Jamiiforums GYM (mazoezi ) thread

Mazoezi ni mazuri na ni kitu cha muhimu sana kwenye mwili wa binadamu kama ukiweza kuyazingatia.

Napenda kukimbia lakini napata shida kwenye magoti nikikimbia wiki mbili tu nahisi kama kuna vidonda,nimeanza dozi ya kila siku asubuhi na jioni nakula bamia mbichi tano nahisi zimenisaidia though nilisimama nataka nxt monday nirudi barabarani nione,mleta mada shukrani kwa kutu-inspire ktk hili.
 
Oya kwa dar gym ga I nzuri ambayo wapo warembo classic
 
Magoti shida....mzee utakuwa unakamia sana wakati wa kugegeda 🀣🀣🀣🀣🀣
 
Magoti shida....mzee utakuwa unakamia sana wakati wa kugegeda 🀣🀣🀣🀣🀣
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Mkuu lakini simfikii muwakilishi wetu mzee wa kuwauwa wima wima kimya kimya
Your browser is not able to display this video.
 
Aisee wahi mapema hiyo shida kuna mshkaji wangu alipuuzia amefanyiwa operation ya ligament juzi hapa
Tatizo ni hilo hilo mkuu, sijui shida ni nini haswa, vipi yeye operation yake wamemfanyia kwa sh ngapi goti moja na ni hospitali gani?
 
Tatizo ni hilo hilo mkuu, sijui shida ni nini haswa, vipi yeye operation yake wamemfanyia kwa sh ngapi goti moja na ni hospitali gani?
MOI nenda kamuulizie dr sabas mshkaji na mwamba sana jamaa alifanya kwa bima.. by the way unaweza fanyiwa tiba bila operation inategemea na tatizo.
 
Saint Anno II

Nadhani muhimu ufanye vipimo kwanza kuhusu hayo magoti kabla hujaendelea sababisha uharibifu zaidi. Kama kuna shida utaambiwa na namna ya kupata matibabu.

Muda mwingine kulingana na hali ya magoti itakavyo onekana kwenye vipimo, waweza katazwa kabisa kukimbia, mbadala wake unatembea tu.

Magoti ni kiungo muhimu sana na ndo "the largest and very complex joint in human body".

Kila la heri.
 
Pia unaweza pata tiba bila operation.. jamaa yangu alifuga tatizo.
Niko interested mkuu, hali inakiwa tete kadri siku zinasonga mbele.

Mama yangu mzazi yeye ligament zimeisha kabisa, ni mifupa inasagika tu, nilitaka kuchukua maamuzi magumu ya kuuza kakibanda akapate tiba, akagoma.. Kipindi hiko tuliambiwa mguu mmoja eti milioni 12, yote miwili ni 24, na hapo kuna uwezekano wa kutembelea kiti maisha yako yote, akagoma kabisaa, tokea hapo sikufuatilia tena.
 
Kacheki mapema afya ya hilo goti pale moi kama upo dar kuna wataalam wazuri.. ukipenda nitakudirect magoti ni sensitive sana ukipuuzia utakuja fanyia OP
Hii changamoto ninayo, maana nakimbia sana kwenye lami, ngoja nijipange nikawachek wataalam hao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…