Janga la Corona limempaisha Rais Magufuli kisiasa

Janga la Corona limempaisha Rais Magufuli kisiasa

Tambukareli

Member
Joined
May 8, 2020
Posts
35
Reaction score
64
Namna ambavyo Rais magufuri amejipambanua kukabiliana na janga la corona ni dhahiri amekonga nyoyo za walio wengi na hii imepelekea kupata uungwaji mkono na maelfu ya watanzania wakiwemo wa vyama vya upinzani.

Kitendo cha Rais Magufuli kutokubaliana na agenda ya kujifungia (LOCK DOWN) ambayo ndio ilikuwa agenda kuu ya upinzani, wananchi wamekipokea kama maamuzi sahihi ya kuwavusha katika kipindi hiki cha janga la corona dhidi ya baa la njaa na matatizo mengine ya kiuchumi.

Leo Rais Magufuli ametoa tamko la kufungua vyuo na shule kwa wanafunzi wa form six hili pia wananchi wamelipokea kama uamuzi wa busara kwa sababu linasaidia kulinda ajira za walimu wa shule na vyuo binafsi ambao walikuwa wanaishi katika kipindi kigumu kutokana na kusitishiwa mishahara yao. Hali kadhalika uamuzi huu unasaidia kulinda usalama wa wanafunzi dhidi ya vishawishi mitaani na hatari ya mimba za utotoni.

Kwa namna Rais Magufuli amejitoa na hatua alizochukua kukabiliana na corona hakika amepata wafuasi wengi hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. kwahivyo vyama vya upinzani vijipange kisawa sawa kwa sababu uchaguzi ujao utakuwa ni mgumu kwa upande wao baada ya kupoteza wafuasi wake kutokana na agenda zilizokosa credibility katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona.

Sambamba na hatua nzuri anazochukua Rais Magufuli kupambana na corona ni vema sasa akaangalia areas of weakness ambazo bado zinahitaji utatuzi mathalani suala la ajira kwa vijana, azitatue ili kufikia October wananchi wawe na kazi moja pekee ya kuchukua na kuweka waaa.
 
Hilo janga limempaisha Rais "Magufuri" kisiasa kutoka hatua gani kwenda nyingine? Tayari Corona imeshageuka na kuwa siasa!

Kama Kiongozi Mkuu wa nchi, jukumu lake ni lipi sasa! Kupongezwa na kutukuzwa, au kuiongoza nchi kwa weredi na kwa kuifuata misingibya Katiba?
 
Unataka aongoze kwa weledi upi? Kama amekulinda Wewe hujafa na corona Unataka nini tena?

Nyie chadema ni giza totoro
Hilo janga limempaisha Rais "Magufuri" kisiasa kutoka hatua gani kwenda nyingine? Tayari Corona imeshageuka na kuwa siasa!

Kama Kiongozi Mkuu wa nchi, jukumu lake ni lipi sasa! Kupongezwa na kutukuzwa, au kuiongoza nchi kwa weredi na kwa kuifuata misingibya Katiba?
 
Hilo janga limempaisha Rais "Magufuri" kisiasa kutoka hatua gani kwenda nyingine? Tayari Corona imeshageuka na kuwa siasa!

Kama Kiongozi Mkuu wa nchi, jukumu lake ni lipi sasa! Kupongezwa na kutukuzwa, au kuiongoza nchi kwa weredi na kwa kuifuata misingibya Katiba?
Kwani kuna mwanasiasa aliye nyamaza kipindi hiki cha Corona?
 
JPM atabaki kuwa JPM mambo anayofanya wanaoweza kuyaona na kukiri ni wachache sana, kama wanaweza kusema ukweli ni Mwinyi, Mkapa pamoja na Kikwete maana wao walikuwepo pale. Wakisema bila kumung'unya ukweli ndio mtafahamu Hili ni jembe tena sio jembe tu bali la chuma cha pua. If you know what I mean.
 
Muulize Mbowe alikuwa na maana gani kuitisha yale matamko na muulize nini kimemtokea baada ya pale

Sent using Jamii Forums mobile app

Nyinyi watu wa Ccm acheni kuleta masihara dhidi ya hili janga la Corona! Lakini siwashangai maana hata kipindi kile cha kupatwa kwa jua, mlimpongeza pia Rais kwa kufanikisha tukio la kupatwa kwa jua nchini mwetu kiasi cha watalii wengi kumiminika kuja kulishuhudia hilo tukio.
 
Hilo janga limempaisha Rais "Magufuri" kisiasa kutoka hatua gani kwenda nyingine? Tayari Corona imeshageuka na kuwa siasa!

Kama Kiongozi Mkuu wa nchi, jukumu lake ni lipi sasa! Kupongezwa na kutukuzwa, au kuiongoza nchi kwa weredi na kwa kuifuata misingibya Katiba?
Kama kiongozi wa nchi jukumu lake kubwa ni kutulinda ndio maana up to this moment rate ya maambukizi imepungua na watu wanachapa kazi kama kawaida kama hiyo haitoshi mimi na wewe hapa tulipo tuna chati, hii inaonyesha ni kwa kiasi gani amepambana vya kutosha kuhakikisha tunakuwa salama dhidi ya ugonjwa wa covid 19
 
Hakika janga la corona limewazamisha sana wapinzani na hoja yao ya kulazimisha lockdown, kulazimisha habari za uongo kwamba hali ni mbaya saana wakati watanzania wao wanadunda na maisha kama kawa.

Lockdown waliyoishabibia sana;

1. Imekosa kabisa uhalisia wa utekelezaji kwa nchi kama zetu. Madhara ya kukataa lockdown yameeleweka na yanaimbwa na wananchi wa kawaida kabisa.

2. Hata nchi za Ulaya/US zimekuja kuacha a na lockdown.

3. Faida zilizokuwa zinapigiwa upatu zimekuja kuonekana si halisia. Badala yake kuna consensus ya kwamba lockdown ina madhara na haifai kufuatwa

4. Mifano ya wananchi kuigomea lockdown iko wazi nchi nyingi wananchi wa kawaida wanaoandamana ikiwemo majirani zetu Kenya, Zambia, Afrika ya kusini.

Hata hivyo nawasifu viongozi wa upinzani kwa mshipa wa ung'ang'anizi! Wamejua lockdown haikubaliki na watanzania, haina faida za kiafya kama wanavyosema, kuna madhara makubwa zaidi ya lockdown, siyo mbinu inayopendwa tena! Lakini bado wameshindwa kukiri!
 
Unalindaje RAIA kwa kutotoa data husika kuhusu hali ya Ugonjwa Nchini? Wiki ya tatu sasa hatujui kuna wagonjwa wangapi Nchini na vifo vingapi vya huu ugonjwa na sasa tunaona juhudi za KUTUZUGA Watanzania hata kuvaa BARAKOA hawavai tena. Mnadhani Ramaphosa ni MPUMBAVU kwa kuvaa Barakoa hadharani?

Kama kiongozi wa nchi jukumu lake kubwa ni kutulinda ndio maana up to this moment rate ya maambukizi imepungua na watu wanachapa kazi kama kawaida kama hiyo haitoshi mimi na wewe hapa tulipo tuna chati, hii inaonyesha ni kwa kiasi gani amepambana vya kutosha kuhakikisha tunakuwa salama dhidi ya ugonjwa wa covid 19
 
Naunga mkono hoja, tena jinsi rais Magufuli anavyokubalika, ingekuwa ni amri yangu, ningeamuru tufanye uchaguzi wa madiwani na wabunge tuu, kwenye urais, Rais Magufuli aendelee tuu, lakini kwa vile uchaguzi ni takwa la kikatiba, then, tuendelee tuu na hili miezi, la maandalizi ya uchaguzi Mkuu hata kama kwa upande wa urais litakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini Rais ni Magufuli!, na kwasababu Watanzania tunapenda saana maigizo

Swali hili
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? - JamiiForums

Bado liko valid
P
 
Wabunge WATATU wa ccm na wakuu mbali mbali ndani ya Serikali na ccm wamefariki kwa COVID lakini hili haliwekwi hadharani. Tuliambiwa kuna Mbunge ana Corona lakini hakutajwa. Kama kweli corona imepungua Nchini INAKUWAJE wanazificha data husika za kuthibitisha wanachokiongea? Unaongea kwamba ugonjwa umepungua kwa maneno matupu lakini huna data, hiyo ni hatari sana kwa Watanzania kwani wengi wataanza kudharau taratibu mbali za kujikinga na hivyo maambukizi kuendelea kote Nchini.
 
mbona mnahangaika kama aliebanwa na tumbo la kuhara? haya basi limempaisha, tukusaidie je?
 
Bila ya kuwepo TAKWIMU za KUTHIBITISHA kwamba ni kweli Ugonjwa umepungua muendelee kufuata masharti yote ya corona au mtabaki na majuto mjukuu. Na ukishakufa ndiyo umekufa hakuna kukata RUFAA kuhusu kifo chako au cha ndugu.
 
All in all usiri nao umesaidia sana jamaa kupaa ila mambo yangewekwa hadharani hasa zile za kuzika usiku sidhani kama angepaa, wewe hufikirii hadi watu waliwaza sabasaba iwe hospitali ya kovidi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom