JAMVI LA WANAWAKE: Mshaurini binti kayavaa na mwanaume wa South Africa

JAMVI LA WANAWAKE: Mshaurini binti kayavaa na mwanaume wa South Africa

Kama Mtanzania kapata uraia SA mambo ya adoption sio rahisi kama mnavyodhania kwa SA.
Amtafutie shule nzuri aombe vibali vya kuishi kwenye Ubalozi wa SA uliopo Tanzania ishu ndogo tu hiyo analipia Tsh 80,000 akikaa kwa muda mrefu atapata sifa za kupata permanent resident permit ya kwake mwenyewe bila kupitia kwa mtu maana baadae inaweza kumsumbua...
Hapo ugomvi ni huyo mtoto nae awepo kwenye mgawanyo wa Mali Dada ajatoa code hakuna Baharia wa hapa SA ashindwe kukaa na mtoto wakati watu wazima tu humjui katokea wapi huko Tanzania unampa hifadhi mpaka awe na uwezo wa kujitafuta ndio anatoka home pana code zimefichwa hapo kwa wasafiri ni rahisi kujua.
 
Ili tu abaki na ndoa?

Huu ushauri wa 2 na 3 unaweza kumshauri Dadako au binti yako ?
Natoa ushauri kutokana na muktadha uliopo,sitoi ushauri ili kumridhisha mtu yoyote yule,ama kuhusu dada yangu ama binti yangu nitamshauri vipi,pia itategemea muktadha wa hilo tatizo na iwapo muktadha utafanana basi huyo mtoto ntamchukua mimi ili yeye aendelee na ndoa yake kwa amani na furaha
 
Huyo mwanaume anawaza mali zake kumpa mtoto sio wake, muhimu yeye kwenye kipato chake anunue assets amwandike huyo mtoto…!!

Kuhusu huduma zingine muhimu km chakula na afya yake haina shida…!! Mbona hata bongo watu wanalelewa na baba sio wao lakini maisha yanaenda.!!

Kabla sijasahau; Huyo marehemu mumewe hakuacha urithi wa watoto wake? Na huyo mtoto mwingine yeye vipi yuko wapi? Umesema wako wawili…!!
 
Ni kweli mtoto anahudumiwa, ila huko ugenini atakosa haki nyingi kwa sababu siyo mtoto wake bali mtegemezi wa mkewe.
Jiulize alimzaa ugenini,Hana ndugu wengine amuache Tza.
Akiona vipi abebe watoto akaishi Tanzania kwenye haki nyingi.....
1000073287.jpg
 
Uzalishwe na mwanaume Mwingine Kulea akulele mwingine then baadae unamnanga kwa kumuambia mtoto huyu sio babaako.
Soma vizuri, ameolewa akiwa na mwanae ambaye baba yake amefariki, na jamaa akakubali kuwa atamlea, akafanya process zote za kuwahamishia huko SA. Eti wamefika huko ndio anakataa kundelea na hizo process za ku asili na nyingine. Kenge tu.
 
Kang'amua kitu na huyo dada kwa nn ghafla tu akimbilie mtandaoni!?je atakimbilia wapi pengine endapo huyo mtoto wake ataonekana hapati haki yake kutoka kwa baba wa kambo !?
Inaonekana yuko Kasi sana na analengo tofauti na huyo mwanaume
 
Amlee tu ashakua mwanae ata wakitengana atakua na mtu wa kumfariji so ampambanie kivyake maana awezi jua la mbeleni
 
Soma vizuri, ameolewa akiwa na mwanae ambaye baba yake amefariki, na jamaa akakubali kuwa atamlea, akafanya process zote za kuwahamishia huko SA. Eti wamefika huko ndio anakataa kundelea na hizo process za ku asili na nyingine.

Mwanamke kaonyesha upuuzi yaani ukaasili mtoto ambaye ni mwanae ambae huyo mwanaume alimjua before ni nini kama si undezi kuna nini special anataka huyo mtoto apate kwa huyu baba. Au kuna mpango gani anapanga why amuasili mtoto wake mama wa kumzaa wakati alishapromisiwa kuwa atalelewa.
Ange explain in detail akitoa na concrete reason na examples kuna nini special anakihitaji huyo mtoto apate kwa kuhalalisha hilo alitakalo mwanamke?

Hapa kuna maswali mengi yakujiuliza kuliko majibu hasa dunia hii ilovaa chupi yenye mapenzi ya kupenda kwasababu ya manufaa fulani isiyo na mapenzi ya kweli Bali ya fursa
 
Huyo mwanaume Amepata ushauri mbaya kutoka kwa marafiki zake.
Mbona issue ni ndogo maana huyo mtoto wa marehemu ni ndugu na watoto wake aliozaa na wewe mwanamke sasa kwanini asimsaidie huyo mtoto na ukizingatia ni mkubwa kuliko wanae who know atakuja kuwalea wadogo zake.

Wewe kataa kuwalea watoto kiubaguzi walee wote kama baba yao ni mmoja na wawe na umoja huyo mwanaume atajirudi tu.
Nilivyoelewa kumlea na kumsaidia hajakataa ila kumu adopt awe wake kabisa ndio kwa sasa hataki. Kwa mimi naona sio tatizo mbona ndio wengi wanaish hivyo.
 
Kwanza jamaa kakosea maake alishakubali kumchukua mama na mtoto, kwann wafike sauzi amtose Tena mtoto? Kwamba alihitaji tuu mapenzi kutoka kwa bibiye ?

Nadhani mwanaume ajifikirie vizuri juu ya hili ukitoa ahadi kama hiyo ajitahidi kuitekeleza ama atafute njia ya kumsaidia huyo mtoto,

Huyo bibiye alizaa na mwanaume tuu ? Au walikuwa wanandoa mpk jamaa anafariki if yes naona awatafute ndugu wa mume, awaeleze indirect way wamchukue mtoto wa ndugu yao, hata kama walizaa wakiwa wapenzi kwa jamii yetu wakithibitisha huyo mtoto ni wao wanamchukua.

Pengine bibiye akiwa sauzi ajitahidi kutafuta pia NGO's za kusaidia watoto kama wanaotokea mazingira magumu ili asaidike,

WAnaume baadhi tuache upumbavu, humtaki single Maza achana naye. Karma iz real
 
Back
Top Bottom