Upweke unaweza kupelekea msongo wa mawazo, kwa mtazamo wangu afadhali ya upweke kuliko msongo wa mawazo. Ukitafakari sana, yote ni mambo ya kufikirika tu! Upweke unakuaje? Mbona wengine wanapenda upweke na ndio maisha wanayoyafurahia?
Msongo wa mawazo hali kadhalika, jambo unaloliona mzigo au kikwazo kiasi cha kukukatisha tamaa kwa mwingine hata halimsumbui kabisaaa.
Inategemea unalichukuliaje na una weza kukabiliana nalo kwa mikakati ipi. Wengi tunachachawa kama sio kupagawa sana tunapofikwa na mambo.
Kuongea kunasaidia sana, unawezasema jambo au tatizo linalokusibu ukashangaa unapata ushauri au msaada ambao hsukuufikiria na umeshaumia sana na tatizo.