LGE2024 JamiiCheck ilivyoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024: Taarifa sahihi huwawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi

LGE2024 JamiiCheck ilivyoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024: Taarifa sahihi huwawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

JamiiCheck

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2023
Posts
245
Reaction score
267
Uthibitishaji wa taarifa ni msingi unaowawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi kutokana na Taarifa sahihi mathalani kipindi cha uchaguzi, hili linafanikishwa kwa mapambano dhidi ya taarifa potoshi pamoja na kuwajengea uelewa wananchi jinsi ya kutambua na kudhibiti taarifa zisizo za kweli.

Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024, JamiiAfrica kupitia jukwaa lake la JamiiCheck ilikabiliwa upotoshaji wa taarifa kwa njia ya makusudi kwa kutumia mikakati ya prebunking (kabla ya upotoshaji) na debunking (Baada ya upotoshaji).

Prebunking ilihusisha kuwaelimisha wananchi kuhusu mbinu zinazotumika kusambaza taarifa potofu pamoja na kuboresha upatikanaji wa maudhui yanayohusu uchaguzi, ili kuhakikisha kuwa mijadala inajikita kwenye ukweli na si katika uvumi.

Kwa upande mwingine, debunking ilijikita katika kubaini na kusahihisha madai ya uongo baada ya kuwasilishwa JamiiCheck, kwa kutoa ufafanuzi wenye ushahidi ili kuondoa upotoshaji. Mbinu hii ya pande mbili ililenga kuongeza uimara wa umma katika kupambana dhidi ya taarifa potofu, na kuwezesha jamii yenye maarifa na uwezo wa kuchambua uhalisia wa taarifa.


Prebunking

Uundwaji wa “maktaba” ya uchaguzi iliyopangiliwa kwa umakini umechukua nafasi muhimu katika kupunguza ueneaji wa taarifa potofu.

Kupangwa kwa maudhui ya uchaguzi chini ya vipengele vya “LGE2024” na “PreGE2025” kumewawezesha wananchi kulinganisha taarifa na kupata data zilizothibitishwa, hivyo kupunguza athari za ripoti za kupotosha.

Prebunking pia ilihusisha kuwaelimisha wananchi kuhusu mbinu za kawaida zinazotumiwa kusambaza taarifa potofu, hivyo kuwapa zana za kutambua na kupinga simulizi za uongo kabla ya kukutana nazo.


Debunking

Mapambano dhidi ya upotoshaji wa taarifa yameimarishwa kupitia ushiriki hai wa wananchi katika kuhakiki taarifa zinazohusu uchaguzi.

Kati ya mwezi Julai hadi Desemba, wananchi waliwasilisha zaidi ya habari 80 zinazohusiana na uchaguzi kwa ajili ya uhakiki, hali inayoonesha kuongezeka kwa uelewa wa madhara ya taarifa potofu na utayari wa jamii kushiriki katika uhakiki wa taarifa kwa wakati halisi.

Mbinu hii ya ushirikiano imeboresha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa taarifa sahihi, hivyo kurahisisha kwa wapiga kura kuthibitisha madai mbalimbali na kupinga simulizi za za kupotosha.


Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa (Fact-Checking)​

Kupitia vyanzo rasmi kama Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), vyama vya siasa, na taasisi za serikali

Kuchambua video, picha na madai yanayosambaa kwa kutumia nyenzo maalum za kuhakiki taarifa

Kufanya mahojiano na wataalamu wa uchaguzi na sekta husika (mfano: wanasheria) ili kupata muktadha mpana

Kufuatilia mikutano ya kisiasa na hotuba mbalimbali.


Takwimu Muhimu za Uhakiki wa Taarifa

Aina za Upotoshaji wa Taarifa (Data: Juni–Desemba 2024, madai 81):​

10%: Kauli za kisiasa na upotoshaji kuhusu taratibu za uchaguzi

18%: Ripoti za potoshi kuhusu matokeo ya uchaguzi na mchakato wa upigaji kura

72%: Maudhui yaliyoghushiwa (deepfakes), picha/video zilizooneshwa kwa upotoshaji


Walengwa wa Upotoshaji wa Taarifa

3% (2 kesi):
Madai ya uongo kuhusu Rais Samia

6% (5 kesi): Walengwa walikuwa viongozi wa dini

16% (13 kesi): Vyama tawala (CCM) kuoneshwa kwa upotoshaji

75% (61 kesi): Upotoshaji uliwalenga vyama vya upinzani, vikawa walengwa wakuu


Aina za Maudhui ya Taarifa Potofu

63%
: Kauli za kisiasa na upotoshaji kuhusu taratibu za uchaguzi

31%: Ripoti za potoshi kuhusu matokeo ya uchaguzi na mchakato wa kupiga kura

6%: Vyombo vya habari vilivyoghushiwa (deepfakes) au picha/video zilizopotoshwa


Vyanzo vya Upotoshaji wa Taarifa

41%
: Zilitoka X (zamani Twitter)

27%: Zilitoka Facebook

19%: Zilitoka Instagram

13%: Zilitoka vyanzo vingine, hasa makundi ya WhatsApp


Teknolojia Zilizotumika

Kwa sasa, maudhui potofu yanayotengenezwa kwa kutumia akili unde (AI) bado ni kwa kiasi kidogo nchini Tanzania. Ni madai manne tu kati ya yaliyohakikiwa yaliyoonesha kutumia AI kikamilifu, huku maudhui mengi yaliyopotoshwa yakitengenezwa kwa kutumia programu za kawaida kama Canva na Adobe.

Mfano: JamiiCheck ilibainisha upotoshaji kwenye madai yaliyoenea mtandaoni kuwa Jaji Mstaafu, Joseph Sinde Warioba alikuwa amesifia jinsi uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyofanyika.


Hitimisho

Juhudi za JamiiCheck katika kuhakiki taarifa zimeonesha umuhimu wa kuendelea na kampeni za uelimishaji wa umma, ushirikiano kati ya vyombo vya habari na wahakiki wa taarifa, na matumizi ya teknolojia ya kisasa kupambana na taarifa potofu za kidijitali, zikiwemo deepfakes.

Tunapoelekea uchaguzi mkuu wa 2025, kulinda uadilifu wa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kunasalia kuwa jambo la msingi.
 
ila kuna watu hapa ambao wanapotosha sana mnawafumbia macho tena wakisema chadema au kauli ambazo zikiwa ukweli kuhusu mwenendo wa serikali ya ccm mnafuta.
 
Back
Top Bottom