JamiiForums ya Maxence Melo imenipatia mume. Clepatina naolewa

JamiiForums ya Maxence Melo imenipatia mume. Clepatina naolewa

"Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana."
MITHALI 18:22.

Wapendwa nilitaka nipotee kimya kimya, ila kwa namna hii ID yangu ilikaribishwa kwa upendo na kwa upendo nilionao kwa marafiki na ndugu zangu zangu niliojipatia hapa JF nimeona sio ubinadamu nikaitelekeza hii ID bila kuwaaga halafu niwaache wapendwa wangu wakijiukiza Clepatina kapatwa na nini mbona kapotea jukwaani.

Wapendwa, Mungu akitoa kibali November ninaolewa na mchumba niliyempatia hapa JF.[emoji1787][emoji3590].

Huyu jamaa hajanikuta single. Alinikuta nikiwa kwenye uhusiano na jamaa ambae hata hapa jukwaani nishawahi kumtaja kama Mgweno.

Kwa huyu mgweno ndiko moyo wangu uliko. Nilimpenda sio kwa moyo wangu wote bali kwa vyote vilivyotumika kuniumba. Nilimpenda sana huyu mwanaume kiasi cha kuwaona wanaume wengine wote walionitongoza kama wachumba tu[emoji1787].

Baadae nikagundua ninampenda Mgweno zaidi ya anavyonipenda na nikawa mtu wa kulalamika kila siku.

Hata hivyo Mgweno ndio aliyesababisha huyu shemeji yenu mpya atangaze ndoa fasta fasta.

Ni hivi,wakati nakutana na Mgweno nilikua na stress sanaa kiasi kwamba nilikua naonekana kama nina mara mbili ya umri wangu. Nilikua nimechoka sana. Nilikua kibibi[emoji1787] lakini mahaba na faraja alizonipa Mgweno zikarudisha peace of mind na stress zikaisha na Clepatina nikawa pisi kali tena[emoji1787].

Amini usiamini, mwanamke akipendwa na mwanaume anayempenda uzuri wake unarudi[emoji1787]. Ndio maana mtu ukiwa single hufatwi ila ukipata tu wa kukupenda utashangaa kila mwanaume anakutaka[emoji1787].

Sasa baada ya kuona Mgweno haeleweki/kabadilika nikapambania penzi haijasaidia, ndio kajitokeza huyu shemeji yenu mpya na japo hatuna muda mrefu na siwezi kusema namjua vizuri ila nafsini mwangu nahisi amani juu yake.

Kwa hatua alizochukua na gharama alizoingia juu yangu nina imani yuko serious katika kutaka kunioa.

Yeye na familia yake yote ni walokole kama mimi na ninajihisi salama kuwa mikononi mwa mwanaume amchae Mungu.


Ndugu zangu, mwanaume Mcha Mungu, msomi, mwenye ofisi zake kubwa kubwa, handsome, mpole ila mkali kwenye upuuzi, asiyependa wanawake wengi na mwenye mapenzi kama kapewa limbwata, hatoki kokote zaidi ya Mbinguni kwa baba Mungu, Mungu wa ishara na miujiza. Mgweno anisamehe ila naamini huyu ndie niliumbwa toka ubavuni mwake[emoji3590].

Hii itakua ni post yangu ya mwisho hapa. Kwa sasa najikita zaidi kusoma biblia kama alivyoniomba mume wangu mtarajiwa na pia kutumia free time yangu kujifunza kupika. Sijui kupika ndugu zangu[emoji24] na shemu wenu kasema kutojua kwangu kupika ni tatizo na mpaka siku ananioa niwe nimeshajua kupika.

Najua ndoa zina changamoto, najua mume wangu mtarajiwa atakuwa na madhaifu yake, najua kuna siku za kulia na siku za kucheka najua kuna siku tutapata na kuna siku tutakosa najua kuna mengi mazuri na mabaya yatajitokeza ila hata itokee nini kamwe sitafanya yafuatayo;

1) Sitamcheat hata akipoteza dushe yake.

2) Sitamdharau hata akikosa uwezo wa kunipa jero.

3) Kamwe sitajiona nina akili kumshinda.

4) Kamwe sitapaza sauti yangu ninapoongea nae.

5) Kamwe sitonyanyasa watoto wake ambao mama yao amefariki, kwani tayari nawapenda na wao wananipenda kama nimewazaa mimi.

Kwa mnaonipenda naombeni mniage kwa neno zuri la ushauri.

Joannah Half american Gily
I CAME, I SAW, I CONQUERED.

Kweli we mlokole, hiyo Pete Kama ya silver, watoto wa siku hizi mnafeli wapi, mi dada yako hiyo Pete sijaikubali, kitu za dhahabu hata akikuacha unaenda sonara unauza unapata Cha kuanzia kuuza genge.
 
Muda wa spana huu[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Ngoja nivute popcorn na ka duvet na haka kabaridi [emoji38]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mbna mambo maresh maresh.
Woiiiiiiih
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Uduguu usifanye hivyo tutamzika bro kabla ya muda wake! Muonee huruma bas
Uduguu hapanaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] huyo ndugu zake hawanipendii, ko na mie namuachaaaa
Sitaki visa vya reja reja ukweniiiiii.

Woiiiiiiih
 
Yani hapa ninaifikiria ile nyimbo ya basi nenda sikumbuki jina la msanii...Ila kichwa kina vitu vingi by young lunya ni best of all, Maana naona shoga zake wananipakazi maushenzi 🤣🤣
Clepatina
this guy IamBrianLeeSnr sitaki kumsemehea but just logic. He doesn't have girls here if he could openly show his love for you publicly. He doesn't care what he is losing rather than losing you. He is hurting 😢 💔 and with broken heart.

He is laughing outside but crying inside💔
Love is beautiful thing, what is sad is not you saying no. It's just you didn't give him a chance❤️ and say no when you get to know him.
Screenshot_20230531_003032_Google.jpg
 
Back
Top Bottom