Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Kumbe wewe haujui hata maana ya" lockdown ".
sasa ukiacha maduka ya chakula WAZI atanunua nani wakati umekata watu wasitoke NJE?
Ndo maana nawaambia hyo ishu ni ngumu.
Angalia wahindi wanavyotiana bakora
Hakuna nchi iliyozuia uuzwaji wa chakula.View attachment 1401453

Mwisho wa hatua za huyo bwana zipo wazi. Ndio sawa na ubishi wenu kama mnadhani kutakuwa na outcome nyingine serikari isipoumiza kichwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waangalie kwanza India wanavyotiana bakora watu wanalia kama watoto..
Leo hii tukisema tusifanye kazi hata uchumi wa nchi unashuka na mapato hamna.
Hata wale wanategemea mwisho wa mwezi wa naweza wasilipwe..
Alafu unaweza ukawa na hela lakini maduka yamefungwa,magenge yamefungwa utanunua nini?.
Pata picha pale kariakoo pafungwe?.
BORA CORONA KULIKO NJAA.
Kibongo bongo kumwambia mtu akae ndani siku 14 ni sawa na kumuambia achague kati ya njaa na corona ipi inaua vibaya.. obvious kila mtu ata-take chance yake kitaa kuliko kufa na njaa..

Maana njaa ni 100% inakudedisha bila kuangalia lakini corona unaweza kupona..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waangalie kwanza India wanavyotiana bakora watu wanalia kama watoto..
Leo hii tukisema tusifanye kazi hata uchumi wa nchi unashuka na mapato hamna.
Hata wale wanategemea mwisho wa mwezi wa naweza wasilipwe..
Alafu unaweza ukawa na hela lakini maduka yamefungwa,magenge yamefungwa utanunua nini?.
Pata picha pale kariakoo pafungwe?.
BORA CORONA KULIKO NJAA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jana uganda watu wawili wamepigwa risasi eti kisa kukataa kukaa ndani , ongezea na viboko vya india + kenya mambo sio mambo watu wanapigwa balaa.

Kwakweli bora mtu apate corona kuliko mateso ya ajabu hivyo.. sijawahi kuona watu wasiokuwa civillized na wasio tumia common sense kama polisi na wanajeshi.. hawa jamaa hamnazo kabisa.
 
Ndio maana nikasema uwezo wetu wa kiuchumi na mazingira ya kijamii hayaruhusu wananchi kuwafungia ndani zaidi ya wiki moja bila kufanya shughuli za kuwaletea chakula cha siku.

Maana ya maneno yangu niliyosema, think globally but act locally yanasadifu dhana yangu.
Ndio maana na mimi nikasema tatizo letu ni fatalism thinking.

Kwa wenzetu wanapopata majanga ndio akili zao zinapofanya kazi zaidi kutafuta solution; kwenye muda mfupi wameweza kuja na cheap hand held technology inayoweza pima Corona ndani ya nusu saa na kutoa majibu, kuongeza hospital treatment capacity wameweza modify mashine moja ya ventilator kuwa na uwezo wa kuhudumia watu wawili kwa wakati, etc wakati researches zingine luluki za kupambana na changamoto zinaendelea.

Sisi tatizo letu waafrica atupendi kuumiza vichwa tunapenda simple solutions tena ambazo extreme; kusema watu waendelee na maisha kama kawaida ni sawa kukubali kushindwa vita kabla aijaanza.

Let me assure you ata kwa mabeberu compliance is not voluntary ukikamatwa unadhurura bila ya sababu maalum kuna fines, mkikutwa mpo kikundi fine na ukikutwa umetoka una dalili za mafua wanafikiria kukupeleka jela that is how serious they are kwenye kuakikisha wanaidhibiti Corona. Na hawa watu atuwafikii kwa ubora wa hospitali, vifaa tiba wala financial resources.

Chukulia waziri mkuu wa UK, waziri wa afya na Chief medical officer; watu ambao unategemea ofisi zao zitakuwa disinfected regularly, wao wenyewe wana elimu ya kutosha kuweza kuchukua hatua za kujikinga na ndio leaders kwenye kupambana na Corona lakini wamepata maambukizi; sembuse mama ntilie na wateja wake kwenye barabara zetu.

Ni hivi hii Corona tuisikie tu kwa wenzetu muulize mtu anaeishi U.K akueleze usione PM na hao vigogo waliobainika wamepimwa ukadhani kila mtu ana hiyo nafasi ya kupata kipimo; malaki ya watu wanaugulia mafua ndani na kujitibu wenyewe bila ya kuelewa kama wana Corona au mafua ya kawaida.

Uruhusiwi kwenda kwa GP, Pharmacy wala hospitali kama una mafua; umtafute mtu wa kwenda kukununilia dawa unazozijua ujitibie. Kupiga simu hospitali mpaka uwe na homa kali na kikoozi kianze.

Kwa ivyo hao unaoona wamepimwa kama Prince Charles, PM na wengine ni kwa sababu ya kuwa na nafasi. Wenzetu wapo serious na hii control kwa sababu wanajua nini kitafuata wakisema life has to go on as normal. Sasa sisi ambao atufanyi research zozote tunadhani lockdown ni swala la option well it can be but a very costly one.
 
Kumbe wewe haujui hata maana ya" lockdown ".
sasa ukiacha maduka ya chakula WAZI atanunua nani wakati umekata watu wasitoke NJE?
Ndo maana nawaambia hyo ishu ni ngumu.
Angalia wahindi wanavyotiana bakora

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye lockdown essential services zinafanya kazi kama kawaida na kuna utaratibu wa kutoka, kupeana gap ya six feet, etc. Kila nchi inatoa maelezo yake ya social interaction zingine kutoka mpaka upate permits.
 
Unatoa ukweli halafu unajikanyaga! Ukiona mtu anasema tumuachie mungu, jua kuwa maji yakezidi unga! Hivi ulitaka JPM aseme nini kama si kujaribu kuwaconsole anaowaongoza. Maana kwa hali ilivyo anamwachia mungu tu. Umesahau viongozi kama issue ya maji maji hao ndiyo Viongozi
Hivi JPM alisema tumwachie Mungu au anahamasisha watu waendelee kujazana kwenye nyumba za ibada na kuaminisha watu janga linaweza kutoweka kwa maombi?! Ajabu anatolea mfano wa wana-Israel na ugonjwa wa tauni badala ya kutuambia katika dunia ya leo ni janga lipi liliwahi kutoweka kwa ibada!!!

Btw, yaani seriously unalinganisha akina Kinjeketile Ngwale waliokuwa hawajui lolote kuhusu sayansi zaidi ya matambiko, na JPM anayefahamu umuhimu wa sayansi kwenye kupambana na majanga?!
 
JokaKuu,
Kwani baadhi ya nchi kama Uganda, Rwanda, South Africa na Kenya ambao wametoa amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao wana CAPACITY ya kuwapima, kuwahifadhi na kuwatibu wagonjwa wote wa COVID-19?

Kwani wao hawakuwa na option kama ilivyofanya serikali ya Tanzania?

Nadhani hujajua hata msingi wa mada yangu!
Huyo akishakuona umemsifia tu Magufuli, atataka kumcrush magufuli au nchi, kwa namba yoyote ile, ndio roho lake linasuhuzika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi JPM alisema tumwachie Mungu au anahamasisha watu waendelee kujazana kwenye nyumba za ibada na kuaminisha watu janga linaweza kutoweka kwa maombi?! Ajabu anatolea mfano wa wana-Israel na ugonjwa wa tauni badala ya kutuambia katika dunia ya leo ni janga lipi liliwahi kutoweka kwa ibada!!!

Btw, yaani seriously unalinganisha akina Kinjeketile Ngwale waliokuwa hawajui lolote kuhusu sayansi zaidi ya matambiko, na JPM anayefahamu umuhimu wa sayansi kwenye kupambana na majanga?!
Wewe una matatizo. Unafikira za kimihemko. Kutompenda JPM kusiwe ni kikwazo cha kuwa na fikra huru. Utapata ugonjwa wa moyo maana unaye hadi 2025.
 
Magu hakulaumiwa kwa hayo uliyosema bali kalaumiwa kwa mambo kama pale aliposema hawezi kuzuia watalii kuingia nchini! Uzuri ni kwamba, hao watalii wenyewe wana akili na wanafahamu risk iliyopo kwa wao kuendelea kusafiri, na kwahiyo wameamua kujizuia wenyewe huko huko kwao!

Na kwavile ndege nyingi zimesimamisha international flights, hiyo ndo nafuu yenyewe kwetu vinginevyo lau kama airlines na watalii wangekuwa na akili kama za JPM, balaa ambalo lingekuwa limeshatokea tungekuwa tunatafutana hivi sasa!

Zanzibar kwa mfano, wanapokea watalii wengi sana kutoka Italy! Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo Watalii wa Italy wangeendelea kuingia?!

Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo wananchi kwenye mataifa yaliyoathirika wangeendelea kumiminika kwa sababu tu Mpiga Ramli mmoja anaamini coronavirus haifui dafu mbele ya ibada?!

Lingine alilolaumiwa JPM ni kauli yake ya majuzi kwamba eti watu waendelee tu kumiminika kwenye nyumba za ibada na kwamba eti COVID-19 haiwezi kuishinda Damu ya Yesu!!

Ni mtu wa ajabu tu ndie anaweza kutetea ujinga kama huu kwa sababu hakuna janga hata moja lililowahi kuzimwa kwa watu kujazana makanisani na misikitini!

And FYI, zipo nchi nyingi tu ambazo zilidhani zingeendelea kuwa salama! Spain kwa mfano, daktari mmoja alifikia hadi kusema ni ngumu sana kwa Spain kupata maambukizo mengi kwa sababu tu walidhani kuto-share mpaka na Italy ingeweza kuwa salama kwao!

Leo hii, it's a matter of time kabla Spain hawajaifunika Italy!!

Hata Trump nae mwanzoni wala hakudhani ingekuwa serious issue kwa US! Leo hii US imeyapiku mataifa yote kwa idaidi ya maambukizi!!

So, endeleeni tu kutetea ujinga kwa sababu ndicho mlichoapa kukifanya!!
Duh!....hayo maneno uliyomalizia hapo chini....🙄🙄🙄...
 
Kwanini shule na vuo vimefungwa kama nchi za magharibi Fallacy! Nchi za magharibi zimelazimika kutokana na ukali wa maradhi.Tarehe 26 Italy wamefariki watu 900 katika 24 hours, angalia takwimu katika nchi nyingine pia.
Uchumi wa nchi hizo hasa sekta za anga, utalii, uzalishaji zimeathirika katika kiwango kikubwa
Si kweli kuwa hali ya uchumi ni nzuri, bali hali ya maradhi inalazimisha hilo kutokea.
Marekani ina deni la dollar Trilioni 2 kukabiliana na athari za COVID kiuchumi na kijamii.
Wananchi wa nchi hizo hulipa kodi ya EI(Employment Insurance) kila 'cheki' ya mshahara.
Hiyo ni Insurance ikitokea lisilotarajiwa kama sasa .
Hivyo Serikali zinalipa wananchi Insurance zao si kama wanatoa bure ndugu yangu.
Tanzani hatuna EI, hilo ni kosa letu. Wenzetu wanajua Insurance maana yake nini, sasa tunalaumu kwanini.
Mortgage hazijabebwa na serikali, kinachotokea ni udhamini lakini mwisho wa siku utalipa na riba juu.
Ni muhimu kuelewa system za nchi za magharibi zinafanyaje kazi, hata hivyo, kwa Watanzania nina uhakika utawapa wengi tu. Ukweli ni kuwa unapotosha. Unaogopa machafuko, huogopi vifo. Kwamba ikiwa watu watatoka na kufa kwa COVID hilo lina nafuu kuliko machafuko unayosema yatatokea. Unajua machafuko yakitokea nani anaathirika! Muongo mkubwa sana wewe.
Nchi za magharibi kama hufanyi kazi unakufa. Ni rahisi ku survive Tanzania kwa mjomba, kaka , dada na shemeji kwa siku kadhaa. Ukiwa nchi za mgaharibi kuna kitu kinaitwa ''bill'' hakuna mtu wa kukulipia.

Watu wanafanya kazi sana kwasababu ukizembea tu huna nyumba, huna chakula unaondoka.
Tafadhali acha uongo, watu waliowahi kuishi na wanaoishi magharibi wakikusoma hapa wanatema mate
Kumbuka wewe ni mmoja wa viongozi serikalini, sasa hoja kama hizi unatia shaka sana.
Wewe ndugu muongo sana.
Kama kuna mahali watu wanakula good time za maisha ni magharibi. Wakati wa baridi shughuli zinahamia ndani, huko watu wanaburudika kama vile hakuna baridi. Acha kudanganya watu kabisa Unakumbuka kipindu pindu kilipoingia rufiji kwa mara ya kwanza, nini kilitokea! nakumbuka? . Finally upo katika terms na ukweli. najua kwamba umepotosha vya kutosha, nafsi inakusuta na hapa mwisho unaonyesha kwa uwazi ukubwa wa tatizo na matokeo yake! unajua lakini uliamua kupotosha umma, nafsi inakusuta.

JokaKuu Pascal Mayalla Alinda
Mleta mada amepotosha kwa kiasi kikubwa. Ameandika uwongo mwingi na kuwaamunisha watu yasiyokuwepo.

Sidhani kama anazifahamu nchi za Magharibi labda ni wale wanaoenda leo, wanaondoka keshokutwa.

Kama ulivyonena, hakuna nchi ambazo ni vigumu sana kuishi bila kufanya kazi, kama nchi za Magharibi.
 
Acha kupotosha watu wewe!

Hakuna aliyewahi kumlaumu Jiwe eti kwa sababu ya kuacha watu waendelee kufanya kazi bali watu walimlaumu kwa mambo kama alivyokuwa anaongea kwa mbwembwe kwamba hawezi kuzuia watalii kuingia nchini, kufuta international flights na huu ujinga wa last week kwamba eti watu waendelee tu kujazana kwenye nyumba za ibada na kwamba COVID-19 haiwezi kufua dafu mbele Damu ya Yesu!

Ni rahisi wa hovyo hovyo tu kama Magufuli ndie anaweza kuaminisha watu eti unaweza kupambana na coronavirus kwa maombi!
Hivi wewe kwa akili yako ya kimihemko unadhani JPM alimaanisha hiyo? It was a political statement tu.
 
Mkuu kwa nchi za Africa ni HAIWEZEKANI, ili upate mlo ni lazima utoke otherwise utakufa njaa
Ila huyu mzee namsifu hapa tu. Kwa kweli kwa huku Africa swala la watu kubaki nyumbani ni haliwezekani. Tusidanganyane.

Huko Kenya kama hivo hali tete imebidi wabadili msimamo. Uganda hali ngumu mpaka wanachapana bakora.

Hivi mimi uniambie nikae nyumbani na hela ya kula sina? Serious?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzungu anaamini dinosaurs walitoweka kwa sababu miaka zaidi ya million 200 dunia ilitandikwa na comet moja kubwa iliyouwa karibu viumbe vyote ardhini.

Leo kuna watu wameajiriwa kufanya kazi usiku na mchana kuangalia asteroid belt and beyond kama kuna comet kubwa zinazoweza kuja karibu na sayari yetu na wana mipango ya kuifuata huko huko kuipasua miaka kadhaa kabla ya kutufikia.

Ndio tujue huku kufungia watu sio sera ya kubahatisha washakumbana na haya matatizo in the past kupitia ‘spanish flu’, washafanya experiments za simulation kutokana na tabia watu ndani ya jamii zao, washajifunza haya maambukizi yanavyotokea, hatua za kuchukua yakijirudia, wana optional solutions za scenarios mbali mbali kwenye kukabiliana na majanga ya sasa na mengine mbalimbali yanayoweza wakumba (these ppl plan ahead).

Itafika wakati lockdown itakuwa mandotory tu ata kwa Tanzania kukabiliana na virus pamoja na watu mnavyojaribu kujiaminisha; kwa sababu ndio njia pekee health systems zinavyoweza kukabiliana na utoaji wa huduma given their capacity.

Busara ni kushauri watu wenye kuweza kurudi vijijini kwa muda au kuelekea maeneo yenye less population density kuanza kufanya ivyo au kuja na ubunifu mwingine wa kuwalisha watu haswa maeneo ya mjini; hila lockup is inevitable watu wajiandae kabisa kisaikolojia.

Just wait
Vijijini ndio kuna hatari zaidi kama lockdown itafanyika, hakuna miundo mbinu yoyote ya kumuwezesha mtu kukaa ndani hata siku moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..kwenye kuzuia watu wa nje kuingia nchini nakubaliana na wewe.

..lakini janga hili lime-expose uwezo wa Jpm na uwezo wa serikali yetu.
Lime expose Kwa aslimia ndogo saana, tunasubilia full detailed capacity na nadhani in few days tutaelewa zaidi!
 
Magu hakulaumiwa kwa hayo uliyosema bali kalaumiwa kwa mambo kama pale aliposema hawezi kuzuia watalii kuingia nchini! Uzuri ni kwamba, hao watalii wenyewe wana akili na wanafahamu risk iliyopo kwa wao kuendelea kusafiri, na kwahiyo wameamua kujizuia wenyewe huko huko kwao!

Na kwavile ndege nyingi zimesimamisha international flights, hiyo ndo nafuu yenyewe kwetu vinginevyo lau kama airlines na watalii wangekuwa na akili kama za JPM, balaa ambalo lingekuwa limeshatokea tungekuwa tunatafutana hivi sasa!

Zanzibar kwa mfano, wanapokea watalii wengi sana kutoka Italy! Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo Watalii wa Italy wangeendelea kuingia?!

Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo wananchi kwenye mataifa yaliyoathirika wangeendelea kumiminika kwa sababu tu Mpiga Ramli mmoja anaamini coronavirus haifui dafu mbele ya ibada?!

Lingine alilolaumiwa JPM ni kauli yake ya majuzi kwamba eti watu waendelee tu kumiminika kwenye nyumba za ibada na kwamba eti COVID-19 haiwezi kuishinda Damu ya Yesu!!

Ni mtu wa ajabu tu ndie anaweza kutetea ujinga kama huu kwa sababu hakuna janga hata moja lililowahi kuzimwa kwa watu kujazana makanisani na misikitini!

And FYI, zipo nchi nyingi tu ambazo zilidhani zingeendelea kuwa salama! Spain kwa mfano, daktari mmoja alifikia hadi kusema ni ngumu sana kwa Spain kupata maambukizo mengi kwa sababu tu walidhani kuto-share mpaka na Italy ingeweza kuwa salama kwao!

Leo hii, it's a matter of time kabla Spain hawajaifunika Italy!!

Hata Trump nae mwanzoni wala hakudhani ingekuwa serious issue kwa US! Leo hii US imeyapiku mataifa yote kwa idaidi ya maambukizi!!

So, endeleeni tu kutetea ujinga kwa sababu ndicho mlichoapa kukifanya!!

Siamini kuwa mtu yeyote anaemuabudu Magufuli atakuwa na mental capacity ya kuelewa logic iliyomo kwenye post yako hii.
 
Wewe una matatizo. Unafikira za kimihemko. Kutompenda JPM kusiwe ni kikwazo cha kuwa na fikra huru. Utapata ugonjwa wa moyo maana unaye hadi 2025.
Ngoja nikupuuze if you don't mind.
 
..kuwaweka watu majumbani huku huna CAPACITY ya kuwapima na " kuwachomoa" waathirika na kuwahifadhi haisaidii chochote.

..Magufuli hakuwa options zozote zile. Kuwaambia wananchi waongeze MAOMBI amekuwa mkweli.

..Wananchi wasio na maji salama ya kunywa utawaambiaje waoshe mikono mara kwa mara, tena watumie na sabuni? It is unrealistic.

Sasa ndio muone akili au mantiki ya mtu kutumia pesa zake nyingi kununua ndege, kujenga reli etc wakati watu wake hawawezi kupata maji salama.
Halafu kuna mtu anadai huyo ndie Rais alietakiwa!! Pathetic.
 
Mzungu anaamini dinosaurs walitoweka kwa sababu miaka zaidi ya million 200 dunia ilitandikwa na comet moja kubwa iliyouwa karibu viumbe vyote ardhini.

Leo kuna watu wameajiriwa kufanya kazi usiku na mchana kuangalia asteroid belt and beyond kama kuna comet kubwa zinazoweza kuja karibu na sayari yetu na wana mipango ya kuifuata huko huko kuipasua miaka kadhaa kabla ya kutufikia.

Ndio tujue huku kufungia watu sio sera ya kubahatisha washakumbana na haya matatizo in the past kupitia ‘spanish flu’, washafanya experiments za simulation kutokana na tabia watu ndani ya jamii zao, washajifunza haya maambukizi yanavyotokea, hatua za kuchukua yakijirudia, wana optional solutions za scenarios mbali mbali kwenye kukabiliana na majanga ya sasa na mengine mbalimbali yanayoweza wakumba (these ppl plan ahead).

Itafika wakati lockdown itakuwa mandotory tu ata kwa Tanzania kukabiliana na virus pamoja na watu mnavyojaribu kujiaminisha; kwa sababu ndio njia pekee health systems zinavyoweza kukabiliana na utoaji wa huduma given their capacity.

Busara ni kushauri watu wenye kuweza kurudi vijijini kwa muda au kuelekea maeneo yenye less population density kuanza kufanya ivyo au kuja na ubunifu mwingine wa kuwalisha watu haswa maeneo ya mjini; hila lockup is inevitable watu wajiandae kabisa kisaikolojia.

Just wait
Umeongea kama MTU smart, watanzania hatutambui kuwa hakuna jipya chini ya jua, we think we can outsmart smartness itself!!
 
Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanasiasa kutaka Rais Magufuli na serikali yake wafunge mipaka ya nchi na kutoa tamko la kuwataka/kuwalazimisha wananchi wabakie majumbani mwao ili ‘’ kupambana’’ na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 yasisambae nchini.

Mashinikizo yanayotolewa kwa Rais Magufuli unaweza kuyaona niya msingi kama utadhani mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii ni sawa na mazingira ya ''Nchi za Magharibi'' ambazo zinatumia mbinu hii katika kukabiliana na janga la COVID-19.

Nakumbukwa kwenye sherehe ya wafanyakazi mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''Mtu yeyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, na yeye anajua una akili na anajua kuwa niya kipumbavu usipoyakataa anakudharau''.

Ni ukweli kuwa, Mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini yako tofauti sana na mazingira ya nchi za Magharibi na kwa msingi huu, haiwezekani mbinu za kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 yakafanana na nchi hizo.

Mwanasiasa wa Marekani aitwaye Donald Rumsfeld aliwahi kusema, ‘’You go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time.”

Kwa kiswahili ambacho sio sanifu, Donald Ramsfeld alisema, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’.

Kwa mantiki hii, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi la kiuchumi na kijamii alilonalo na sio ambalo baadhi ya wanasiasa wanataka liwepo wakati halipo.

Kwenye suala la kiuchumi, nchi za Magharibi zimeweza kufanikiwa kufunga mipaka na kuwalazimisha wananchi wake wabakie majumbani mwao kwa masaa 24 bila kutoka nje kwa sababu mazingira ya kiuchumi yanaruhusu kufanya hivyo.

Kwa sasa wananchi wote wa nchi hizo pamoja na kwamba hawafanyi kazi lakini serikali imeamua kuwalipa mishahara na pesa za kujikimu na maisha wananchi wake wote mpaka pale watakapoanza kufanya kazi tena. Hata malipo rehani (mortgage) kwa sasa yamebebwa na serikali.

Kwa upande wa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ kama Tanzania, serikali haiwezi kubeba jukumu la kiuchumi kama zilivyofanya nchi za Magharibi kwa sababu haina uwezo huo na kama serikali italazimisha wananchi wake wabakie majumbani basi tutegemee machafuko nchini au familia nyingi kufa kwa njaa hasa zile zinazoishi kwenye maeneo ambayo bila kutoka ‘’nje ya nyumba’’ familia haiwezi kupata chakula cha siku.

Kwa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwamo Tanzania, binadamu anaishi kwa jasho/nguvu zake lakini kwa ‘’nchi za Magharibi’’, binadamu anaweza akaishi bila jasho/nguvu zake bali kwa msaada kutoka serikalini.

Tanzania vile vile ni ''lango kuu'' na mkondo wa usafirishaji katika nchi karibu nane ambazo hazina bahari.

Haishangazi kwa sasa tumeanza kuona wananchi wakipigwa risasi katika nchi za Rwanda na Uganda kwa sababu wamekataa kutii amri ya kubakia majumbani mwao kutokana na ukweli kuwa kubaki ndani pia ni kukaribisha kifo kwa njaa. Ni bora watoke nje wakajaribu bahati ya kutafuta chakula kuliko kubaki majumbani mwao. Nadhani baada ya wiki moja hali itakuwa mbaya zaidi.

Huko Kenya, Rais Kenyatta amegundua makosa na kwa sasa amebadili msimamo wake ambapo badala ya amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao kwa saa 24 kwa sasa watafanya hivyo kuanzia majira ya saa 11 za jioni hadi saa 11 alfajiri. Hii mbinu ya Rais Kenyatta inashangaza kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi katika nchi zetu wanakusanyika zaidi mchana kuliko usiku!

Kwenye suala la kijamii, nchi za Magharibi zimefanikiwa kutokana na ukweli kuwa jamii zake zinaishi maisha ya ‘’kipweke’’. Ninaposema kipweke nina maana mazingira ya hali ya baridi na kazi yamewafanya wananchi wawe wanaishi maisha ya kujifungia ndani hata wakitoka kazini. Wenzetu hawana hii dhana ya ‘’kwenda kwenye kijiwe’’ kupiga stories au kwenda kwa ndugu au rafiki bila kutoa taarifa.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo mikusanyiko ya kijamii na kifamilia ni sehemu muhimu ya maisha, ni vigumu sana kwa serikali kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wengi kama itatoa amri ya kuwataka wananchi wasifanye hivyo na badala yake wabakie majumbani mwao kwa saa 24.

Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwemo Tanzania haiwezekani kuzitumia kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.

Kama alivyosema Donald Ramsfeld, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’. Kwenye janga hili la COVID-19, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi alilonalo!

Subiri siku nchi zote jirani zetu zitakapofunga mipaka yao na sisi na kuzuia watu kutoka kwetu kuingia kwao ndipo utaelewa maana ya maamuzi ya kipumbavu yanayochukuliwa sasa.
 
Back
Top Bottom