JamiiForums wabadilisha jina, Sasa kuitwa JamiiAfrica

Taasisi ya Jamii Forums imebadili jina na sasa kujulikana kama Jamii Africa huku ikijikita katika kutanua wigo wa kuwahudumia wananchi na wadau mbalimbali katika wigo mpana na mkubwa zaidi na si Tanzania pekee ikiwa ni pamoja na kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia na kuja na suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Maxence Melo, katika hafla ya uzinduzi wa jina na mwelekeo mpya wa taasisi hiyo leo Aprili 24, 2025 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Melo amesema mabadiliko haya yamelenga kuleta mbinu mpya na madhubuti za kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika sekta ya habari, uwajibikaji, na teknolojia barani Afrika.

“Tumeamua kuwa Jamii Africa baada ya kutafakari kwa kina. Tumegundua hatuwezi kupata matokeo tofauti tukibaki vilevile,” amesema Melo.

Ameeleza kuwa mchakato wa mabadiliko haya umehusisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwemo serikali, asasi za kiraia, vyombo vya habari na taasisi kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, DRC, Zimbabwe, na Afrika Kusini.

Jamii Africa inatarajia kuzindua jukwaa jipya Mei 2025 litakalohudumia zaidi ya Tanzania na kufikia nchi za Afrika Mashariki na Kusini. Lengo ni kuwapa wananchi taarifa sahihi zitakazowawezesha kufanya maamuzi bora.

Melo amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano, taasisi hiyo imefanikiwa kushirikiana na wadau wa serikali kwa mikataba 26, tofauti na lengo la awali la sita. Pia wamefanya kazi na zaidi ya asasi za kiraia na vyombo vya habari 40.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, taasisi hiyo imeandaa matukio makubwa ya kikanda yakiwemo yaliyojumuisha nchi za Afrika, na kuonesha uwezo wa Tanzania nje ya mipaka yake.

Ameeleza kuwa taasisi hiyo imeanzisha programu mbalimbali kama Story of Change, Jamii Check, na Fichua Ouvu, zinazolenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya uwajibikaji na uthibitishaji wa taarifa.

Akiongelea kuhusu mpango mkakati wa taasisi hiyo Melo amesema, unahusisha maeneo manne muhimu: kujenga mifumo ya kidijitali ya Kiafrika, kuimarisha uwezo wa vyombo vya habari na wananchi, kukuza ushirikiano katika utawala bora, na kuimarisha usalama wa kidijitali.

Sambamba na hilo, Jamii Africa imepanga pia kuzalisha vifaa vya kidijitali kama simu, kompyuta na tablets zenye maudhui ya ndani, zitakazosaidia katika utoaji wa elimu na taarifa sahihi kwa jamii.

Aidha, Melo amesema wamefanikiwa kuwajengea uwezo zaidi ya waandishi wa habari zaidi ya 1,000 nchini, na sasa wanaelekea kuwajumuisha katika muktadha mpana wa Afrika nzima.

Taasisi ya Jamii Africa kwa mwaka huu ni mwenyekiti wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, na imepanga kuleta wataalamu kutoka kampuni za kimataifa kama Meta na Google kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutumia teknolojia kwa tija.

Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Jamii Africa imechangia mabadiliko ya sera nne zinazohusu sekta ya kidijitali na sera tatu za vyombo vya habari, lengo likiwa ni kuwa na sera rafiki kwa mazingira ya sasa ya taarifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya, amesema ushirikiano wao na Jamii Africa utasaidia kuinua kiwango cha habari za Tanzania na kuzifikisha katika ngazi za kimataifa.

“Jamii Africa sasa ni jukwaa la waandishi wa Afrika wote na hata ulimwenguni,” amesema Simbaya.
About time kupanua wigo na kwenda mbali zaidi
 
MBONA JAMII FORUMS ILIPENDEZA TU NA HAIKO LIMITED! “JAMII AFRICA” IS VERY LIMITED, MAANA SIKU TUKITAKA KUJITANUA WORLDWIDE ITABIDI TUBADILI TENA JINA, ILA JAMII FORUMS IPO UNLIMITED MAANA YES NI FORUMS MBALIMBALI. KWAHIYO SIKU MKITAKA KUBADILI TENA JAMII AFRICA ILI IWE WORLDWIDE MTAIITA “JAMII WORLD??” JAMII FORUMS IS A BRAND ALREADY. FIKIRIENI HILO TAFADHALI.
 
IS A BIG MILESTONE.

MUENDANE NA HIYO HATUA.

WABONGO SASA TUACHE TREAD ZA UTELEZI
 
Ingenoga kama ingeitwa Jamiiforum Africa

* Kuna kero Huwa inajitokezaga siku za uchaguzi Mkuu hapa Bongo,
Watu wa kitengo kisichojulikana walihack hii JF na kufanya JF Iikawa haipo hewani Kwa siku 2

Angalau Kwa wazo hili JF Africa inaweza ikawa na plan B wapo Lile tatizo litajitokeza Tena.
 
Wakiweka mijadala kwa lugha ya malkia huu ujinga wote unaondoka kama unapopuliza Xpel kwenye chumba chenye mbwa.
Mawazo yako, na yanaheshimiwa.
Ila tambua kuna watu Wana content ila hawajui kimalkia; pia kuna watu wanajua kimalkia ila hawana content.
 
Wakiweka mijadala kwa lugha ya malkia huu ujinga wote unaondoka kama unapopuliza Xpel kwenye chumba chenye mbwa.
Mawazo yako, na yanaheshimiwa.
Ila tambua kuna watu Wana content ila hawajui kimalkia; pia kuna watu wanajua kimalkia ila hawana content.
 
Wakiweka mijadala kwa lugha ya malkia huu ujinga wote unaondoka kama unapopuliza Xpel kwenye chumba chenye mbwa.
Mawazo yako, na yanaheshimiwa.
Ila tambua kuna watu Wana content ila hawajui kimalkia; pia kuna watu wanajua kimalkia ila hawana content.
 
Taasisi ya Jamii Forums imebadili jina na sasa kujulikana kama Jamii Africa huku ikijikita katika kutanua wigo wa kuwahudumia wananchi na wadau mbalimbali katika wigo mpana na mkubwa zaidi na si Tanzania pekee ikiwa ni pamoja na kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia na kuja na suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Maxence Melo, katika hafla ya uzinduzi wa jina na mwelekeo mpya wa taasisi hiyo leo Aprili 24, 2025 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Melo amesema mabadiliko haya yamelenga kuleta mbinu mpya na madhubuti za kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika sekta ya habari, uwajibikaji, na teknolojia barani Afrika.

“Tumeamua kuwa Jamii Africa baada ya kutafakari kwa kina. Tumegundua hatuwezi kupata matokeo tofauti tukibaki vilevile,” amesema Melo.

Ameeleza kuwa mchakato wa mabadiliko haya umehusisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwemo serikali, asasi za kiraia, vyombo vya habari na taasisi kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, DRC, Zimbabwe, na Afrika Kusini.

Jamii Africa inatarajia kuzindua jukwaa jipya Mei 2025 litakalohudumia zaidi ya Tanzania na kufikia nchi za Afrika Mashariki na Kusini. Lengo ni kuwapa wananchi taarifa sahihi zitakazowawezesha kufanya maamuzi bora.

Melo amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano, taasisi hiyo imefanikiwa kushirikiana na wadau wa serikali kwa mikataba 26, tofauti na lengo la awali la sita. Pia wamefanya kazi na zaidi ya asasi za kiraia na vyombo vya habari 40.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, taasisi hiyo imeandaa matukio makubwa ya kikanda yakiwemo yaliyojumuisha nchi za Afrika, na kuonesha uwezo wa Tanzania nje ya mipaka yake.

Ameeleza kuwa taasisi hiyo imeanzisha programu mbalimbali kama Story of Change, Jamii Check, na Fichua Ouvu, zinazolenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya uwajibikaji na uthibitishaji wa taarifa.

Akiongelea kuhusu mpango mkakati wa taasisi hiyo Melo amesema, unahusisha maeneo manne muhimu: kujenga mifumo ya kidijitali ya Kiafrika, kuimarisha uwezo wa vyombo vya habari na wananchi, kukuza ushirikiano katika utawala bora, na kuimarisha usalama wa kidijitali.

Sambamba na hilo, Jamii Africa imepanga pia kuzalisha vifaa vya kidijitali kama simu, kompyuta na tablets zenye maudhui ya ndani, zitakazosaidia katika utoaji wa elimu na taarifa sahihi kwa jamii.

Aidha, Melo amesema wamefanikiwa kuwajengea uwezo zaidi ya waandishi wa habari zaidi ya 1,000 nchini, na sasa wanaelekea kuwajumuisha katika muktadha mpana wa Afrika nzima.

Taasisi ya Jamii Africa kwa mwaka huu ni mwenyekiti wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, na imepanga kuleta wataalamu kutoka kampuni za kimataifa kama Meta na Google kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutumia teknolojia kwa tija.

Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Jamii Africa imechangia mabadiliko ya sera nne zinazohusu sekta ya kidijitali na sera tatu za vyombo vya habari, lengo likiwa ni kuwa na sera rafiki kwa mazingira ya sasa ya taarifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya, amesema ushirikiano wao na Jamii Africa utasaidia kuinua kiwango cha habari za Tanzania na kuzifikisha katika ngazi za kimataifa.

“Jamii Africa sasa ni jukwaa la waandishi wa Afrika wote na hata ulimwenguni,” amesema Simbaya.
Tutegemee ongezeko kubwa la nyuzi za hovyo sasa.
 
Jamii Africa sasa ni jukwaa la waandishi wa Afrika wote na hata ulimwenguni,” amesema Simbaya
 
Back
Top Bottom