JamiiForums imenifanya tuamue maamuzi haya mimi na wife

Mkuu katika hii mada yako nimegundua wana JF wengi uwezo wa kufikiri ni mdogo lakini pia hawana experience yoyote yamaisha wanaangalia vitu Kwa udogo Sana au naweza sema ni watoto watoto(sio wote wengi wao).

Hivyo basi nenda nawale wanao kusaidia/kufaa watoto watoto achana nao.
 
Ifikie hatua tuache unafiki tuwe wakweli.

Unapomwaga ndani kila siku unategemea nini zaidi ya mimba?

Na hao watoto unatarajia nani aje kuwahudumia?

Tujipange ili tusiwatese watoto, tunawaumiza sana kwa ujinga wetu
Sio unafiki Mkuu.

Nikweli kabisa Mkuu watoto wanateseka Sana.

Nilishawahi kuleta Uzi hapa wa kukemea/kuwakumbusha watu uzazi wa mpango. Watu wengi sana wana feli hapo.

Nakama umesha feli inatakiwa ukomae kulea sio kukimbia/kutelekeza au kuwaachia ndugu wakati nawao hamna kitu.

Komaa na watoto wako fight mpaka mwisho ndicho ninacho maanisha Mkuu.

Sina maana yakwamba watu wazae hovyo NO.
 
Sehemu ya pili hii hapa 👉🏻👉🏻JamiiForums imenifanya tuamue maamuzi haya mimi na wife sehemu 2
 
Mimba nne bahati mbaya?
Sijasema Bahati mbaya Mkuu. Wala sitetei yeye kuzalisha hao watoto 4.

Nampongeza kwasababu hajakimbia majukumu yake kama baba anaendelea kupambana with her wife and their kids.

Sisi ndiyo tunasikia story yake Leo inamaana miaka yote yeye si ndiyo alikuwa anatunza familia yake inawezekana mambo tu yamemwendea kombo sio kwamba hajielewi Mzee mambo yanabadirika don't forget that.
 
Mkuu ngoja nikupe ushauri mmoja hivi,humu ndani hatupo kwa ajili ya kubishana na wala usione kama watu wanakukejeli ila unatakiwa uichukue hiyo kama challenge na ubadilishe fikra zako usiwe stagnant maisha hayataki hivyo
 
Mkuu ngoja nikupe ushauri mmoja hivi,humu ndani hatupo kwa ajili ya kubishana na wala usione kama watu wanakukejeli ila unatakiwa uichukue hiyo kama challenge na ubadilishe fikra zako usiwe stagnant maisha hayataki hivyo
Nakubaliana na kila mawazo ya mtu ndo ningekuwa tayari kupokea nisingelileta humu ila panapo bidi inabidi nijibu story hata sijaimaliza mtu kasha conclude kuwa fanya hivi mzee hata mimi maisha mazuri japo sio mazuri kama ya kwenu nilishawahi kuyaishi vizuri tu tena nikiwa na hao watoto wangu nitakapo maliza simulizi utanielewa
 
Mdogo wangu watoto 4 kwa maisha yako huo mtihani.
Hamkuwaza uzazi wa mpango?
Au mkeo aligoma? Maana hawa ndugu zetu baadhi wanajua wenyewe wanataka Nini.
 
Pole.
Ushauri wangu kama utapata mtaji usimpe mkeo, huo mtaji pambana nao wewe mwenyewe, kama mtaji utampa mtaji mkeo na biashara ikafanya vizuri mwanamke atakuzarau na ataona wewe sio hadhi Yake na ndio itakuwa mwisho wa ndoa Yako.
 
Pole,
Ninafikiria business ideas za kukupa mtaji mdogo mnaweza fanya pamoja.. ofa sitapokea senti yako. Inbox me, nikiwa free tutachati inbox. Lazima utajibu maswali na sio ya personal info unipe mwangaza. If unajua ya library naamini utaweza mengi. Hii wengine kupata passive income inawasaidia pia. Kill la kheri usiruhusu wansosema ya kukushusha moyo humu wakafanikiwa kukushusha.
 
Barikiwa sana
 
Asante kwa ushauri mkuu kama umebarikiwa kupata pakujiegesha paheshimu sana sio kila mtu ana bahati hiyo
Mkuu,
mi mwenyewe mpambanaji tu hapo nimekupa ushauri kidogo tu
 
Wakati kina wenzio wanazaa watoto wanawapeleka kwa mama zao ndowalee
 
Kwamba wakiumwa wanaumwa wote kwa wakati mmoja mkuu,huku mtaani mambo si kama huku mnavyojinadi,mahusiano ya kawaida kabisa yapo mke na mume hawana kitu lakini wanafight pamoja leo wamekosa kesho wanasaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…