King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 64,227
- 98,761
Imekaa njema sana ila Jamii Africa isije ikauza taarifa za Whistle Blowers na wanaharakati.
Wapo watu wa masoko na matangazo humu,itajulikana tuu vizuri na mambo yanaenda,Hakuna Cha kuharibika!Because JamiiForums has built a strong identity and reputation over the years, especially in Tanzania. Changing the name could dilute that recognition and confuse long-time users. It might also affect trust and traffic in the short term, as people may not immediately connect with the new brand.
Lkn mimi siyo muandishi wa habari.Jamii Africa sasa ni jukwaa la waandishi wa Afrika wote na hata ulimwenguni,” amesema Simbaya
Kwakweli hakuna sababu ya kubadili jina, JAMII FORUMS imesimama kidunia zaidi, labda kama pahala pa neno jamii lingekaa neno Tanzania. Hapo ingefaa kutoka "Tanzania forums" kwenda "Africa forums" hadi "Worldwide forums" ila "JAMII FORUMS" Hii imekaa kidunia bana, watuachie JF yetu kama ilivyo, na wao wabaki na JAMII AFRICA LTD, kama kampuni inayomiliki JF. Kama ambavyo META wamefanya kwa FACEBOOKMBONA JAMII FORUMS ILIPENDEZA TU NA HAIKO LIMITED! “JAMII AFRICA” IS VERY LIMITED, MAANA SIKU TUKITAKA KUJITANUA WORLDWIDE ITABIDI TUBADILI TENA JINA, ILA JAMII FORUMS IPO UNLIMITED MAANA YES NI FORUMS MBALIMBALI. KWAHIYO SIKU MKITAKA KUBADILI TENA JAMII AFRICA ILI IWE WORLDWIDE MTAIITA “JAMII WORLD??” JAMII FORUMS IS A BRAND ALREADY. FIKIRIENI HILO TAFADHALI.
ulitegemea atajiunga elon musk🤣🤣🤣.Mnabadili jina ila watu Wana IQ zile zile
Kama vipi atuuzie basi hii jamii forums, halafu yeye akaanzishe hiyo Jamii Afrika.Taasisi ya Jamii Forums imebadili jina na sasa kujulikana kama Jamii Africa huku ikijikita katika kutanua wigo wa kuwahudumia wananchi na wadau mbalimbali katika wigo mpana na mkubwa zaidi na si Tanzania pekee ikiwa ni pamoja na kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia na kuja na suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Maxence Melo, katika hafla ya uzinduzi wa jina na mwelekeo mpya wa taasisi hiyo leo Aprili 24, 2025 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Melo amesema mabadiliko haya yamelenga kuleta mbinu mpya na madhubuti za kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika sekta ya habari, uwajibikaji, na teknolojia barani Afrika.
“Tumeamua kuwa Jamii Africa baada ya kutafakari kwa kina. Tumegundua hatuwezi kupata matokeo tofauti tukibaki vilevile,” amesema Melo.
Ameeleza kuwa mchakato wa mabadiliko haya umehusisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwemo serikali, asasi za kiraia, vyombo vya habari na taasisi kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, DRC, Zimbabwe, na Afrika Kusini.
Jamii Africa inatarajia kuzindua jukwaa jipya Mei 2025 litakalohudumia zaidi ya Tanzania na kufikia nchi za Afrika Mashariki na Kusini. Lengo ni kuwapa wananchi taarifa sahihi zitakazowawezesha kufanya maamuzi bora.
Melo amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano, taasisi hiyo imefanikiwa kushirikiana na wadau wa serikali kwa mikataba 26, tofauti na lengo la awali la sita. Pia wamefanya kazi na zaidi ya asasi za kiraia na vyombo vya habari 40.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, taasisi hiyo imeandaa matukio makubwa ya kikanda yakiwemo yaliyojumuisha nchi za Afrika, na kuonesha uwezo wa Tanzania nje ya mipaka yake.
Ameeleza kuwa taasisi hiyo imeanzisha programu mbalimbali kama Story of Change, Jamii Check, na Fichua Ouvu, zinazolenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya uwajibikaji na uthibitishaji wa taarifa.
Akiongelea kuhusu mpango mkakati wa taasisi hiyo Melo amesema, unahusisha maeneo manne muhimu: kujenga mifumo ya kidijitali ya Kiafrika, kuimarisha uwezo wa vyombo vya habari na wananchi, kukuza ushirikiano katika utawala bora, na kuimarisha usalama wa kidijitali.
Sambamba na hilo, Jamii Africa imepanga pia kuzalisha vifaa vya kidijitali kama simu, kompyuta na tablets zenye maudhui ya ndani, zitakazosaidia katika utoaji wa elimu na taarifa sahihi kwa jamii.
Aidha, Melo amesema wamefanikiwa kuwajengea uwezo zaidi ya waandishi wa habari zaidi ya 1,000 nchini, na sasa wanaelekea kuwajumuisha katika muktadha mpana wa Afrika nzima.
Taasisi ya Jamii Africa kwa mwaka huu ni mwenyekiti wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, na imepanga kuleta wataalamu kutoka kampuni za kimataifa kama Meta na Google kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutumia teknolojia kwa tija.
Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Jamii Africa imechangia mabadiliko ya sera nne zinazohusu sekta ya kidijitali na sera tatu za vyombo vya habari, lengo likiwa ni kuwa na sera rafiki kwa mazingira ya sasa ya taarifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya, amesema ushirikiano wao na Jamii Africa utasaidia kuinua kiwango cha habari za Tanzania na kuzifikisha katika ngazi za kimataifa.
“Jamii Africa sasa ni jukwaa la waandishi wa Afrika wote na hata ulimwenguni,” amesema Simbaya.
I agree, nahisi kutakuwa na majukwaa empty either watu wanaposti hamna wachangiaji.Sioni JF ikitoboa Africa, tatizo kubwa Watanzania wengi hawajui Kingereza.
Watu ni sisi…Mnabadili jina ila watu Wana IQ zile zile