JamiiForums ya Maxence Melo imenipatia mume. Clepatina naolewa

"Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana."
MITHALI 18:22.

Wapendwa nilitaka nipotee kimya kimya, ila kwa namna hii ID yangu ilikaribishwa kwa upendo na kwa upendo nilionao kwa marafiki na ndugu zangu zangu niliojipatia hapa JF nimeona sio ubinadamu nikaitelekeza hii ID bila kuwaaga halafu niwaache wapendwa wangu wakijiukiza Clepatina kapatwa na nini mbona kapotea jukwaani.

Wapendwa, Mungu akitoa kibali November ninaolewa na mchumba niliyempatia hapa JF.šŸ¤£ā¤ļø.

Huyu jamaa hajanikuta single. Alinikuta nikiwa kwenye uhusiano na jamaa ambae hata hapa jukwaani nishawahi kumtaja kama Mgweno.

Kwa huyu mgweno ndiko moyo wangu uliko. Nilimpenda sio kwa moyo wangu wote bali kwa vyote vilivyotumika kuniumba. Nilimpenda sana huyu mwanaume kiasi cha kuwaona wanaume wengine wote walionitongoza kama wachumba tu🤣.

Baadae nikagundua ninampenda Mgweno zaidi ya anavyonipenda na nikawa mtu wa kulalamika kila siku.

Hata hivyo Mgweno ndio aliyesababisha huyu shemeji yenu mpya atangaze ndoa fasta fasta.

Ni hivi,wakati nakutana na Mgweno nilikua na stress sanaa kiasi kwamba nilikua naonekana kama nina mara mbili ya umri wangu. Nilikua nimechoka sana. Nilikua kibibi🤣 lakini mahaba na faraja alizonipa Mgweno zikarudisha peace of mind na stress zikaisha na Clepatina nikawa pisi kali tena🤣.

Amini usiamini, mwanamke akipendwa na mwanaume anayempenda uzuri wake unarudi🤣. Ndio maana mtu ukiwa single hufatwi ila ukipata tu wa kukupenda utashangaa kila mwanaume anakutaka🤣.

Sasa baada ya kuona Mgweno haeleweki/kabadilika nikapambania penzi haijasaidia, ndio kajitokeza huyu shemeji yenu mpya na japo hatuna muda mrefu na siwezi kusema namjua vizuri ila nafsini mwangu nahisi amani juu yake.

Kwa hatua alizochukua na gharama alizoingia juu yangu nina imani yuko serious katika kutaka kunioa.

Yeye na familia yake yote ni walokole kama mimi na ninajihisi salama kuwa mikononi mwa mwanaume amchae Mungu.

Ndugu zangu, mwanaume Mcha Mungu, msomi, mwenye ofisi zake kubwa kubwa, handsome, mpole ila mkali kwenye upuuzi, asiyependa wanawake wengi na mwenye mapenzi kama kapewa limbwata, hatoki kokote zaidi ya Mbinguni kwa baba Mungu, Mungu wa ishara na miujiza. Mgweno anisamehe ila naamini huyu ndie niliumbwa toka ubavuni mwakeā¤ļø.

Hii itakua ni post yangu ya mwisho hapa. Kwa sasa najikita zaidi kusoma biblia kama alivyoniomba mume wangu mtarajiwa na pia kutumia free time yangu kujifunza kupika. Sijui kupika ndugu zangu😭 na shemu wenu kasema kutojua kwangu kupika ni tatizo na mpaka siku ananioa niwe nimeshajua kupika.

Najua ndoa zina changamoto, najua mume wangu mtarajiwa atakuwa na madhaifu yake, najua kuna siku za kulia na siku za kucheka najua kuna siku tutapata na kuna siku tutakosa najua kuna mengi mazuri na mabaya yatajitokeza ila hata itokee nini kamwe sitafanya yafuatayo;

1) Sitamcheat hata akipoteza dushe yake.

2) Sitamdharau hata akikosa uwezo wa kunipa jero.

3) Kamwe sitajiona nina akili kumshinda.

4) Kamwe sitapaza sauti yangu ninapoongea nae.

5) Kamwe sitonyanyasa watoto wake ambao mama yao amefariki, kwani tayari nawapenda na wao wananipenda kama nimewazaa mimi.

Kwa mnaonipenda naombeni mniage kwa neno zuri la ushauri.

Joannah Half american Gily
I CAME, I SAW, I CONQUERED
Hongera,zingatia hapo ulipoambiwa usome neno la Mungu na uhakikishe unaliishi,hiyo ndio itakuwa salama yako,kinyume cha hapo utaambulia mabua,maana umeingia kwenye ulingo ambao shetani anauwinda na kuupiga vita usiku na mchana...
 
Juzi umejifungulia Uzi kwa ID nyingine na Leo umekuja kujijibu..

Inabidi saa hizi tutumie NIDA kuwa na account JF, Ili ukitaka kucreate nyingine ikugomee tu
 
Kwa nini umamuombea mabaya mwanadamu mwenzako. Huwezi kusema Eh Mola naomba mabaya yampishe mpaka umtabirie mabaya?
I believe in Karma, lazima ulipie.
Hata matatizo mengi ya ndoa za saivi yanatokana na karma, esp wale wanaoana mume alikuwa mnunuaji/mhongaji mke alikuwa mchunaji/mdangaji they will never know peace labda unless they make make peace with themselves first, Sina mambo ya kupeana moyo nikuchanana ukweli, I'm not religious person
 
IamBrianLeeSnr akija naomba unitag. Toka juzi sijamuona sijui kama hata alilala nyumbani šŸ˜‚ Nilimshauri ameze panadol mbili usikute alimeza mseto kibunda kizima
Demu chenga huyu anawenge kilo 100 hata kupika hajui šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚ Clepatina hahahaaa... nasema huyo mlokole wa watu atakufa mapema sana, Bado unavingi vya kujifunza tukutane... Mbeleni nipo na wewe sambamba 🤣🤣🤣
 
kamwe sitafanya yafuatayo;

1) Sitamcheat hata akipoteza dushe yake.

2) Sitamdharau hata akikosa uwezo wa kunipa jero.

3) Kamwe sitajiona nina akili kumshinda.

4) Kamwe sitapaza sauti yangu ninapoongea nae.

5) Kamwe sitonyanyasa watoto wake ambao mama yao amefariki, kwani tayari nawapenda na wao wananipenda kama nimewazaa mimi.

Mpendwa.

Inaonekana unajitambua na unaitambua nafasi yako kama mke; na hauko kama hawa pasua kichwa feminists uchwara wanaojifanya wanajua kila kitu kisa tu wamesoma, wana viajira (au vijihela vyao) na sasa eti wanajiona wako sawa na mwanaume!

Ukiweza kutimiza japo robo tu ya ahadi hizi "takatifu" ulizojiwekea basi kwa hakika utakuwa mke mwema; jamaa atakuwa amepata bonge la mke; na wanaume wengi watamwonea wivu.

Mungu na Akawasaidie na kuibariki ndoa yenu.....

Screenshot_20230602_085347_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom