Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Mkuu mimi ninavyojua ni kua awamu hii inapesa nyingi tu ..So serikali ikiweka lock down moja kwa moja utaweza ata kulipa watu na kutoa msaada wa pesa na chakula
Mkuu;
Nashukuru kwa kutoa maoni yako!
 
Mkuu;
Wewe unadhani angefanyaje ili kukabiliana na hili janga la COVID-19?
Angechukua harsha and radicala actions kama Korea
1.Tangaza hali ya dharura nchini (emergency)
2. Funga mipaka kwa muda hadi hali itakapoimarika, ahirisha shughuli za kitalii n.k.
3. Wazawa wanaorudi nyumbani wawe chini ya karantini, serikali igharamie ili kuondoa ukwepaji
4. Funga shughuli za mikusanyiko makanisani, misikitini, vikao vya harusi, michezo n.k.
5. Funga vyuo, shule , makongamano, warsha n.k
6. Hakuna Hoteli za kukusanya watu, ziruhusiwe kwa ''take away'
7. Weka social distancing, na zuia shughuli zisizo za lazima kwa wiki kadhaa.
8.Hakikisha kuna maeneo maalumu pindi hospitali maalumu zitakazidiwa
9. Hakikisha vifaa kwa wahudumu wa afya ili kuwakinga na janga
10. Tayarisha Watumishi wa afya wastaafu kama ''reserve'' ikibidi warudi kazini
11. Unda kamati maalumu itakayotoa taarifa kila siku katika vyombo vya habari kuhusu hali ilivyo nchini na duniani
 
Kuna mtu alisema, think globally but act locally!

Ndicho serikali ilichokifanya!
 
Wakati huo wewe na jamii yako mtakuwa mumeketi pembeni mkiendelea kuwacheka kwa mambo waliyotenda.

Hivi sasa kwani wamarekani wanamcheka Trump na ujinga wake wa kusema corona itapotea bila dawa!!! Yeye mwenyewe amegundua kuwa yale aliyoyasema ugonjwa ulipoingia marekani hayakuwa sahihi na hayakuwa ya busara , amekunja mkia wake na wenzie wenye busara wanawahudumia wananchi!!! Hapa muda si mrefu Viongozi wetu wataumbuka kwa kutokuwa makini kwao covid-19 itakapo shika kasi!
 
Tokea corona iingie nchi za africa ni muda gani sasa umepita?
 
Mkuu;
Maoni yako yamenifanya nikacheka!

Umeandika kama utani lakini kuna mabo ya msingi sana umeyaweka!
 
Tokea corona iingie nchi za africa ni muda gani sasa umepita?

Wataalam wanasema kutokana na uzoefu wa nchi nyingine, baada ya wiki tatu zijazo Afrika ndio itaanza kuona makali ya covid-19!
 
Wataalam wanasema kutokana na uzoefu wa nchi nyingine, baada ya wiki tatu zijazo Afrika ndio itaanza kuona makali ya covid-19!
Ikiwa na maana kwamba kwa sasa hivyo virusi havina makali hadi huo muda waliyosema au wana maana ipi hasa?
 
Ikiwa na maana kwamba kwa sasa hivyo virusi havina makali hadi huo muda waliyosema au wana maana ipi hasa?

Ndio maana yake; baada ya incubation period yake ndio makali yake yanaonekana zaidi!!
 
Wataalam wanasema kutokana na uzoefu wa nchi nyingine, baada ya wiki tatu zijazo Afrika ndio itaanza kuona makali ya covid-19!
Yes, watu wote waliotambuliwa kuwa na COVID ni kutoka nje. Hata hivyo, kuna mtu mmoja amepata akiwa ndani ya nchi. Hiyo inatitwa community spread. Kwa maneno mengine incubation period inaendelea na itakapoanza kujitokeza ni balaa inafuata. Nigeria ilikuwa hivi hivi.

US ilianza na mtu kutoka nje Trump akaita Hoax, sasa US inaongoza.
Italy ililetwa na mtu mmoja, ilipoanza community transmission hali ndiyo hiyo.

Watu wasijipe matumaini ya uongo, hili ni 'bomu' tu linasubiri muda.

Hatujui kama tuna respirators za kutosha, kuna wataalam wa kutosha au tuite ''reserve''

Tupo hapa ipo siku utasikia, Mbeya hakuna vifaa, Mwanza hakuna abcd.

Kila mtu anahofia moto ukipamba Afrika nini kitatokea.
Bado hatuna habari tunatumaini maombi bila kujishughulisha
 
Kila mtu anahofia moto ukipamba Afrika nini kitatokea.
Bado hatuna habari tunatumaini maombi bila kujishughulisha

Hii ni habari mbaya sana kwani muda huu viongozi wetu are in denial, hawaamini kuwa hili ni janga. Wanafanya mzaha na kuendelea kunywa tangawizi vijiweni!!
 
Ndio maana yake; baada ya incubation period yake ndio makali yake yanaonekana zaidi!!
Incubation period ni muda wa wadudu kuzaliana na hadi dalili zitakapojitokeza ''symptom''
Haina maana kila mtu ataonyesha symptoms, kuna watu watahimili na hao watakuwa asymptomatic, hawana dalili.

Asymptomatic ni carrier wazuri wa virus na watakpovikisha kwa vlnerable group mathalani watu wenye kinga dhaifu 'immuno compromised'' kama wagonjwa cancer, HIV na maradhi kama Asthama, Diabetic, au moyo hapo ndipo utaona wagonjwa wenye dalili kwa wingi. Katika kundi hilo hadi sasa Wazee ndio wanaathirika sana.

Tofauti na mafua ya kawaida, corona wanasababisha maradhi katika mfumo wa chini wa hewa ''lower respiratory'', kwahiyo si lazima mtu awe na mafua makali, bali kikohozi na homa hujitokeza.

Watu wengi wanafanya mzaha wakiita haya kama mafua ya kawaida. Ukweli ni kuwa si ya kawaida kwasababu hawa virus ni wapya ''novel'' na miili haina kinga na wala haijakutana nao. Hapo ndipo tatizo lilipo.

Kuna nafasi ya joto katika kupunguza kasi ya maambukizi, tunachosahau Tanzania ni kuwa nasi pia tuna maeneo yenye baridi na sasa tunaelekea majira ya kipupwe ''winter'' hivyo kwetu ni tatizo linalosubiri muda

Kwanini kuna vifo sana, ni kwasababu hakuna dawa ya kutibu virus.
Kinachofanyika ni kutoa muda wa mwili kutengeneza kinga na kuzuia madhara ya vitu kama homa kali.

Katika kufanya hivyo kunahitajika respirator hasa kwa watu waliozidiwa.
Swali la kujiuliza , je tuna respirator za kutosha nchini? Kumbuka CT-Scan si zaidi ya 20 nchini kama nipo sahihi.

Kinachotisha zaidi ni kwamba, bila vifaa vya kujikinga kama mask, gown n.k.
Wataalam wa afya watakuwa katika wakati mgumu sana.

Katika nchi za magharibi tayari madhara yanaonekana.
Sasa sijui kama huko Wilayani kuna kinga kwa madaktari na manesi.
Tatizo hili litakuwa kubwa pale watumishi wa afya watakapoamua kujinusuru.

Msifanye mzaha kama wa mleta mada! hili ni janga la dunia na Tanzania hakuna immunity, tupo vulnerable kama taifa jingine lolote, tofauti ni muda tu.
 
Kuna mtu alisema, think globally but act locally!

Ndicho serikali ilichokifanya!
Ndiyo maana sitaacha kukupa shule au kukuumbua kwasababu umedhamiria kwa dhati kabisa kupotosha umma.

Think globally haina nafasi katika baadhi ya mambo. WHO ndiyo inayotoa miongozo ya tatizo duniani kote.
Huwezi kutengeneza mask za plastic bag ukasema una think locally. Mask lazima zikidhi international standards au ''think globally''. Quarantine ni ''think globally'' huwezi ku isolate watu uksema ni suala locally, hiko ni muongozo wa WHO na isolation ina taratibu zake

PPE ni globally si kwamba Daktari au Nurse wa Tanzania atavaa kanga au shuka kwasababu tuna think locally.

Respirator ni 'think globally'' haina maana Daktari wa Tanzani ataweka pipe ya mpira wa maji kooni eti ana think locally.

Hatuwezi kufanya mambo locally kwa tatizo ambalo ni global. Leo China inasaidia nchi za magharibi kwasababu global problem needs global solution.

Usiwadanganye watu tuna tatizo na muda ukifika tutakimbiana, trust me! ninyi viongozi mtakuwa katika ma VX sisi tukipumuliana katika dala dala.

Usipotoshe watu kama huna hoja tunga nyimbo za kusifia weee hatutakugusa, lakini kwa suala hatari kama hili, wewe ni mumiani.
 
Ukiacha hiyo corona ni kwanini mafua huwa ni ugonjwa hatari kwa hao wenzetu tofauti na sie?
 
Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli
Ni kiongozi ambaye anapaswa kuigwa na kuendelea kupewa ushirikiano angali hai...
Huyu ni kiongozi ambaye ni zaidi ya tunuku kutoka kwa Mungu,mbali na mambo anayoyafanya bali ni mtu anayeweza kufikilia maisha ya mtu wa chini kabisa na akayaishi bila kujali nafasi yake aliyonayo "HUU NDIYO USHUJAA WA UONGOZI"Huyu ni kiongozi wa kweli anayejali watanzania wa ngazi zote bila kujali jambo lolote,kwa kipindi hiki cha covid 19 angekuwa kiongozi mwingine,asingethubutu kushare kikombe cha kahawa kwa muuza kahawa,angesema anaweza kuambukizwa corona,lakini amethubutu kunywa na kurudia mara mbili zaidi.....
Naomba mungu ndoto zangu za uongozi wa taifa hili pindi zitakapokamilika,nije kuwa na mfano wa rais Magufuli..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: UCD
Arudi Dar akashee kikombe cha kahawa...katoka nduki na harudi mpaka corona iishe.
 
Reactions: UCD
Nashukuru Mkuu kwa kunipa hongera!
 
Tanzania sample 26 cases 13
Uganda sample 267 , cases 23
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…