JamiiForums na FikraPevu, walaani nguvu inayotumika kuzuia uhuru wa maoni

hivi walikuwa 191?dah wengi sana wameshatoka?polen sana jamii
 
Ni ujinga kufikiri kama jamiiforum inaeneza sumu ya mabadiliko, wananchi wamechoka mifumo mibovu, kuattack jamiiforum sidhani kama ni suruhisho, LA kumaliza matatizo kati ya wananchi na serikali. Serikali inabidi iwajibike, tutaendekea kupiga kelele hata kama wataziba masikio. Pongezi kwa uongozi mzima wa jamii forum kwa kupambana na maharamia wa kimtandao.
 
Bila shaka kuna take home baada ya mashambulizi kama haya! Jitahidi sana kuweka security features zenu salama ili kuzuia mashambuliz zaidi!
 
Wakuu,

Zamasiku, kuna jambo ninaendelea nalo kufanya uchunguzi wa kina, nipo katika hatua nzuri, naendelea kukusanya ushahidi na baadhi ya nyaraka nyingine muhimu.....

Kwa wale wageni ni kwamba katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2015 uliyomuweka madarakani mweshimiwa "Hapa kazi tu" , yalitokea matukio yasio ya kawaida ikiwamo kukosekana kwa huduma, inasemekana ni mashambilizi kutoka kwa wajuzi wa mitandao, kwa lugha za kitaalamu DoS (Denial of Service) kisha tukaaminishwa kuwa mashambilizi yameongezeka kufikia kiwango cha DDoS (Distributed denial of service ) ambayo ni makubwa kabisa kwa kuwa mashambilizi yanatoka sehemu mbali mbali kwa kutumia IP moja kuhakikisha hakuna mtu ambaye anaweza kupata huduma.

Ikumbukwe kuwa hadi kabla ya kampeni kuanza, idadi kubwa ya watanzania walitegemea sana taarifa toka JF, Media nyingi zilibanwa na kauli mbiu ya "kujiepusha na uchochezi , Kudumisha Amani", kiasi kwamba walikuwa waoga sana kuripoti matukio muhimu, hili liliendelea hadi kipindi cha matokeo ya uchaguzi ambapo Media zote zilibanwa na kaulimbiu "Matokeo rasmi kutoka Tume ya uchaguzi" kaulimbiu iliyopelekea media kushindwa kuripoti hadi matokea yaliyosainiwa na kubandikwa kituoni.

Hali iliendelea hivyo hadi kutangazwa kwa yanayoitwa "Matokeo rasmi". Watu wajiulize ile iliyokuwa inaitwa "Azam TV kituo chako cha uchaguzi" iliyeyukia wapi? ile investment yote ya mzee Bakhresha, magari, vifaa na mitambo iliyeyukia wapi? kwanini ghafla hakukuwa na live coverage na kuishia kukimbilia NEC kusikiliza "Matokeo rasmi"! Iweje matokea yaliyosainiwa na wagombea na msimamizi wa kituo yaogopwe kutangazwa? Anyway maswali ni mengi mno......

Kurudi kwenye agenda, ni kwamba Katika kipindi hicho, JF ilikuwa na nafasi adhimu kuhakikisha wananchi wanahabarishwa kutoka kwa maripota waliojitolea kutoka pembe zote za nchi, lakini ya yenyewe hali ilikuwa mbaya zaidi kwa kuwa mtandao haukufanya kazi au uligubikwa na changamoto sana.

Kabla ya kutokea haya kuna mambo mawili matatu yanayonitia shaka sana yalijitokeza kuelekea uchaguzi huo
1) Wasimamizi wa mtandao wa JF walibadili mwelekeo ghafla na kujaribu kulinda taarifa za wafuasi wa "hapa kazi tu" na chama chake , mada nyingi dhidi yao zilifutwa au kuonganishwa, yalitokea malalamiko makubwa sana kutoka kwa member... Hii ilipelekea hadi member wa "Hapa kazi tu" waliowahi kuanzisha mada zinaohusu wapinzani wao, na zikaachwa zikiongozwa na wao, bahati mbaya "UPDATES" zilikuwa biased na kila aliyejaribu kuanzisha mada iliunganishwa.

2) Pili, ulitokea ushwahiba wa ghafla sana wa baadhi ya viongozi wa JF na media nyengine "pro-Hapa kazi tu", media ambazo zililalamikiwa kwa kutokuwa fair katika kutoa matukio ya uchaguzi.
kama lengo ni kujenga mahusiano mema, iweje mialiko ile ikome ghafla baada ya uchaguzi? Je unajua wakina nani walikuwa nyuma ya mialiko ile?

Hatua ninayopanga kuchua.

Nianaendelea kufuatilia, kusoma sheria za JF, sheria za nchi na kukusanya ushahidi mwengine ili kujiridhisha kama Uongozi wa JF umetenda kosa lolote kwa wajumbe wake, ikiwamo kama walishiriki kwenye "uovu" ule na kama hawakushiriki iwapo "walizembea". Katika hili pia kuangalia kama taarifa za wajumbe wa mtandao huu zipo salama baada ya yale yanayoitwa mashambulizi.

Wito wangu kwa wanaJF.

Yoyote mwenye ushahidi wa ziada tafadhari aniPM au aumwage hapa, hii ni pamoja na zile video/clip zote za mada mbali mbali walizoalikwa viongozi wa JF kwenye media mbali mbali. Ni lazima tuchukue hatua kali sana "IKITHIBITIKA" kulikuwa na ukiukwaji wa sheria ya makubaliano baina ya waendeshaji na watumiaji wa mtandao ili jambo kama hili lisijirudie tena.

Kumbuka: Kunyima uhuru wa habari, kunafifisha demokrasia...tushirikiane kupambana.

Asanteni

Tume ya katika
Mcheza Pool table
 
Acha kuturudisha nyuma sisi tunapiga speed ya maendeleo.sio majungu,unauhakika gan.kama walihack na.kama una uhakika huo si fata taratibu establish grounds zako nenda,unataka kuleta issue za uchaguz ambazo zimepita hayo ni.mawazo mgando,tumepata rais wa tanzania subiri siku zingine
 
Maendeleo gani mkuu? Kupanga foleni kununua sukari? Hali ya maisha kuwa ngumu? kukosekana kwa ajira?

Hatuwezi kuacha watu wanyime habari ili kufanikisha malengo yao....
 
Jf mods wanazingua kuna siku nimetupia hot uzi unao husiana na lugumi ukafutwa fasta .
 
82d129c70930c3cc906e4898bf5e10a6.jpg
 
Acha kuturudisha nyuma sisi tunapiga speed ya maendeleo.sio majungu,unauhakika gan.kama walihack na.kama una uhakika huo si fata taratibu establish grounds zako nenda,unataka kuleta issue za uchaguz ambazo zimepita hayo ni.mawazo mgando,tumepata rais wa tanzania subiri siku zingine
Tunataka tujue ni kwanini ilitokea vile, na ni nani alikuwa nyuma ya ule mchezo!!!!
Inawezekana kama wapo wanaoujua ukweli halisi wanakucheka muda huu.
 
Back
Top Bottom