Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
Nimekopi meseji kama nilivyoipokea.
************
Dada shikamoo,
Miaka 4 iliyopita niliolewa na mwanaume wa Kitanzania anayeishi South Africa. Nimezaa naye mtoto mmoja na nina ujauzito wa mtoto wetu wa pili. Huyu mwanaume alinikuta na mtoto mdogo wa miaka 2 ambaye baba yake alifariki kwa ajali ya gari nikabaki namlea peke yangu.
Baada ya kunioa alisema atamchukua mtoto wangu kama mtoto wake wa damu na kweli akawa anatuhudumia kwa kila kitu. Baada ya kuoana tukaanza na kufuatilia na process za kuasiri (adoption) kisheria. Sasa wiki iliyopita tumefanikiwa wote kuhamia South ila nilivyofika huku amenikalisha chini akasema hawezi kumuadopt mtoto wangu wala kumuweka kwenye makaratasi ya residence kama mwanaye kwa sababu ikitokea tumeachana au nimetangulia atabaki na jukumu la kulea mtoto ambaye si damu yake, litabaki kwake.
Nimeumia sana, nahisi maumivu na hasira mwanangu kukataliwa na kutengwa.
Nilimleta mtoto huku SA nikijua naye atanufaika kama wenzake ila mambo yamekua tofauti, sijui nifanyaje, naomba nishauri dada.
***********
MSAIDIENI JAMANI AFANYAJE NA YUKO UGENINI!