Janga la Betting kwa Watanzania tujiandae na rehab center

Janga la Betting kwa Watanzania tujiandae na rehab center

Umekua mkweli.
Hivyo vyanzo vi2 vitaleta pesa kwenye Betting, hakuna mtu anabet ili awe addicted
Betting usijaribu ni addiction ambayo wazee wetu hawajui kama ni addiction wao wanajua ni madawa tu ndio yanaleta addiction kwaio wanaunderrate
 
Haya ni majanga ya chama cha majambazi
Yapate utatuzi kwa waathirika wote tuokoe jamii ,naami wapo wengi kwenye familia ila kwakua ni mchezo wa siri ni ngumu kujua unashangaa mtu anaumwa moyo au presha ila sababu haijulikani na mwenye shida anaona aibu kusema ila wakienda rehabs wanakuwa open
 
Kaka kwa akili ya kawaida huwezi kukubaki kuliwa pesa nyingi ila kutoka na uraibu akili ya kawaida haifanyi kazi hapo mwili,kila ukitaka kuacha huwezi kwasababu muda huo mwili unatakiwa kurelease dopamine ili ujisikie vema
Kuacha unaweza kama haubeti kupata hela ya kula.
Ukitaka kuacha inabidi uachane na watu wanaobeti, uache kuhifadhi hela kwenye simu.
 
Hehehe.
Nafurahi sababu bado hujaijua kamari vzr, stake ya 3000 usiitumie kumotivate watu mkuu kuingia kwenye hili demon
Najua hilo mkuu na kuna siku niliweka 1m ndani ya dkk 10 mkeka uka ungua ile siku nilijiona bongee la falaaa

Nikaja kuweka tena 10k nikala laki 320....na apo ndo akili ikanifunguka sasa, sibeti pesa ambayo najua ikiliwa ntaumia
 
Rehab ya nini sasa wakati betting ndio kiwanda pekee cha ajira kilichobaki nchi hii? Serikali yenyewe inajua tax revenue inayotoka kwenye kamari.

Halafu umeandika kwa uchungu sana mkuu... kwani umepoteza kiasi gani? Pole sana, lakini investment ina siri kubwa, usikate tamaa mapema hivi, cheza tena!
 
Hata usipohifadhi pesa kwenye simu ikiwa unashida tu ujue utafanya njia yeyote ile ili uweze kubet
Mtu anabeti kwajili ya kupata hela ya vocha tu hawezi kuwa mraibu akipata 15k anajua habeti tena for weeks mpaka bando liishe.

Wanaobeti kwa lengo la kupata utajiri hao ndiyo changamoto.
 
Nilianza sports betting nikiwa na miaka 14... nilichojifunza:

1. Betting & Gambling ni biashara kubwa sana kwa wamiliki makampuni. The house always wins.

2. Ni mchezo wa bahati, marketing strategy kubwa ya makampuni ni kutumia washindi wachache waliopiga mamilioni kuvutia wateja wengi zaidi... kuna kampuni zinaenda mbali zaidi kwa kutangaza washindi feki.

3. Ni mchezo wa numbers, usipokaa chini kufikirisha ubongo wako utaona hesabu za betting zinalipa, ila ukifuatilia historia utakuta unapoteza pesa zaidi ya unayoshinda.

4. Hakuna utajiri kupitia betting: ndiyo, wapo watu waliofanikiwa kupitia betting lakini takwimu zinaonyesha 99% ya wachezaji wa sports betting wanafukuzia losing streak. Lakini ukizunguka dunia nzima kuna 51% za kuwa tajiri kupitia biashara, na 1% kupitia betting/gambling.

5. Betting inadhoofisha akili, na kudumaza uwezo wa kufikiri. Unapo-bet akili yako inawaza zaidi mikeka na matokeo, na yale matumaini unayopata jinsi mkeka unavyotembea yanakupa dopamine rush ili uamini betting ndiyo itakutoa kimaisha, kitu ambacho kinaweza kuja kuishia vibaya kwa kusababisha msongo wa mawazo, kukosa njia nyingine halali za kujiingizia kipato na kupelekea wizi na vitendo vingine vya kihalifu.

6. Sports betting ni comfort zone na siku zote "comfort zone is where dreams go to die." Wakamaria wote wanachojaribu ni ku-play safe, jinsi opportunities zinavyokuwa limited kwenye maisha yako ndiyo nafasi ya wewe kuangukia kwenye addictions za betting, drugs zinavyoongezeka... vijana wengi wanakosa vision na kujua nini kinaweza kuwapa maisha wanayoyataka hivyo njia nyepesi ni kuweka mkeka na kusubiri Mbappe afunge, au Barcelona ishinde ndiyo ule.

7. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi. Wahenga hawakukosea, siyo kila kinachofanya kazi kwa mwingine kwako kitafanya kazi. Kuna watu wanapiga mamilioni kila siku kwenye betting, na kuna watu betting imewapa umasikini, takwimu za betting zipo wazi: wamiliki na washindi ni 1% wakati wanaoliwa ni 99% hakuna uwiano kabisa.

8. Betting kama ilivyo sarafu, ina pande mbili... lakini waraibu wa kamari wanaangalia upande mmoja tu wa sarafu kwa kuamini huenda kesho itakuwa siku yangu.

9. Capitalism na betting ni watoto wa baba na mama mmoja. System hizi zote zinatengeneza pyramid scheme: mgawanyo wa utajiri unapungua jinsi unayoshuka chini. Ubepari na kamari vyote vinategemea masikini ili ku-survive. Masikini wote wakiacha ku-bet ambao ndiyo wanatengeneza 99% ya idadi kwenye mfumo makampuni yote yatajifia.

10. Delayed gratification ni bora zaidi kuliko instant gratification. Mifano ipo mingi ya watu waliofanikiwa kwa kufanya kazi, biashara n.k. vitu ambavyo vina matokeo ya taratibu sana kulinganisha na picha nzuri inayotengenezwa kuwa betting ni njia rahisi ya kujipatia mamilioni.

Mwisho wa siku kila mtu mwenye akili timamu lazima ajitathmini kujua nini kinamrudisha nyuma au kumzuia kupiga hatua kwenye maisha yake... uzuri wa maisha mifano ipo: kuna wanaofanikiwa na kufeli kwenye kila sekta unayoijua wewe... wapo waliofanika kwenye biashara, pia wapo waliofeli, wapo walifanikiwa kwenye betting, pia wapo wengi waliopigwa wakachakaa kwenye betting. Cha muhimu kwenye maisha ni kujua kitu gani kinafanya kazi kwako: hatuwezi wote kuwa, wafanya-biashara, madaktari, au walimu... muhimu ni kujua wapi una-fit kwenye jamii na wapi unakuwa bora zaidi kwenye maisha yako. Kwangu sports betting in kitu ambacho hakikufanya kazi lakini kwa wachache kimewabadilishia maisha.

Baada ya miaka 12 ya kamari, ni mwaka 1 sasa tangu niachane kabisa na sports betting. Na sasa naachana kabisa na kufuatilia sports.

"Give them bread and circuses and they will never revolt.” – Juvenal
 
Back
Top Bottom