JAMVI LA WANAWAKE: Mshaurini binti kayavaa na mwanaume wa South Africa

Huyo mwanaume Amepata ushauri mbaya kutoka kwa marafiki zake.
Mbona issue ni ndogo maana huyo mtoto wa marehemu ni ndugu na watoto wake aliozaa na wewe mwanamke sasa kwanini asimsaidie huyo mtoto na ukizingatia ni mkubwa kuliko wanae who know atakuja kuwalea wadogo zake.

Wewe kataa kuwalea watoto kiubaguzi walee wote kama baba yao ni mmoja na wawe na umoja huyo mwanaume atajirudi tu.
 
Shida baadhi ya wanawake akiwa natatizo au changamoto ni mtiifu sana

Cha ajabu akiwa na uwezo pasi na kuhitaji tegemezi ndipo utamjua kila rangi

Sijabariki mtoto kubaguliwa ila kama anapata mahitaji muhimu bidada atulie

Wanaume tunadesturi ya kuishi kesho kwahiyo ukimsoma mwanamke wako tayari alarm inalia
 
Nakubaliana na wewe 100%
 
Apeleke mtoto kwa vituo vya kulelea watoto wakati mama yupo hai? Jamani....
 
Heshima mbele wanajukwaa.

Kwanza, huyo mwanaume alifanya jambo zuri kumchukua bibie single maza akaenda nae sauzi.

Pili, bibie kakosea kumwamini mtu 100%.

Tatu, huyo jamaa hana msimamo kazingua kwanini akubali wakiwa Tanzania, halafu wafike sauzi abadilike, huyo ni boya. Kama anajua baba wa mtoto alifariki kwanini akatae,
mtoto ni baraka anaona so dogo(mtoto asiewake) kuwa mrithi wa vitu vyake.

Nne, huyo mwanamke amfate mwamba wayasort kiutu uzima, kama atagoma apewe shase yake au nauli tu arudi bongo.

Tano na mwisho, leo sina ushauri kwa mtu anaetaka kukata tamaa kama anataka kukata tamaa yeye akate tu mi mwenyewe nimetingwa sio poa.
 
Duuh hiyo namba 3
 
Kwani huwa mnafikiria mabaya tu?
Vipi kama mtoto atawasaidia wadogo zake akikua? vipi kama mtoto atafanikiwa na kuwa msaada kwa baba yake akizeeka?
Shida iko hapa
Kama ilivyovigumu wanawake kulea watoto wa mwanamke mwingine aliyeachana na mumewe na iwe vivo hivyo.

Jinaume lingine lipige mbupu na kulikuwa kwa utamu libebewe mimba then lipo linatanua mtaani na ndugu zake huyo jinaume wapo eti wanaume tulee wasio wetu hii hapana

Hii iwe somo kwa wanawake wote beba ujauzito wa mwanaume aliyetayari kulea mtoto.

Mwanaume Lea mtoto yatima pekee ila makesure umeonyeshwa kaburi na cheti cha kifo cha huyo baba ili usijejidhuru kwa stress kwani wanawake wameweka hisia mbele waweza jitoa kwa kulea ukajapigwa na kitu kizito
 
Ili tu abaki na ndoa?

Huu ushauri wa 2 na 3 unaweza kumshauri Dadako au binti yako ?
 
Kwani huwa mnafikiria mabaya tu?
Vipi kama mtoto atawasaidia wadogo zake akikua? vipi kama mtoto atafanikiwa na kuwa msaada kwa baba yake akizeeka?
Kwa mwanamke kila afanyalo mwanaume ujue mbeleni Lina masimango dhidi yake.
Nimlee bila ubaguzi mtoto akijua mm babaye,akianza kufanikiwa mwanamke unamwambi huyu si baba yako na sumu kibao, ukoo wako ni huu (egemeo kuwa mwanaume ukifulia mkitofautiana ye kwa mwanaye). Wanaume Hawa wanawake siyo wa kuwabeba mizigo yao abadani.

Mtasema Nina ubinafsi na mifano ya born 80s- 90s kufanyiwa vyema, je Hawa wachumia tumbo wa sasa mmewaangalia wanvyowatenda wanaume?


Mwajua kulea mtoto nyie , siyo kuzaa huko yaani kipindi kirefu Cha maisha yako mpaka afanikiwe uwekeze kwa ajili yake.


Kesho yake tena kwa nauli yako mama yake anaenda kumuonesha ukoo wake! Ulitumia nguvu ,pesa na muda mpaka kutumia jina lako, atatumia the same kurudi kwenye jina lake.

Omba yasikukute haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…