi maisha yake. Kwa nini watu wanakusema as if ni kitu kibaya kuwa mkimya? Kuna mtu humu alisema eti ni mental health problem. Well I love my mental health problem,

Huenda hujawahi ku experience kusemwa semwa na watu kimyakimya na unawasikia wanavyokusema halafu wenyewe wanadhani huwasikii. Siku ukipata hiyo feeling utaelewa kwa nini watu wanataka waachwe free waishi wanavyopenda
 
Unamsaidia mtu sababu mmezoeana au kisa ushikaji wa kupigishana stories huu ni unafiki, maana msaada wa kweli hauhitaji kujuana ndipo utoe msaada, kitendo cha mtu kukupa salamu hiyo inatosha msipende kuwafanya watu wafuate mienendo yenu ya maisha mwishoe mzoeane kipumbavu na muanze maugomvi yasiyo na tija
Kabisa mkuu, watu wanalazimisha eti ili umsaidie mtu lazima uwe unapiga naye story kila siku
Kwamba kama mtu akipata maumivu ya kichwa akakuomba umsaidie Panadol na unazo karibu hautampa eti kwa sababu hapigi story na wewe? Huo unakuwa ni unafki
 
Mkuu unaonekana una tabia za "Introvert
Muhimu hakikisha una pata mke na watoto mapema, ukifeli kwenye hili utapata tabu sana hapo baadaye
 
Kuna video moja ya mmarekani mweusi aliyehamia Ghana niliona;

Anasema magharibi wana maendeleo makubwa ya kiuchumi ila afrika kuna maendeleo makubwa ya kijamii(intangible social development).

Watu wanahudumia wazazi waliozeeka, wanasaidia wapita njia, wanasemeshana japo hawafahamiani nk. Ukifikiria ni kweli.

Hao wanaokusemesha hawana nia mbaya wanataka ujumuike nao tu. Wewe jikaze hiyo ni kazi ndogo huwezi kushindwa.
Sahihi mkuu, ila tatizo na wao wanasahau hata mtu mkimya pia hana nia mbaya nao
 
Back
Top Bottom