Jana niliionea huruma sana familia ya Polepole

Jana niliionea huruma sana familia ya Polepole

Dennis Robert Shughuru

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2024
Posts
5,559
Reaction score
8,747
Jana kuna barua ilikuwa ina-surface mtandaoni iliongelea mambo mengi ila sehemu iliyonifikirisha sana ni pale waliposema mazingira ya siasa nchini yapo vizuri nikaachia kusoma pale sikuendelea tena sababu nilisikia uchungu mkubwa sana

Nikajiuliza familia ya polepole inajisikiaje inaposoma ile sehemu inaposema mazingira ya siasa yapo shwari inaumiza sana ni sawa na kuchomwa na msumari wa moto

Tokea polepole alivyotekwa na habari iliropotiwa kutoka kwa ndugu zake sikutaka kuongea chochote kwa kusubiria mamlaka zitoe taarifa rasmi

Mimi polepole sikubaliani naye hata huku jamiiforums kuna thread nyingi sana nampinga kama binadamu hakustaili yale madhila ya kuja kubebwa kama kuku na kipigo juu sababu ile scene ina damu ni wazi wakati ule ulikuwa ni wa maumivu makubwa sana kwake na mpaka sahivi haijajulikana ni nani alikuja kumchukua

Na hapo sijaongelea watu wengine ambao walichukuliwa na hawajulikani hawapo

KWA UCHUNGU MKUBWA SANA BAADA YA MDA MLE SIJUI NILIPATA WAPI ILE BOULDNESS NIKAMUULIZA MUNGU HIVI KWELI HIVI NDO MAISHA YETU YANATAKIWA YAWEPO NA HOJA YANGU ILIJIKITA KWENYE MASWALI MAWILI
  1. Kama haya ndo maisha yetu uliyotupangia tupe nguvu ya kuweza kupuuzia haya yanayotokea
  2. Kama sio ndo maisha yetu unaujumbe gani wa matumaini kwetu

A)-Nilishika biblia na kuomba kwa dakika kadhaa nikafungua na kupelekwa mpaka
1 Samwel 16
Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.


B)-Nikasali tena mara ya pili nikapelekwa mpaka
Ezekiel 32

I-kawa katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana likanijia, kusema,

2-Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwana-simba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.

3-Bwana MUNGU asema hivi; Nitautanda wavu wangu juu yako, kwa kusanyiko la watu wa kabila nyingi; nao watakuvua katika jarife langu.

4 Nami nitakuacha juu ya nchi kavu, nitakutupa juu ya uso wa uwanda, nami nitawaleta ndege wote wa angani watue juu yako, nami nitawashibisha wanyama wa dunia yote kwako wewe.

5 Nami nitaweka nyama yako juu ya milima, na kuyajaza mabonde kwa urefu wako.
Unaweza endelea mpaka mstari wa 32

C)- Nikasali tena kwa ya tatu na mwisho nikapelekwa
Mathayo 1
 
Kontak: WhatsApp di +62 81944399827.
Nyie mpo hapa wengi sana sasa hivi. mnalipwa kuvuruga kila mjadala muhimu kwa maslahi ya Taifa.

Mnatumia mbinu mbalimbali kama hizi, matusi, kuweka vitu ambavyo havihusiani na mada ili kuvuruga mijadala.
 
Nyie mpo hapa wengi sana sasa hivi. mnalipwa kuvuruga kila mjadala muhimu kwa maslahi ya Taifa.

Mnatumia mbinu mbalimbali kama hizi, matusi, kuweka vitu ambavyo havihusiani na mada ili kuvuruga mijadala.
Wanazingua sana yaani kazi yao ni kuharibu uzi
 
Back
Top Bottom