Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
“Uwezekano wa binadamu aliyekulia kwenye mazingira yenye upendo, furaha na amani kuwa mbabe, katili anayefurahia na kukejeli maumivu ya wenzake ni sawa na sifuri. Ukatili si asili yetu. Nadra sana binadamu kuzaliwa katili isipokuwa inapotokea kazaliwa na hitilafu za kibaiolojia.” Mwisho wa kumnukuu mwanasaikolojia Chris Bwaya.
Mambo tunayoyaona sasa kwenye siasa yanachangiwa kwa namna moja au nyingine na makuzi ambayo tumejijengea majumbani na kwenye mifumo yetu ya elimu. Imekuwa kawaida kupiga watoto kupita kiasi, kuwaadhibu bila huruma, kutotenga muda kuwasikiliza, kuwatengenezea uoga na kutoruhusu watoto kuchallenge - asipokubaliana na wewe kidogo mtoto au kijana ataambiwa ana kiburi au ni jeuri na kuadhibiwa.
Unapolea na kukuza mtoto hivi , ni nadra sana kuwa kuwa mtu mzima ambaye ana ubinadamu, utu au ambaye anakubali kukosolewa hasa akipewa mamlaka. Wazazi hasa akina mama tuna kazi kubwa ya kulea watoto kwa upendo na kuwaonyesha vile wanatakiwa kuwa ukubwani kupitia matendo yetu.
Jali mtoto, samehe, muonyeshe huruma, acha kuadhibu kupita kiasi, mjengee ujasiri na kujiamini, msifie mtoto siyo kila wakati kumkosoa pekee, tenga muda na ufanye naye vitu vya kumpatia furaha n.k. Tukitaka taifa la watu tofauti, tulee na kukuza watoto na vijana kwa utofauti tunaotaka kuuona wakiwa watu wazima, viongozi au wenye mamlaka.
Namaliza tena na nukuu ya Chris “Ukatili wa mtu, kwa kawaida, ni jitihada za kujisahaulisha upweke, kupooza majeraha yanayotokana na kudhoofu kwa mahusiano na familia yake. Mtu katili ni ama ana historia ya utoto wenye unyonge, maumivu, kuonewa, kudhalilishwa ama basi anauguza majeraha ya mahusiano ya ukubwani”
CC:
Ushimen