Utapata tabu sana. Soma ripoti ya IMF hapa
https://www.imf.org/-/media/Files/Publications/CR/2023/English/1CHNEA2023001.ashx labda ikusaidia kuelewa matatizo yaliyopo china. IMF wanaandika diplomatically sana lakini just read between the lines ndipo ufunguke akili.
Haya mambo ya serikali kupika data hata hapa kwetu wapo na kila wanapotoa ripoti huwa hawazipindi namba hizo ila wanaweka postscript note kuhusu namba zetu hizo
Nini kinachokushangaza mkuu kwenye hiyo report ya IMF ya 2022 kuhusu China?
Wakati ripoti yenyewe imesema na inajulikana kuwa mwaka 2022 China wali-adapt zero-Covid policy na ndio maana uchumi wa China ulipanda kwa 3.8% tu mwaka 2022 kutoka 8.5% mwaka 2021. Na ndio rekodi mbaya zaidi kwa China ndani ya miaka 40
Kitendo cha China kuadapt zero-Covid policy kiliathiri global supply chains.
Ndio maana mkutano wa mwaka huu wa G7 pale Japan, mataifa ya G7 yalikuwa yanailaumu China kuufungia uchumi wake.
Hapo ndo ujue kuwa uchumi wa China una impact kwenye dunia.
Uchumi wa China umefunguliwa rasmi mwaka huu 2023, ona sasa ndani ya miezi 3 ya mwanzo (Q1) tu baada ya kuufungua uchumi;
●Ndani ya miezi 3 uchumi umekua kwa 4.5%
●Ndani ya miezi 3 wameiovertake Japan na kuwa the world's biggest vehicles exporter
●Ndani ya miezi 3 Kwa mara ya kwanza katika historia ya mauzo ya nje ya bidhaa za China (China's crossborder transactions) mauzo kwa kutumia Yuan yameipiku US dollar
●Ndani ya miezi 3 uzalishaji viwandani umekua kwa 3.9%
●Service sector imekua kwa 5.4%
●Retails sales 5.8%
●Export 23.4%
●Investment in fixed asset 5.1%
●Investment in infrastructure & manufacturing 8.8%
●investment in high-tech industries 15.2%
●Investment in high-tech services 17.8%
●Low inflation rate (wakati mataifa mengine makubwa kiuchumi yakisumbuliwa na inflation China imekuwa na low inflation rate)
WB na IMF kwenye forecast zao za mwaka 2023 wameripoti kuwa uchumi wa China utakua kwa 5.6% au zaidi.
WB GDP growth forecast 2023
👉U.S.A 1.1%
👉Japan 0.5%
👉Ulaya 0.4%
👉Germany -0.1%
👉UK -0.3%
👉Canada 2.8%
👉South Korea 1.6%
Baki kusema tu uchumi wa China unaporomoka mkuu, wakati G7 na washirika wao uchumi hoi