Janeth Ndimbo afikishwa Mahakamani kwa mashtaka 8 ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
​

Mkazi wa Sinza Mori, Janeth Ndimbo (30) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka manane ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Amefikishwa mahakamani hapo leo Agosti 4, 2026 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.

Mshtakiwa amesomewa mashtaka hayo na wakili wa Serikali Mwandamizi, Harbert Kamugisha.

Wakili Kamugisha alidai katika shtaka la kwanza, tarehe isiyofahamika Juni, 2024 Wilaya ya Kigamboni, mshtakiwa alimwajiri Mina Ntengule chini ya kivuli cha kupata ajira nje ya nchi kwa lengo la kunyanyaswa kingono.

Pia, Agosti 1, 2024 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mshtakiwa huyo anadaiwa kumsafirisha Mina kwenda Guangzhou, nchini China.

Kamugisha aliendelea kudai kuwa, tarehe isiyofahamika Juni, 2024, eneo la Sinza Dar es Salaam, mshtakiwa alimwajiri Ana Bernard Gabriel kwa kivuli cha kupata ajira za nje ya nchi.

Mwananchi
 
Hana hea huyu😀😀
 
Mbona mweupe kama mchina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…