Beesmom
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 37,420
- 92,254
Ina ubaya gani?Inauzuri gani?
Ina ubaya gani?Inauzuri gani?
😆🤣Wakiweka mijadala kwa lugha ya malkia huu ujinga wote unaondoka kama unapopuliza Xpel kwenye chumba chenye mbwa.
This sounds good.Itapendeza ikiwa JFA
Ni kama tu ile tume ilivopewa jina tume huru ya uchaguzi halafu ikafuata No reforms no electionMnabadili jina ila watu Wana IQ zile zile
Ahsante,inafanyika lini hiyo ya waandishi Duniani na Mkoa Gani?Taasisi ya Jamii Forums imebadili jina na sasa kujulikana kama Jamii Africa huku ikijikita katika kutanua wigo wa kuwahudumia wananchi na wadau mbalimbali katika wigo mpana na mkubwa zaidi na si Tanzania pekee ikiwa ni pamoja na kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia na kuja na suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Maxence Melo, katika hafla ya uzinduzi wa jina na mwelekeo mpya wa taasisi hiyo leo Aprili 24, 2025 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Melo amesema mabadiliko haya yamelenga kuleta mbinu mpya na madhubuti za kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika sekta ya habari, uwajibikaji, na teknolojia barani Afrika.
“Tumeamua kuwa Jamii Africa baada ya kutafakari kwa kina. Tumegundua hatuwezi kupata matokeo tofauti tukibaki vilevile,” amesema Melo.
Ameeleza kuwa mchakato wa mabadiliko haya umehusisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwemo serikali, asasi za kiraia, vyombo vya habari na taasisi kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, DRC, Zimbabwe, na Afrika Kusini.
Jamii Africa inatarajia kuzindua jukwaa jipya Mei 2025 litakalohudumia zaidi ya Tanzania na kufikia nchi za Afrika Mashariki na Kusini. Lengo ni kuwapa wananchi taarifa sahihi zitakazowawezesha kufanya maamuzi bora.
Melo amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano, taasisi hiyo imefanikiwa kushirikiana na wadau wa serikali kwa mikataba 26, tofauti na lengo la awali la sita. Pia wamefanya kazi na zaidi ya asasi za kiraia na vyombo vya habari 40.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, taasisi hiyo imeandaa matukio makubwa ya kikanda yakiwemo yaliyojumuisha nchi za Afrika, na kuonesha uwezo wa Tanzania nje ya mipaka yake.
Ameeleza kuwa taasisi hiyo imeanzisha programu mbalimbali kama Story of Change, Jamii Check, na Fichua Ouvu, zinazolenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya uwajibikaji na uthibitishaji wa taarifa.
Akiongelea kuhusu mpango mkakati wa taasisi hiyo Melo amesema, unahusisha maeneo manne muhimu: kujenga mifumo ya kidijitali ya Kiafrika, kuimarisha uwezo wa vyombo vya habari na wananchi, kukuza ushirikiano katika utawala bora, na kuimarisha usalama wa kidijitali.
Sambamba na hilo, Jamii Africa imepanga pia kuzalisha vifaa vya kidijitali kama simu, kompyuta na tablets zenye maudhui ya ndani, zitakazosaidia katika utoaji wa elimu na taarifa sahihi kwa jamii.
Aidha, Melo amesema wamefanikiwa kuwajengea uwezo zaidi ya waandishi wa habari zaidi ya 1,000 nchini, na sasa wanaelekea kuwajumuisha katika muktadha mpana wa Afrika nzima.
Taasisi ya Jamii Africa kwa mwaka huu ni mwenyekiti wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, na imepanga kuleta wataalamu kutoka kampuni za kimataifa kama Meta na Google kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutumia teknolojia kwa tija.
Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Jamii Africa imechangia mabadiliko ya sera nne zinazohusu sekta ya kidijitali na sera tatu za vyombo vya habari, lengo likiwa ni kuwa na sera rafiki kwa mazingira ya sasa ya taarifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya, amesema ushirikiano wao na Jamii Africa utasaidia kuinua kiwango cha habari za Tanzania na kuzifikisha katika ngazi za kimataifa.
“Jamii Africa sasa ni jukwaa la waandishi wa Afrika wote na hata ulimwenguni,” amesema Simbaya.
Kivipi?!Bad idea so far..
Hicho kutakuwa Kaifrkana Cha Afrika kusini!Kwanini mchanganye jina kwa lugha mbili? Basi mtumie JamiiAfrika sio JamiiAfrica
Vitaje mkuu!wakati wakiendelea na hayo mabadiliko isiishie kwenye jina tuu, kuna vingi wanahitaji improvement
Good newsTaasisi ya Jamii Forums imebadili jina na sasa kujulikana kama Jamii Africa huku ikijikita katika kutanua wigo wa kuwahudumia wananchi na wadau mbalimbali katika wigo mpana na mkubwa zaidi na si Tanzania pekee ikiwa ni pamoja na kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia na kuja na suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Maxence Melo, katika hafla ya uzinduzi wa jina na mwelekeo mpya wa taasisi hiyo leo Aprili 24, 2025 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Melo amesema mabadiliko haya yamelenga kuleta mbinu mpya na madhubuti za kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika sekta ya habari, uwajibikaji, na teknolojia barani Afrika.
“Tumeamua kuwa Jamii Africa baada ya kutafakari kwa kina. Tumegundua hatuwezi kupata matokeo tofauti tukibaki vilevile,” amesema Melo.
Ameeleza kuwa mchakato wa mabadiliko haya umehusisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwemo serikali, asasi za kiraia, vyombo vya habari na taasisi kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, DRC, Zimbabwe, na Afrika Kusini.
Jamii Africa inatarajia kuzindua jukwaa jipya Mei 2025 litakalohudumia zaidi ya Tanzania na kufikia nchi za Afrika Mashariki na Kusini. Lengo ni kuwapa wananchi taarifa sahihi zitakazowawezesha kufanya maamuzi bora.
Melo amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano, taasisi hiyo imefanikiwa kushirikiana na wadau wa serikali kwa mikataba 26, tofauti na lengo la awali la sita. Pia wamefanya kazi na zaidi ya asasi za kiraia na vyombo vya habari 40.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, taasisi hiyo imeandaa matukio makubwa ya kikanda yakiwemo yaliyojumuisha nchi za Afrika, na kuonesha uwezo wa Tanzania nje ya mipaka yake.
Ameeleza kuwa taasisi hiyo imeanzisha programu mbalimbali kama Story of Change, Jamii Check, na Fichua Ouvu, zinazolenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya uwajibikaji na uthibitishaji wa taarifa.
Akiongelea kuhusu mpango mkakati wa taasisi hiyo Melo amesema, unahusisha maeneo manne muhimu: kujenga mifumo ya kidijitali ya Kiafrika, kuimarisha uwezo wa vyombo vya habari na wananchi, kukuza ushirikiano katika utawala bora, na kuimarisha usalama wa kidijitali.
Sambamba na hilo, Jamii Africa imepanga pia kuzalisha vifaa vya kidijitali kama simu, kompyuta na tablets zenye maudhui ya ndani, zitakazosaidia katika utoaji wa elimu na taarifa sahihi kwa jamii.
Aidha, Melo amesema wamefanikiwa kuwajengea uwezo zaidi ya waandishi wa habari zaidi ya 1,000 nchini, na sasa wanaelekea kuwajumuisha katika muktadha mpana wa Afrika nzima.
Taasisi ya Jamii Africa kwa mwaka huu ni mwenyekiti wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, na imepanga kuleta wataalamu kutoka kampuni za kimataifa kama Meta na Google kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutumia teknolojia kwa tija.
Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Jamii Africa imechangia mabadiliko ya sera nne zinazohusu sekta ya kidijitali na sera tatu za vyombo vya habari, lengo likiwa ni kuwa na sera rafiki kwa mazingira ya sasa ya taarifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya, amesema ushirikiano wao na Jamii Africa utasaidia kuinua kiwango cha habari za Tanzania na kuzifikisha katika ngazi za kimataifa.
“Jamii Africa sasa ni jukwaa la waandishi wa Afrika wote na hata ulimwenguni,” amesema Simbaya.
Jamii UniverseNasubiri jamii world
AiseeeIna ubaya gani?
Mbona Jamiiforums fresh tuKwanini mchanganye jina kwa lugha mbili? Basi mtumie JamiiAfrika sio JamiiAfrica