Sidhani.Kwa nini Watanzania wanapenda kulazimishana kuongea na watu
Unakuta mtu unapenda kukaa peke yako kimya bila kusumbua watu, unashangaa wanaanza kukuuliza mbona huongei na watu, na kuanza kukupangia kuwa unapaswa uanze kuongea na watu
Kuna muda unawasikia wanakusema kimyakimya eti huongei na watu, na sijui kwa nini wanadhani wakikusema hivyo basi wewe hautajua 🤦
Acheni kila mtu a enjoy maisha yake, tusipangiane namna ya kuishi. Unakuta mwingine eti anataka akusaidie kukuchangamsha uwe unaongea na watu. Aliyekuambia nataka msaada wako ni nani?
Mtu unakaa kimya usiwasumbue watu, lakini bado hata ukimya wako nao unawasumbua 🤔
Walikuambia kwamba ukiongea nao unawasumbuaYani unipige kofi kwa kosa gani? Kutowasumbua watu?
Unamsaidia mtu sababu mmezoeana au kisa ushikaji wa kupigishana stories huu ni unafiki, maana msaada wa kweli hauhitaji kujuana ndipo utoe msaada, kitendo cha mtu kukupa salamu hiyo inatosha msipende kuwafanya watu wafuate mienendo yenu ya maisha mwishoe mzoeane kipumbavu na muanze maugomvi yasiyo na tijaJe ukitingwa sasa huto watafuta?,haijalishi uchumi wako ukoje na unajimudu kiasi gani ila kama wewe hutak kusumbuliwa na majilan asa kwa kujuliana hali,kusaidiana kwenye shida na raha basi usije sumbua na wewe
Kwa nini wamdanganye ,wewe unafikiri kila mtu ana hizo tabiaWatakuja wakudanganye ooh wewe ni introvert na uongo kibao.
Punguza kupiga puli
Nakumbuka neno "Introvert" mara ya kwanza kuliona ilikuwa ni humu Jamii Forums, hata nilikuwa silijui.Watakuja wakudanganye ooh wewe ni introvert ni uongo kibao.
Punguza kupiga puli
Kabisa mkuu, watu wanalazimisha eti ili umsaidie mtu lazima uwe unapiga naye story kila sikuUnamsaidia mtu sababu mmezoeana au kisa ushikaji wa kupigishana stories huu ni unafiki, maana msaada wa kweli hauhitaji kujuana ndipo utoe msaada, kitendo cha mtu kukupa salamu hiyo inatosha msipende kuwafanya watu wafuate mienendo yenu ya maisha mwishoe mzoeane kipumbavu na muanze maugomvi yasiyo na tija
Sahihi mkuu, ila tatizo na wao wanasahau hata mtu mkimya pia hana nia mbaya naoKuna video moja ya mmarekani mweusi aliyehamia Ghana niliona;
Anasema magharibi wana maendeleo makubwa ya kiuchumi ila afrika kuna maendeleo makubwa ya kijamii(intangible social development).
Watu wanahudumia wazazi waliozeeka, wanasaidia wapita njia, wanasemeshana japo hawafahamiani nk. Ukifikiria ni kweli.
Hao wanaokusemesha hawana nia mbaya wanataka ujumuike nao tu. Wewe jikaze hiyo ni kazi ndogo huwezi kushindwa.