JamiiForums wabadilisha jina, Sasa kuitwa JamiiAfrica

Wapo watu wa masoko na matangazo humu,itajulikana tuu vizuri na mambo yanaenda,Hakuna Cha kuharibika!
 
Kwakweli hakuna sababu ya kubadili jina, JAMII FORUMS imesimama kidunia zaidi, labda kama pahala pa neno jamii lingekaa neno Tanzania. Hapo ingefaa kutoka "Tanzania forums" kwenda "Africa forums" hadi "Worldwide forums" ila "JAMII FORUMS" Hii imekaa kidunia bana, watuachie JF yetu kama ilivyo, na wao wabaki na JAMII AFRICA LTD, kama kampuni inayomiliki JF. Kama ambavyo META wamefanya kwa FACEBOOK
 
Kwa nje ni hatua kubwa ila ukilichunguza hilo jina ni kama tumewabagua mabara mengine na kulipendelea Bara la Afrika .

Aliyetunga jina la Jamii Forums alikuwa mbele ya muda ila aliyetunga jina la Jamii Africa yupo nyuma ya muda.
 
Nianze kwa pongezi hongera sana Mzee Max na wakurugenzi WENZAKO, menejiment nzima na wadai MLIO shirikishwa katika maboresho yanayoemdana na mabadiliko ya Jina

Pili hakuna furusa Badala ya JA IKAWA JFA MEANS JAMII FORUM AFRICA?😂💕😝😃👍
 
Kama vipi atuuzie basi hii jamii forums, halafu yeye akaanzishe hiyo Jamii Afrika.
 
Iwepo freedom ya Kuremove accounts au kudelete post.
Tusing'ang'aniane sana kama Mapenzi ya O level.
 
Watanzania wenzangu🙄 wapo wapi?


Uzi huu utanieleza mambo mengi hususan kuhusu wachangiaji wa Kitanzania

Nauliza wapo wapi?

Kitaeleweka.
 
Naona wamefikiria kwa mtazamo mdogo Sana ..... yaani Mm taarifa za Zimbabwe n.k sizijui ila namleta Mzimbabwe azijue zangu kupitia mgongo WA kupanua wigo...

Hata WAtz wenyewe JF hawaijui vzr ao WA nje tunawaleta WA nn sasa
Maswali ya msingi
1.Kama uchangiaji Tu WA majukwaa kama English Forum ni watochi je tukiongeza Watu tutatua tatizo?
2.Usalama WA taarifa uko wapii?maana kama Browser ilishawai chezewa,Je wakiongezeka tutawamudu?

3.Mods hawatokuwa na upendeleo kwa upande wowote?

4.Mabadiliko yameshirikisha wadau kutoka mataifa mengi Ila Sisi wenyewe Wana JF Huo mchango mm sijawai uona ,Je haya mliyoongea Yana ukwl?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…