Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Mimi nafikiri mpango wa Raisi Magufuli unafanana na Darwin Theory survival for the fittest au Law of the jungle
Kama yakiokea maambukizi mengi watu watakaoathirika ni watu ambao immunity yaani kinga ya mwli imepungua kama wazee kuanzia miaka 70 na kuendelea.
Au Watu wenye maradhi kama kifua kikuu,HIV,Canser,Kisukali,Pumu n.k
au watoto wachanga ambao kinga yake bado ni ndogo sana.
Wazee over 70 years ni wengi,wagonjwa wa maambukizi yanayopunguza kinga mwilini wako wengi,na watoto wachanga kabisa wako wengi.
Kwa hali kama hii tumuombe Mungu maabukizi yasienee ni moto.
 
Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanasiasa kutaka Rais Magufuli na serikali yake wafunge mipaka ya nchi na kutoa tamko la kuwataka/kuwalazimisha wananchi wabakie majumbani mwao ili ‘’ kupambana’’ na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 yasisambae nchini.

Mashinikizo yanayotolewa kwa Rais Magufuli unaweza kuyaona niya msingi kama utadhani mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii ni sawa na mazingira ya ''Nchi za Magharibi'' ambazo zinatumia mbinu hii katika kukabiliana na janga la COVID-19.

Nakumbukwa kwenye sherehe ya wafanyakazi mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''Mtu yeyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, na yeye anajua una akili na anajua kuwa niya kipumbavu usipoyakataa anakudharau''.

Ni ukweli kuwa, Mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini yako tofauti sana na mazingira ya nchi za Magharibi na kwa msingi huu, haiwezekani mbinu za kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 yakafanana na nchi hizo.

Mwanasiasa wa Marekani aitwaye Donald Rumsfeld aliwahi kusema, ‘’You go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time.”

Kwa kiswahili ambacho sio sanifu, Donald Ramsfeld alisema, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’.

Kwa mantiki hii, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi la kiuchumi na kijamii alilonalo na sio ambalo baadhi ya wanasiasa wanataka liwepo wakati halipo.

Kwenye suala la kiuchumi, nchi za Magharibi zimeweza kufanikiwa kufunga mipaka na kuwalazimisha wananchi wake wabakie majumbani mwao kwa masaa 24 bila kutoka nje kwa sababu mazingira ya kiuchumi yanaruhusu kufanya hivyo.

Kwa sasa wananchi wote wa nchi hizo pamoja na kwamba hawafanyi kazi lakini serikali imeamua kuwalipa mishahara na pesa za kujikimu na maisha wananchi wake wote mpaka pale watakapoanza kufanya kazi tena. Hata malipo rehani (mortgage) kwa sasa yamebebwa na serikali.

Kwa upande wa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ kama Tanzania, serikali haiwezi kubeba jukumu la kiuchumi kama zilivyofanya nchi za Magharibi kwa sababu haina uwezo huo na kama serikali italazimisha wananchi wake wabakie majumbani basi tutegemee machafuko nchini au familia nyingi kufa kwa njaa hasa zile zinazoishi kwenye maeneo ambayo bila kutoka ‘’nje ya nyumba’’ familia haiwezi kupata chakula cha siku.

Kwa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwamo Tanzania, binadamu anaishi kwa jasho/nguvu zake lakini kwa ‘’nchi za Magharibi’’, binadamu anaweza akaishi bila jasho/nguvu zake bali kwa msaada kutoka serikalini

Tanzania vile vile ni ''lango kuu'' na mkondo wa usafirishaji katika nchi karibu nane ambazo hazina bahari.

Haishangazi kwa sasa tumeanza kuona wananchi wakipigwa risasi katika nchi za Rwanda na Uganda kwa sababu wamekataa kutii amri ya kubakia majumbani mwao kutokana na ukweli kuwa kubaki ndani pia ni kukaribisha kifo kwa njaa. Ni bora watoke nje wakajaribu bahati ya kutafuta chakula kuliko kubaki majumbani mwao. Nadhani baada ya wiki moja hali itakuwa mbaya zaidi.

Huko Kenya, Rais Kenyatta amegundua makosa na kwa sasa amebadili msimamo wake ambapo badala ya amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao kwa saa 24 kwa sasa watafanya hivyo kuanzia majira ya saa 11 za jioni hadi saa 11 alfajiri. Hii mbinu ya Rais Kenyatta inashangaza kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi katika nchi zetu wanakusanyika zaidi mchana kuliko usiku!

Kwenye suala la kijamii, nchi za Magharibi zimefanikiwa kutokana na ukweli kuwa jamii zake zinaishi maisha ya ‘’kipweke’’. Ninaposema kipweke nina maana mazingira ya hali ya baridi na kazi yamewafanya wananchi wawe wanaishi maisha ya kujifungia ndani hata wakitoka kazini. Wenzetu hawana hii dhana ya ‘’kwenda kwenye kijiwe’’ kupiga stories au kwenda kwa ndugu au rafiki bila kutoa taarifa.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo mikusanyiko ya kijamii na kifamilia ni sehemu muhimu ya maisha, ni vigumu sana kwa serikali kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wengi kama itatoa amri ya kuwataka wananchi wasifanye hivyo na badala yake wabakie majumbani mwao kwa saa 24.

Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwemo Tanzania haiwezekani kuzitumia kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.

Kama alivyosema Donald Ramsfeld, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’. Kwenye janga hili la COVID-19, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi alilonalo!
Utakuja jutia na ulicho andika , Sasa hivi South Africa iko kwenye lockdown, Sio kipindi cha siasa Sasa hivi inabidi ujifunze kwa Wenzio .Hiii hali sio nzuri kabisa .Nimejionea kwa macho yangu mwenyewe . Resource inahitajika kwenye kupambana na corona virus. Nigeria wametenga USD Mil 27 wakati Tanzania bado wako kimya itumesikia fungu la pesa za Mwenge limepelekwa kwenye kupambana na corona , Serikali tu Ndio wanajua ni sh ngapi, Baadhi za nchi za magharibi wanajilaumu kwanini hawakuchukua hatua mapema Kama nchi nyingine
 
Magu hakulaumiwa kwa hayo uliyosema bali kalaumiwa kwa mambo kama pale aliposema hawezi kuzuia watalii kuingia nchini! Uzuri ni kwamba, hao watalii wenyewe wana akili na wanafahamu risk iliyopo kwa wao kuendelea kusafiri, na kwahiyo wameamua kujizuia wenyewe huko huko kwao!

Na kwavile ndege nyingi zimesimamisha international flights, hiyo ndo nafuu yenyewe kwetu vinginevyo lau kama airlines na watalii wangekuwa na akili kama za JPM, balaa ambalo lingekuwa limeshatokea tungekuwa tunatafutana hivi sasa!

Zanzibar kwa mfano, wanapokea watalii wengi sana kutoka Italy! Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo Watalii wa Italy wangeendelea kuingia?!

Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo wananchi kwenye mataifa yaliyoathirika wangeendelea kumiminika kwa sababu tu Mpiga Ramli mmoja anaamini coronavirus haifui dafu mbele ya ibada?!

Lingine alilolaumiwa JPM ni kauli yake ya majuzi kwamba eti watu waendelee tu kumiminika kwenye nyumba za ibada na kwamba eti COVID-19 haiwezi kuishinda Damu ya Yesu!!

Ni mtu wa ajabu tu ndie anaweza kutetea ujinga kama huu kwa sababu hakuna janga hata moja lililowahi kuzimwa kwa watu kujazana makanisani na misikitini!

And FYI, zipo nchi nyingi tu ambazo zilidhani zingeendelea kuwa salama! Spain kwa mfano, daktari mmoja alifikia hadi kusema ni ngumu sana kwa Spain kupata maambukizo mengi kwa sababu tu walidhani kuto-share mpaka na Italy ingeweza kuwa salama kwao!

Leo hii, it's a matter of time kabla Spain hawajaifunika Italy!!

Hata Trump nae mwanzoni wala hakudhani ingekuwa serious issue kwa US! Leo hii US imeyapiku mataifa yote kwa idaidi ya maambukizi!!

So, endeleeni tu kutetea ujinga kwa sababu ndicho mlichoapa kukifanya!!
Na mambo yakibadilka,wataanza kulaumu wasaidizi wa JPM huku wakimtetea JPM kuwa alishauriwa vibaya.
 
Kimsingi mimi sio msemaji au muwakilishi wa yoyote hapa jukwaani, ila ninachojua ukija na maoni biased lazima nikupe ukweli wako.
Ndio nauliza mkuu umeacha upinzani? Maana humu ndio utaratibu wetu ukikosoa basi wewe ni mpinzani na ukipongeza au kuunga mkono basi ni ccm.
 
  • Thanks
Reactions: 30P
Mkuu, revisit your details. Kwa jinsi nilivyoiona hiyo barua ni kuwa Prof anajulisha watu wa taasisi yake kuwa kuna mtu A hatakuwa ofisini hivyo mtu B atakaimu nafasi yake ktk hiyo idara kipindi huyo mhusika hayupo. Simple like that.

Unless uwe haujui mambo ya office au hujawai kukaimisha au kukaimishwa.
Alafu bodi ndiyo itamteua huyu B..ebu kua utimamu mkuu
 
Baada ya wiki moja wakiwa kwenye amri ya kutotoka nje hali itakuwa mbaya zaidi kwa sababu hata kile kidogo walichonunua kwa pesa kidogo walizonazo kitaisha.

Kwa nchi zetu za Afrika unaweza kutoa amri hiyo ya kukaa ndani iwe kwa siku moja au mbili lakini siyo kwa zaidi ya wiki moja!
Mkuu mimi ninavyojua ni kua awamu hii inapesa nyingi tu ..So serikali ikiweka lock down moja kwa moja utaweza ata kulipa watu na kutoa msaada wa pesa na chakula
 
MsemajiUkweli ,

..Tz haina CAPACITY ya kuwapima, kuwahifadhi, na kuwatibu, wagonjwa wa Corona ikiwa ugonjwa huo utaingia hapa nchini.

..Kutegemea msaada wa serikali hii ni UENDAWAZIMU. Hivyo basi ni bora kumuomba MUNGU atuepushe kwasababu hatuna serikali ya kuitegemea.

..Uamuzi wa Raisi ulikuwa very simple. He does not have the options ambazo mataifa mengine yanayo. Uamuzi hapa ni KUSUBIRI tuone nini kitatokea. Kwa wale wenye imani wanatakiwa KUSALI.

..Hatuna vifaa, hatuna wataalamu, hatuna fedha. Lakini tunaweza KUSALI.

Hata huko unapoaminia wamekufa wengi tu pamoja na capacity yao lakini bado hawajaweza kuzuia mtu kufa, jambo hili si la kusemea uwezo wa nchi.
 
Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwemo Tanzania haiwezekani kuzitumia kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.
Umenena vyema.
Nikiwa mmoja ya watu walioshauri lockdown (sio total lockdown), nilisema iwe kwenye mipaka ya kuingia nchini, nyumba za ibada, na kuandaliwa taratibu ya mikusanyiko ya mazishi n.k.

Kiukweli kabisa hali zetu dunia ya tatu wengi hatuna akiba ya chakula wala ya fedha kukidhi mahitaji ya watu kujifungia ndani.

Nimeridhishwa sana na juhudi zilizo chukuliwa na serikali kwenye mipaka, usafiri wa umma(kuzuia mlundikano na kupuliza dawa) na mengineyo. Ingawa baadhi kama kudhibiti wanao ingia nchini kwa kuwaweka ktk uangalizi wakiwa wametengwa zimecheleweshwa kidogo. Better late than never.

Kilichobaki tuombe Mungu hali isiwe mbaya maana kwa uchumi wetu sijui tutapona vipi bila msaada wake. Ukikaa ndani unakufa njaa na ukitoka nje unaweza kuambukizwa na kufa kwa COVID-19.
Hii inaitwa kwa utani kule kwa wamakonde wanasema "Ukisimama nchale, ukikimbia nchale, ukikaa nchale, uchiteme wala uchimumunye".
Vijana wa mjini wanasema tumewekwa mtu kati na Coronavirus.

Hongera serikali kwa hatua ya kutosikiliza miluzi yetu mingi inayoweza kumpoteza mtu.
 
Kwenye mapambano haya kila nchi itatoka na CD player yake, jinsi nchi ilivyokuwa ikiendesha vita vyake, sasa kila nchi ikiwa na Aina moja tu ya kuicheza hii sinema, kama Dunia yote itacheza Kwa mtindo mmoja uleule, wataujuaje utamu wa mchezo unaochezwa na Jemedari Magufuli pamoja na wasaidizi wake? Kwa TZ Huu mchezo ulivyokaa utadhani hakuna vita vinavyoendelea, kumbe hata wewe unanawa maji kila Wakati, ukishupaza shingo, unazikwa na mapambano yanaendelea, fuata maelezo ya watalaamu, Tanzania bila Corona inawezekana chini ya Jemedari JPM
..kuwaweka watu majumbani huku huna CAPACITY ya kuwapima na " kuwachomoa" waathirCDika na kuwahifadhi haisaidii chochote.

..Magufuli hakuwa options zozote zile. Kuwaambia wananchi waongeze MAOMBI amekuwa mkweli.

..Wananchi wasio na maji salama ya kunywa utawaambiaje waoshe mikono mara kwa mara, tena watumie na sabuni? It is unrealistic.
 
Ndio nauliza mkuu umeacha upinzani? Maana humu ndio utaratibu wetu ukikosoa basi wewe ni mpinzani na ukipongeza au kuunga mkono basi ni ccm.

Sio kweli usemacho, kila mara tuko humu humu ndani, michango yote tunaiona, ni wakati gani unaitwa ccm hilo pia linaeleweka. Acha upotoshaji kama vile hatujui michango ikoje humu ndani.
 
Huu uzi pamoja na ulivyojitahidi kuupamba nasikitika kukutaarifu ni moja ya mifano hai TWAWEZA wanapaswa kuiambatanisha kuhusiana kale ka 'trait' ka watanzania kwenye maamuzi yao yanayowagharimu vilivyo bila kutambua.

Tunayo matatizo ya elimu na bahati mbaya watawala wetu ambao walipaswa kuwa viongozi wetu wanayatumia to our detriment.

Cases tatu za lockdown zinazotuzunguka:

1. Rwanda: Wananchi wame elimishwa sana kuhusu huu ugonjwa. "Inafahamika pasi na shaka kwa watu wote kuwa huu ugonjwa ni wetu". Yaani wao kama jamii.

Kwamba jamii yote iko salama kama hakuna mtu hata mmoja anao. Vinginevyo si tajiri wala masikini bali wote ni marehemu watarajiwa.

Serikali za mitaa zina orodha ya familia zinazohitaji msaada wa chakula. Kuna mfuko unaochangiwa na makampuni na watu binafsi kusaidia familia hizo. Serikali inakamilisha kilicho pungua.

Tozo mbalimbali zikiwamo kodi za serikali, marejesho ya mikopo bank, malipo ya kodi za mapango, gharama za miamala simu nk zimeahirishwa au kuondolewa kabisa kuwapa watu ahueni.

Rwanda wako kwenye lockdown ya siku 14 tayari wanabakiwa na takribani siku 7 hakuna aliykufa na njaa wala kukosa chakula.

Malo ya mizigo yanaingia na kutoka Rwanda si kuwa total lockdown maana yake kila kitu kimesimama na watu wamefungiwa vyumbani. Acheni kupotosha.

2. Kenya Mombasa wanataka total lockdown. Hawafurahishwi na hii partial ambayo kimsingi ni curfew iliyopo in place sasa hivi. Tayari Mombasa wamesha mobilize pesa kuhakikisha hakuna familia itaathirika maamuzi ya total lockdown yatakapotoka.

Pana nafuu nyingi serikali imetoa. Mishahara ya wakuu wakiwamo wabunge imekatwa.

Wananchi wanaelewa na wako pamoja katika hili.

Nafuu nyingi kwenye tozo mbalimbali zimewekwa kama ilivyo Rwanda. Hawa ni muda mdogo tu bado wanaenda total lockdown kama Rwanda.

3. Uganda huku kuna jenerali mwenye mkono wa chuma (haambiliki labda naye wanamwita jiwe). Ushirikishaji umma kwake ni mdogo. Yeye badala ya kwenda total lockdown anafanya ubaguzi wa wazi na bila kujali.

Mifano ni mingi: Kwa nini bodaboda, mabasi nk wasimame hali masoko yako wazi? Hana mipango yoyote ya kuwafidia wananchi, wengine wana mikopo bank, kula yao ni kazi ya siku nk. Hapa ni chaos.

Kwetu sisi tumebakia kudanganyana muda unakwenda. Total lockdown ni inevitable. Kama alivyosema Ramaphosa ni suala la muda tu. Jinsi muda unavyokwenda itaja tugharimu zaidi.

Kina Msigwa, kina Mashinji na wenzao Ilikuwa wafungwe. Ndani ya siku 3 zilichangwa 350,000,000/= na wananchi. Kwa nini kwenye jambo serious hili mnaliwekea siasa uchwara namna hii. Kwa nini isiwezekane kuchangisha kwa watakakuwa na upungufu wa chakula kama serikali haitaona umuhimu huo.

Hata hivyo kwa kipindi hiki cha dharura hii ya kuishi au kufa serikali inapaswa kusimamisha miradi yote mikubwa. Haya mambo ya uchaguzi mkuu si priority tena. Kuna ruzuku za vyama vya siasa. Tuweke raslimali zote tutoke hapa tukiwa salama kwanza mengine baadaye.

Taabu iko wapi? Hiyo njaa mnayokaa mnaongea iko wapi?

Pathetic!

TWAWEZA ushahidi mwingine katika ule utafiti wenu pendwa ni huu uzi wa huyu bwana msemajiukweli.
Mimi nimeongelea mambo yaliyo halisi, wewe unatuletea nadharia!
 
Asante sana mkuu kwa uchambuzi mzuri na wa maana sana.
Nawashangaa hawa waajiriwa wa serikali wanataka nchi iwekwe karantini wakati uchumi utasimama ukisimama kinachofuata ni kupunguza mishahara tu.

Nani kaumia hapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Aksante na wewe Mkuu kwa maoni yako.
 
Huko kwa Madiba raia wameligomea tamko halali la serikali yao....sababu kuu ni njaa wananzengo hawana chakula ndani... wanasema watapigana ana kwa ana na covid 19 afe yeye au wafe wao ila lockdown kwao itaishia mdomoni mwa watawala tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali zinawapa wananchi wake wachagua jambo moja kati ya mawili! Kukaa ndani na kufa kwa njaa au kutoka nje na kupata kipigo cha "mbwa koko".

Wananchi wameanza kuchagua kutoka nje ili kupambana na watoa kipigo!
 
Back
Top Bottom