Janga la Corona : CAF yaifuta Mechi ya Namungo huko Angola

Fuata sheria bila shuruti hutaki utalazimishwa, umeshaambiwa wasikilize Who wao ndiyo wataalamu ukileta ubishi utaishia kwenye makambi ya Jeshi full stop.
 
Serikali hairuhusiwi kujiingiza kwenye michezo kwa kuwapangia vilabu kosa hilo pia
Hivi umeelewa hoja yangu, wizara ya afya ndio imezuia timu kuingia kwasababu za kiafya sasa hapo serikali imeingilia vipi michezo? Wao wameipima timu corona kama wanavyopima mtu yeyote anaeingia nchini kwao
 
Ni mamlaki ipi hiyo ya Angola imetoa taarifa tofauti na ya Namungo, mnaleta siasa zenu za kishamba huku, rudini Jukwaa la siasa nyumbxxxxx nyie hamjui mpira wala siasa za mpira.
Hawa ni nyumbu tena wa serengeti,
Kazi kubwa waliyonayo ni kuiombea nchi mabaya.
 
Mechi ya Chelsea UCL inahamishiwa Uturuki kwa sababu Spain hawaruhusu Muingereza yeyote kuingia Spain.
 
Hivi ni nini kinachowafanya muwe na akili za aina hii? Unajua kuna baadhi ya nchi Ulaya Waingereza hawaruhusiwi kuingia? Je jumuia ya kimataifa inavhukuliaje msimamo wa Tanzania dhidi ya corona?
 
Ujinga wao ni faida kwetu, Namungo ataingia hatua ya makundi bila shaka. Taifa linaenda kuwa na wawakilishi wawili kwenye hatua ya makundi CL na CC kwa mara ya kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio taarifa ya sasa kutoka CAF kutokana na sakata la wachezaji watatu na kiongozi mmoja wa Namungo kukutwa na corona

Tusubiri taarifa zaidi kutoka CAF ambalo ndio shirikisho linalosimamia soka barani Africa

View attachment 1701605

Hii ndio taarifa ya sasa kutoka CAF kutokana na sakata la wachezaji watatu na kiongozi mmoja wa Namungo kukutwa na corona

Tusubiri taarifa zaidi kutoka CAF ambalo ndio shirikisho linalosimamia soka barani Africa

View attachment 1701605
Suala ni kwamba je wachezaji wa namungo walipimwa kabla ya kuondoka Tanzania. Mana kuna Sheria ya angola hii hapa ''Persons entering the country require a negative polymerase chain reaction (PCR) COVID-19 test taken no more than 72 hours before arrival''
Isije kuwa walisafiri tu kwa mazoea kwamba tutaenda kupima uko uko.
Ila kama walipima na majibu yao wanayo basi timu ya angola imekula kwao ila kama waliondoka kimazoea basi iyo ndio nguvu waliotumia waangola.
 
Hapakuwa na haja ya kutaka kuweka karantin timu nzima mbona Qatar muller alionekana na maambukizi baada ya match na al ahly na Bayern yote haikutengwa isipokuwa yeye?kimsingi hapa kuna kitu hakiko sawa
 
Kwanini wapewe pointi wakati serikali ndio imewazuia namungo na si timu iliyopaswa kucheza na namungo?
Inapotokea mkanganyiko kama huo timu Mgeni huwa inapewa point dhidi ya timu mwenyeji hasa pale inapokuwa willing kuja na mwenyeji ndie hataki (hata kama ni serikali refer German kwenye uefa)
 
Yanga waliwahi kucheza pale wakawa wanapigwa na matofali uwanjani Angola ni nchi ya kipumbavu sana
 
Mimi sikati vipimo na wala sibishi vipimo, unakumbuka FC PLATINUM walivyokuja hapa bongo ni wachezaj wao wangapi walikutwa na COVID? JESHI ILIWASHIKILIA AU NINI KILIFANYIKA?
Kila nchi ina taratibu zake mkuu.. ni sawa na nyumba tu kila nyumba ina utaratibu wake, sio wewe ufike kwa mwenzako ulete utaratibu wako.. ndio hivo mkuu ile ni nchi yao na wana taratibu zao, kama platinum hawakufanywa chochote huo ni utaratibu wetu, tuwe wapole
 
Mechi ya Chelsea UCL inahamishiwa Uturuki kwa sababu Spain hawaruhusu Muingereza yeyote kuingia Spain.
Na waliofanya kazi ya kutafuta pa kwenda ni Spain wenyewe kama wasingefanya hivyo Chelsea angepewa point 3 na goli 3
 
Nitajie nchi ambazo jeshi inasimia kuhusu corona
 
Wakubali kukaa karantini hizo siku ili gemu ipigwe hakuna namna ukizingatia wapo kwenye ko stage na ratiba haiwasubiri, vinginevyo angola watapewa point za mezani. Aibu kwa nchi
Wewe si mfuatiliaji mzuri wa michezo tangu janga la covid liingie.. Muongozo upo kama idadi ya wachezaji waliopatikana na COVID ni ndogo 2,3 ama 4 wachezaji husika tu ndiyo wanazuiwa kucheza mechi... ndiyo maana unaona hata league kubwa zinaendelea kama kawaida licha ya baadhi ya wachezaji kuwa wanakutwa na maambukizi.. Pia CAF ndiye muamuzi wa mechi kuhairishwa ama la.. Kama mamlaka ya nchi iliingilia hili no wazi waangola watapokonywa ushingi na goli 3
 
Hivi umeelewa hoja yangu, wizara ya afya ndio imezuia timu kuingia kwasababu za kiafya sasa hapo serikali imeingilia vipi michezo? Wao wameipima timu corona kama wanavyopima mtu yeyote anaeingia nchini kwao

Jeshi ndio wizara ya afya? Kumbe kule angola jeshi ndio wizara ya afya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…