JamiiForums imenifanya tuamue maamuzi haya mimi na wife

Mkuu Intelligent businessman,
Binafsi nimesoma comments zako na kuelewa, huenda jamaa alikurupuka, huenda pia alijipanga.

Swala la ndoa ni very complicated, unaweza kujipanga kihisia, kiuchumi na kila kitu na bado ndoa ikakushinda. Na kuna wenzetu wala hawajipangi, anamtia mtoto wa watu mimba, analazimishwa kumuoa na ndoa inakuwa na baraka zote.

Swala la kukaa vizuri kiuchumi halina guarantee hata kidogo kwamba ndoa itakuwa poa, as tunaona wengi wanakaa poa, baada ya muda wanaanguka.

Binafsi sitaki kumlaumu mleta mada, we really don't know kilichotokea kabla/baada ya yeye kuoa. Japo alitakiwa kuzingatia uzazi wa mpango😅
 
Mkuu wala mimi sija mlaumu, ila nime mpa ushauri hali ikiwa ngumu awa rudishe home ili aji pange kwanza.

Binafsi nime ishi maisha ya aina tatu, kishua, average na hadi choka mbaya na mpaka leo nina experience kubwa juu ya maisha.

Uko sahihi muda mwingine kuweka standard ya juu kwenye maisha, nako ni kamzozo kidogo.
simplifying mambo nayo haimaanishi mambo ni mukide.

hahaha usi mlaumu shemeji yetu, jambo la uzazi ni la familia bwana na si mtu mmoja.
 
Ana watoto wanne we ungempokea?
 
Mkuu hilo linafahamika sawa sio mbaya kumuoa mwanamke uliyezaa naye ila ndio upige dabodabo hadi watoto 4 wakati hela ya kula mtihani?
Huoni kuwa hapo amewaleta hao viumbe ili wateseke tu na baadae kutengeneza kizazi kingine cha umaskini
 
Wangeenda shamba kufanya kilimo ingekuwa vizuri zaidi.

Wataomba mpaka lini?

Asilazimishe kuishi mjini
 
Awarudishe home wapi Mkuu?

Wakati Story yake tu inaonekana jamaa home kugumu(sijajua Kwa Binti Yani mke wake) kifupi jamaa hana home yeye ndiyo Kila kitu.

(Nyongeza siku hizi usi zae ukategemea bibi au babu au ndugu yeyote atakulelea watoto wako mambo hayako hivyo Mkuu).

EXPERIENCE.
 
Toka magetoni Bob , chukua maamuzi , maisha yako ni jukumu lako, ndoto zako utatimiza mwenyewe, ukitegemea binadamu watakugeuka na ukitegemea mungu naye haonekani.
 
Ifikie hatua tuache unafiki tuwe wakweli.

Unapomwaga ndani kila siku unategemea nini zaidi ya mimba?

Na hao watoto unatarajia nani aje kuwahudumia?

Tujipange ili tusiwatese watoto, tunawaumiza sana kwa ujinga wetu
 
Kila siku nasisitiza ndoa ni kwa watu wenye akili timamu tu.

Huyu kijana hata sijui ni wa mkoa gani aisee maana naona kabisa hapa shida ipo kwenye ubongo wake hivi maisha ya mlo mmoja unapataje nguvu ya kutombana na kuzaana kama simbilisi, Bro hata wanyama mbugani wamekushinda akili hukuti wanazaliana kipindi cha kiangazi/ njaa huzaliana kipindi cha uhakika wa malisho.

Huyu hata mumpe mtaji wa 1M hatatoboa kwasababu akili yake imelala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…