Janga la Betting kwa Watanzania tujiandae na rehab center

Janga la Betting kwa Watanzania tujiandae na rehab center

Nilianza sports betting nikiwa na miaka 14... nilichojifunza:

1. Betting & Gambling ni biashara kubwa sana kwa wamiliki makampuni. The house always wins.

2. Ni mchezo wa bahati, marketing strategy kubwa ya makampuni ni kutumia washindi wachache waliopiga mamilioni kuvutia wateja wengi zaidi... kuna kampuni zinaenda mbali zaidi kwa kutangaza washindi feki.

3. Ni mchezo wa numbers, usipokaa chini kufikirisha ubongo wako utaona hesabu za betting zinalipa, ila ukifuatilia historia utakuta unapoteza pesa zaidi ya unayoshinda.

4. Hakuna utajiri kupitia betting: ndiyo, wapo watu waliofanikiwa kupitia betting lakini takwimu zinaonyesha 99% ya wachezaji wa sports betting wanafukuzia losing streak. Lakini ukizunguka dunia nzima kuna 51% za kuwa tajiri kupitia biashara, na 1% kupitia betting/gambling.

5. Betting inadhoofisha akili, na kudumaza uwezo wa kufikiri. Unapo-bet akili yako inawaza zaidi mikeka na matokeo, na yale matumaini unayopata jinsi mkeka unavyotembea yanakupa dopamine rush ili uamini betting ndiyo itakutoa kimaisha, kitu ambacho kinaweza kuja kuishia vibaya kwa kusababisha msongo wa mawazo, kukosa njia nyingine halali za kujiingizia kipato na kupelekea wizi na vitendo vingine vya kihalifu.

6. Sports betting ni comfort zone na siku zote "comfort zone is where dreams go to die." Wakamaria wote wanachojaribu ni ku-play safe, jinsi opportunities zinavyokuwa limited kwenye maisha yako ndiyo nafasi ya wewe kuangukia kwenye addictions za betting, drugs zinavyoongezeka... vijana wengi wanakosa vision na kujua nini kinaweza kuwapa maisha wanayoyataka hivyo njia nyepesi ni kuweka mkeka na kusubiri Mbappe afunge, au Barcelona ishinde ndiyo ule.

7. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi. Wahenga hawakukosea, siyo kila kinachofanya kazi kwa mwingine kwako kitafanya kazi. Kuna watu wanapiga mamilioni kila siku kwenye betting, na kuna watu betting imewapa umasikini, takwimu za betting zipo wazi: wamiliki na washindi ni 1% wakati wanaoliwa ni 99% hakuna uwiano kabisa.

8. Betting kama ilivyo sarafu, ina pande mbili... lakini waraibu wa kamari wanaangalia upande mmoja tu wa sarafu kwa kuamini huenda kesho itakuwa siku yangu.

9. Capitalism na betting ni watoto wa baba na mama mmoja. System hizi zote zinatengeneza pyramid scheme: mgawanyo wa utajiri unapungua jinsi unayoshuka chini. Ubepari na kamari vyote vinategemea masikini ili ku-survive. Masikini wote wakiacha ku-bet ambao ndiyo wanatengeneza 99% ya idadi kwenye mfumo makampuni yote yatajifia.

10. Delayed gratification ni bora zaidi kuliko instant gratification. Mifano ipo mingi ya watu waliofanikiwa kwa kufanya kazi, biashara n.k. vitu ambavyo vina matokeo ya taratibu sana kulinganisha na picha nzuri inayotengenezwa kuwa betting ni njia rahisi ya kujipatia mamilioni.

Mwisho wa siku kila mtu mwenye akili timamu lazima ajitathmini kujua nini kinamrudisha nyuma au kumzuia kupiga hatua kwenye maisha yake... uzuri wa maisha mifano ipo: kuna wanaofanikiwa na kufeli kwenye kila sekta unayoijua wewe... wapo waliofanika kwenye biashara, pia wapo waliofeli, wapo walifanikiwa kwenye betting, pia wapo wengi waliopigwa wakachakaa kwenye betting. Cha muhimu kwenye maisha ni kujua kitu gani kinafanya kazi kwako: hatuwezi wote kuwa, wafanya-biashara, madaktari, au walimu... muhimu ni kujua wapi una-fit kwenye jamii na waoi ni bora. Kwangu sports betting in kitu ambacho hakikufanya kazi lakini kwa wachache kimewabadilishia maisha.

Baada ya miaka 12 ya kamari, ni mwaka 1 sasa tangu niachane kabisa na sports betting. Na sasa naachana kabisa na kufuatilia sports.

"Give them bread and circuses and they will never revolt.” – Juvenal
Fafanua hapo namba 2. Kampuni gani imemtangaza mshindi feki?
 
Bro serious issue betting haina uzoefu nimeandika nikiwa najua madhara yake kwasababu nimebetting karibia michezo yote kampuni zote premier,pm,meridian ,betika,betpawa
kuna Uzi wa hivi majuzi mtu ametoa ushuhuda wa kuliwa milioni 25 jumla kwenye betting. Alieleza kwa machungu sana
 
Upo upande upi?? Kwamba betting sio janga?
Nikijizungumzia mimi, kwangu sio janga sababu imebadilisha maisha yangu kwa ujumla. Niliwahi kupiga kiasi kikubwa sana cha pesa kipindi nikiwa sina kazi na Ndio sababu ya kujiita Jobless Billionaire. Nimeweza kufanya uwekezaji na maisha yapo stable.

Hata hivyo, kwangu sio janga sababu sipo addicted. Nafanya pale ninapoamua tu na ninacheza kile ambacho hakiaffect kwa namna yoyote nyanja yangu yoyote ya kimaisha
 
Na ujinga wa baadhi ya wanaobet wanaamini ipo siku "watamlaza kanji na viatu"
Bila kujua determination ya kumla muhindi mtu anazidi kuwa addicted+kupoteza zaidi

Kutajirika kupitia betting ni ndoto ambayo wengi wanatakiwa kuamka kabla hawajajikojolea, hakunaga hela rahisi
Betting ni mchezo wa kujifurahisha, ukiufanya kama kitega uchumi lazima ukufokonyoe 🔞
 
Naunga mkono.
Kuna mwaka jamaa nilimfululiza kumpiga mpk ikafika 4M within a two weeks , wee jamaa alianza kurudisha pesa yake kama masikhara, na betting ukiwa na hela basi hata stake zinabadilika.
Mimi kuacha betting siwezi kwaiyo nilichoamua ni kulower stakes halafu odds mlima just for fun. Nikiweka 10k SportyBet nabetia mwezi mzima.

Hii ni baada ya siku kanji kuondoka na milioni moja yangu kimasikhara miaka mitatu nyuma
 
Betting ni mchezo wa kujifurahisha, ukiufanya kama kitega uchumi lazima ukufokonyoe 🔞
Ingekuwa inaleta tafsiri iyo kwa haraka kwa kila mtu basi pasingekuwa na haya makampuni haya makampuni yametengeneza mfumo ambao unabet kidogo ila ukiingia kwemye mfumo wake katika kumi basi saba wanakuwa depends wa kubetting ndio inatengeza addiction inabidili mtazamo na malengo
 
Nikijizungumzia mimi, kwangu sio janga sababu imebadilisha maisha yangu kwa ujumla. Niliwahi kupiga kiasi kikubwa sana cha pesa kipindi nikiwa sina kazi na Ndio sababu ya kujiita Jobless Billionaire. Nimeweza kufanya uwekezaji na maisha yapo stable.

Hata hivyo, kwangu sio janga sababu sipo addicted. Nafanya pale ninapoamua tu na ninacheza kile ambacho hakiaffect kwa namna yoyote nyanja yangu yoyote ya kimaisha
Shukuru Mungu umenusurika
 
Mimi kuacha betting siwezi kwaiyo nilichoamua ni kulower stakes halafu odds mlima just for fun. Nikiweka 10k SportyBet nabetia mwezi mzima.

Hii ni baada ya siku kanji kuondoka na milioni moja yangu kimasikhara miaka mitatu nyuma
Uliweza kunusurika ila umechase hiyo million basi hali ingekuwa tofauti
 
Back
Top Bottom