Janga la Betting kwa Watanzania tujiandae na rehab center

Fafanua hapo namba 2. Kampuni gani imemtangaza mshindi feki?
 
Bro serious issue betting haina uzoefu nimeandika nikiwa najua madhara yake kwasababu nimebetting karibia michezo yote kampuni zote premier,pm,meridian ,betika,betpawa
kuna Uzi wa hivi majuzi mtu ametoa ushuhuda wa kuliwa milioni 25 jumla kwenye betting. Alieleza kwa machungu sana
 
Upo upande upi?? Kwamba betting sio janga?
Nikijizungumzia mimi, kwangu sio janga sababu imebadilisha maisha yangu kwa ujumla. Niliwahi kupiga kiasi kikubwa sana cha pesa kipindi nikiwa sina kazi na Ndio sababu ya kujiita Jobless Billionaire. Nimeweza kufanya uwekezaji na maisha yapo stable.

Hata hivyo, kwangu sio janga sababu sipo addicted. Nafanya pale ninapoamua tu na ninacheza kile ambacho hakiaffect kwa namna yoyote nyanja yangu yoyote ya kimaisha
 
Betting ni mchezo wa kujifurahisha, ukiufanya kama kitega uchumi lazima ukufokonyoe 🔞
 
Naunga mkono.
Kuna mwaka jamaa nilimfululiza kumpiga mpk ikafika 4M within a two weeks , wee jamaa alianza kurudisha pesa yake kama masikhara, na betting ukiwa na hela basi hata stake zinabadilika.
Mimi kuacha betting siwezi kwaiyo nilichoamua ni kulower stakes halafu odds mlima just for fun. Nikiweka 10k SportyBet nabetia mwezi mzima.

Hii ni baada ya siku kanji kuondoka na milioni moja yangu kimasikhara miaka mitatu nyuma
 
Betting ni mchezo wa kujifurahisha, ukiufanya kama kitega uchumi lazima ukufokonyoe 🔞
Ingekuwa inaleta tafsiri iyo kwa haraka kwa kila mtu basi pasingekuwa na haya makampuni haya makampuni yametengeneza mfumo ambao unabet kidogo ila ukiingia kwemye mfumo wake katika kumi basi saba wanakuwa depends wa kubetting ndio inatengeza addiction inabidili mtazamo na malengo
 
Shukuru Mungu umenusurika
 
Mimi kuacha betting siwezi kwaiyo nilichoamua ni kulower stakes halafu odds mlima just for fun. Nikiweka 10k SportyBet nabetia mwezi mzima.

Hii ni baada ya siku kanji kuondoka na milioni moja yangu kimasikhara miaka mitatu nyuma
Uliweza kunusurika ila umechase hiyo million basi hali ingekuwa tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…