Jamii yote shangilieni, kaeni mkao wa kula na kunywa vinono!

Kwa hiyo na mimi nikitaka mstari wakutembea nao kibingwa mwaka huu naupata? Hebu nipe japo kitu naona una kitu
 
Sijaelewa
Pole, mkuu Addons , nafikiri uli-miss tukio la kuagana. Usijali, tunaishi enzi za kidigitali. Tukio lenyewe lilihifadhiwa salama salimini. Ilikuwa hivi:
 
Kwa hiyo na mimi nikitaka mstari wakutembea nao kibingwa mwaka huu naupata? Hebu nipe japo kitu naona una kitu
Nimekuja na makapu yaliyojaa lishe. Pata hii supu yenye nguvu utembee nayo kibingwa mwaka huu..
Isaya 41:10
Usiogope, maana mimi ni pamoja nawe[@Iceberg9 ]; usifadhaike, maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
 
Setfree me nipe ubwabwa wa kiroho weka na kachumbari, pilipili kwa mbaaali 🤌
 
Ningeokoka ila kwa kutonitag navunja urafiki na wewe leo
 
Setfree me nipe ubwabwa wa kiroho weka na kachumbari, pilipili kwa mbaaali 🤌
Ubwabwa bado sijaanza kugawa. Tumeanza na Starter soup.
Kiri maneno haya. Sema...
“Bwana ni mwamba wangu mimi [@Nomadix ], ngome yangu, na Mwokozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu nimkimbiliaye...” (Zaburi 18:2)
 
Umerudi na zawadi gani?

Kuna id ndio naziona leo kati ya izo zote ulizo taja hapo
 
Ubwabwa bado sijaanza kugawa. Tumeanza na Starter soup.
Kiri maneno haya. Sema...
“Bwana ni mwamba wangu mimi [@Nomadix ], ngome yangu, na Mwokozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu nimkimbiliaye...” (Zaburi 18:2)
Tuanze na majani mabichi

Zab 23:1-
"BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza."
 
Una kitu, ikawe hivyo kama mtumishi wake Bwana alivyodhamilia, naubeba na ninaishi nao✅
 
Umerudi na zawadi gani?
Zawadi hii itakufaa sana
Yeremia 29:11
"Maana najua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa tumaini siku zenu za mwisho."
 
Karibu sana mtumishi, nilikumiss....
 
Usijali, mkuu. Hao niliowatag ni wale walionishika mkono siku ya farewell. Wewe ulikuwa wapi siku hiyo?
Safari hii usipookoka, usimlaumu Mungu kabisa, maana kwa huruma zake amenituma nilete tena chakula cha uzima.
Basi bwana liwalo na liwe bwana
 
wahubiri wa siku hizi mnapenda kunywa balimi shida ni nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…