JamiiForums linaweza kuwa darasa zuri sana la waandishi wa habari wanaoiona fursa hii

JamiiForums linaweza kuwa darasa zuri sana la waandishi wa habari wanaoiona fursa hii

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
JamiiForums ni darasa huru ambalo kama mtu anatamani kuwa mwandishi bora kabisa wa masuala mbalimbali anaweza kujiona na kufikia viwango vya juu sana. Nashauri waandishi wa habari najaribu kuitumia fursa hii ili kuepusha uandishi holela na kurupushi.

Nakiri kujifunza mengi sana yanayohusiana na uandishi mzuri katika viwanja huu mardhawa. Sijawahi kuwaza kuwa mwandishi kabisa lakini kupitia viwanja huu nimejifunza mengi sana juu ya uandishi bora wa masuala mbalimbali. Nadiriki kusema hivi kwa sababu zifuatazo;

(i) JamiiForums ni jamii pana yenye watu wenye umahiri na umilisi juu ya masuala mbalimbali hivyo hata kama ulioandika chochote unaweza kujifunza mengi sana kutika kwao bila gharama yoyote.

(i) JamiiForums ni uwanja wa uzoefu na utendaji na siyo darasa tu la kujifunza nadharia. Shuleni unaweza utajifunza nadharia nyingi sana juu ya uandishi bora lakini Jamii forum inatoa uwanja bora kabisa wa kiutendaji.

(iii) JamiiForums inatoa nafasi ya mtu kuongeza uelewa wake zaidi juu ya masuala anayoyapenda. Jamii hii inatoa uwanja moana wenye kila kitu hivyo ni rahisi sana kwa mtu kuboresha maarifa yake zaidi juu ya pendeleo zake. Kuna wabobevu katika maeneo mbalimbali.

(iv) Uwanja huu unatoa nafasi ya mtu kuwa na akili huru au mawazo huru "open minded" hivyo unafanya mtu kuendelea kujifunza badala ya kujifungia akili au mawazo yake mahali pamoja. Mathalani unaweza ukaandika uzi humu na ukaona watu wanavyochangia kwa miono tofauti tofauti na hivyo ni nafasi ya kujifunza ustahimilivu wa kiakili na kukubali kukosolewa.

(v) Uwanja huu unaonesha wazi wazi kuwa unaendana na utofauti kama ladha ya maisha hivyo haumchoshi mtu kuendelea kujifunza labda aamue mwenyewe kujifungia katika eneo moja tu. Tabia hii ya mhamo wa kiakili juu ya vitu mbalimbali kuzidisha taharuki ya kiudadisi ya kiakili kwa mwandishi.

Itaendelea...
 
Mimi nikipata habari yoyote nikitaka kujiridhisha haingia kwenye uwanja wa Jamii forum naona mashaka yote, mawazo tofauti tofauti na nimepata hitimisho humuhumu.
 
Back
Top Bottom