Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanasiasa kutaka Rais Magufuli na serikali yake wafunge mipaka ya nchi na kutoa tamko la kuwataka/kuwalazimisha wananchi wabakie majumbani mwao ili ‘’ kupambana’’ na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 yasisambae nchini.

Mashinikizo yanayotolewa kwa Rais Magufuli unaweza kuyaona niya msingi kama utadhani mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii ni sawa na mazingira ya ''Nchi za Magharibi'' ambazo zinatumia mbinu hii katika kukabiliana na janga la COVID-19.

Nakumbukwa kwenye sherehe ya wafanyakazi mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''Mtu yeyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, na yeye anajua una akili na anajua kuwa niya kipumbavu usipoyakataa anakudharau''.

Ni ukweli kuwa, Mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini yako tofauti sana na mazingira ya nchi za Magharibi na kwa msingi huu, haiwezekani mbinu za kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 yakafanana na nchi hizo.

Mwanasiasa wa Marekani aitwaye Donald Rumsfeld aliwahi kusema, ‘’You go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time.”

Kwa kiswahili ambacho sio sanifu, Donald Ramsfeld alisema, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’.

Kwa mantiki hii, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi la kiuchumi na kijamii alilonalo na sio ambalo baadhi ya wanasiasa wanataka liwepo wakati halipo.

Kwenye suala la kiuchumi, nchi za Magharibi zimeweza kufanikiwa kufunga mipaka na kuwalazimisha wananchi wake wabakie majumbani mwao kwa masaa 24 bila kutoka nje kwa sababu mazingira ya kiuchumi yanaruhusu kufanya hivyo.

Kwa sasa wananchi wote wa nchi hizo pamoja na kwamba hawafanyi kazi lakini serikali imeamua kuwalipa mishahara na pesa za kujikimu na maisha wananchi wake wote mpaka pale watakapoanza kufanya kazi tena. Hata malipo rehani (mortgage) kwa sasa yamebebwa na serikali.

Kwa upande wa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ kama Tanzania, serikali haiwezi kubeba jukumu la kiuchumi kama zilivyofanya nchi za Magharibi kwa sababu haina uwezo huo na kama serikali italazimisha wananchi wake wabakie majumbani basi tutegemee machafuko nchini au familia nyingi kufa kwa njaa hasa zile zinazoishi kwenye maeneo ambayo bila kutoka ‘’nje ya nyumba’’ familia haiwezi kupata chakula cha siku.

Kwa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwamo Tanzania, binadamu anaishi kwa jasho/nguvu zake lakini kwa ‘’nchi za Magharibi’’, binadamu anaweza akaishi bila jasho/nguvu zake bali kwa msaada kutoka serikalini

Tanzania vile vile ni ''lango kuu'' na mkondo wa usafirishaji katika nchi karibu nane ambazo hazina bahari.

Haishangazi kwa sasa tumeanza kuona wananchi wakipigwa risasi katika nchi za Rwanda na Uganda kwa sababu wamekataa kutii amri ya kubakia majumbani mwao kutokana na ukweli kuwa kubaki ndani pia ni kukaribisha kifo kwa njaa. Ni bora watoke nje wakajaribu bahati ya kutafuta chakula kuliko kubaki majumbani mwao. Nadhani baada ya wiki moja hali itakuwa mbaya zaidi.

Huko Kenya, Rais Kenyatta amegundua makosa na kwa sasa amebadili msimamo wake ambapo badala ya amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao kwa saa 24 kwa sasa watafanya hivyo kuanzia majira ya saa 11 za jioni hadi saa 11 alfajiri. Hii mbinu ya Rais Kenyatta inashangaza kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi katika nchi zetu wanakusanyika zaidi mchana kuliko usiku!

Kwenye suala la kijamii, nchi za Magharibi zimefanikiwa kutokana na ukweli kuwa jamii zake zinaishi maisha ya ‘’kipweke’’. Ninaposema kipweke nina maana mazingira ya hali ya baridi na kazi yamewafanya wananchi wawe wanaishi maisha ya kujifungia ndani hata wakitoka kazini. Wenzetu hawana hii dhana ya ‘’kwenda kwenye kijiwe’’ kupiga stories au kwenda kwa ndugu au rafiki bila kutoa taarifa.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo mikusanyiko ya kijamii na kifamilia ni sehemu muhimu ya maisha, ni vigumu sana kwa serikali kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wengi kama itatoa amri ya kuwataka wananchi wasifanye hivyo na badala yake wabakie majumbani mwao kwa saa 24.

Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwemo Tanzania haiwezekani kuzitumia kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.

Kama alivyosema Donald Ramsfeld, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’. Kwenye janga hili la COVID-19, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi alilonalo!
umechambua na kuelezea vizuri sana,hakunaga darasa la mafanikio duniani,aliyefanikiwa anaweza akashindwa kukufundisha ww kufanikiwa maana tunatofautiana ki mtazamo,mahitaji,vipaumbele,machaguo,matamanio na mazngra,huwez ukategemea kufanikiwa kwa kuigaiga hata kwa vitu ambavyo kwako haviwezekani,hongera mkuu
 
Sio kweli usemacho, kila mara tuko humu humu ndani, michango yote tunaiona, ni wakati gani unaitwa ccm hilo pia linaeleweka. Acha upotoshaji kama vile hatujui michango ikoje humu ndani.
Nilichopotosha ni kipi na kwa nini nifanye hivyo? Labda wewe huoni kwa kuwa pengine ni muathirika wa hilo jambo ila sie tunaosoma sana michango ya watu humu kuliko kuchangia tunaona.
 
  • Thanks
Reactions: 30P
Acha kupotosha watu wewe!

Hakuna aliyewahi kumlaumu Jiwe eti kwa sababu ya kuacha watu waendelee kufanya kazi bali watu walimlaumu kwa mambo kama alivyokuwa anaongea kwa mbwembwe kwamba hawezi kuzuia watalii kuingia nchini, kufuta international flights na huu ujinga wa last week kwamba eti watu waendelee tu kujazana kwenye nyumba za ibada na kwamba COVID-19 haiwezi kufua dafu mbele Damu ya Yesu!

Ni rahisi wa hovyo hovyo tu kama Magufuli ndie anaweza kuaminisha watu eti unaweza kupambana na coronavirus kwa maombi!
Mkuu misimamo yako ya kisiasa inakufanya uonekane mpuuzi by far kuliko unayelazimisha aonekane hivyo. Wakati mwingine busara ikutume kuhifadhi hasira zako dhidi ya Rais hata kama haistahiki kwa kiasi hicho. Ok haya tufanye alikosea na kwa vile hana immune ya kutofanya kosa, wewe unashauri nini ili tukifuate? Chuki zako zinafanya baadhi ya watu wasi concentrate na hoja zako.
 
"Chige, post: 34792764, member: 12993"]
kalaumiwa kwa mambo kama pale aliposema hawezi kuzuia watalii kuingia nchini!
Na hapa kuna swali. Ikiwa Watalii wanaruhusiwa kwanini tufunge vyuo na shule za ndani?
Uzuri ni kwamba, hao watalii wenyewe wana akili na wanafahamu risk iliyopo kwa wao kuendelea kusafiri, na kwahiyo wameamua kujizuia wenyewe huko huko kwao
Wanafahamu healthcare system yetu ilivyo na kwamba, uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa sana. Hawana uhakika kama tuna respirator machine
Na kwavile ndege nyingi zimesimamisha international flights, hiyo ndo nafuu yenyewe kwetu vinginevyo lau kama airlines na watalii wangekuwa na akili kama za JPM, balaa ambalo lingekuwa limeshatokea tungekuwa tunatafutana hivi sasa!
Tumepata kinga bila kufanya lolote.
Lingine alilolaumiwa JPM ni kauli yake ya majuzi kwamba eti watu waendelee tu kumiminika kwenye nyumba za ibada na kwamba eti COVID-19 haiwezi kuishinda Damu ya Yesu!!
Nani mkatoliki zaidi ya Papa wa Vatican, Italy?
Ni mtu wa ajabu tu ndie anaweza kutetea ujinga kama huu kwa sababu hakuna janga hata moja lililowahi kuzimwa kwa watu kujazana makanisani na misikitini!
Marekani , Mapadri wanatoa ''sala ya mwisho'' Hao ndio walioleta dini huku kwetu.
Hata Trump nae mwanzoni wala hakudhani ingekuwa serious issue kwa US! Leo hii US imeyapiku mataifa yote kwa idaidi ya maambukizi!!
Aliita democrats hoax, leo ana bail out ya 2T. Unemployment imefikia record high! Stock zilifikia bear market.
So, endeleeni tu kutetea ujinga kwa sababu ndicho mlichoapa kukifanya!!
Huyu mleta uzi anawadanganya Watanzania akijua wengi hawajafikia nchi za magharibi. Anasema wanakula bata na mishahara inaingia bwerere. Haelezi nini kimetokea, inafikia mahali madaktari wanafanya DNR (Do not resuscitate)
Imefika mahali respirator zinachaguliwa, ukiwa above 60 unaachwa, anapewa kijana.

Hali ni mbaya msidanganye watu. Sasa hivi Tanzania tunaelekea majira ya baridi ''winter'' sijui kama virus hao wakiendelea kitatokea nini.
 
Zanzibar huko kuna wazungu wameona bora waendelee kukaa zanzibar kwa kipindi kuliko kurudi kwako kwenye korona.
 
Mkuu jmushi1;
Ni kweli time is the answer lakini pia mazingira ni sehemu muhimu sana katika kufikia maamuzi.

Nimesema, njia aliyotumia Rais Magufuli sio kwamba ndio sahihi katika kupambana na janga la COVID-19 bali njia aliyoitumia inaendana na mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii.

Tunaona kwa sasa kinachoendelea katika nchi za Kenya, Uganda na Rwanda baada ya kutumia njia kama iliyotumiwa na nchi za Magharibi. Polisi wameanza kuwapiga risasi wananchi ambao wameamua kukaidi amri za kujifungia ndani ya nyumba zao. Baada ya wiki moja, hali itakuwa mbaya zaidi.

Ni mtu mjinga ambaye atajifungia ndani ya nyumba yake wakati anakufa polepole kwa kukosa chakula wakati akitoka nje anaweza kupata chakula.

1. Kenya na Uganda na wengine hapa Afrika wanapata shida kwa sababu huwezi kutoa amri ya watu kujifungia ndani (lockdown) kwa mwezi mzima bila kuwahakikishia upatikanaji wa mahitaji yao muhimu hasa chakula na mengine...

2. Kiukweli kama serikali za nchi hizi zilitoa amri za namna hii bila kufikiri juu ya haya, walifanya makosa

3. Kwa hapa Tanzania, binafsi nadhani tuendelee kuchukua tahadhari na huu siyo muda wa kuanza kujisifu.

Ukijisifu hivi, utafika wakati utalazimika kuchukua hatua hizihizi na sijui utaweka wapi sura yako....!

Tuendelee kuomba na pengine kikubwa ni ukiona mwenzio ananyolewa, ni bora na wewe ukaanza kujiandaa kutia maji nywele zako...

Kama ni lazima kuwafungia watu ndani kama sehemu ya uponyaji wao, itakazimika iwe hivyo tu bila kujali nini ni nini....!!
 
Kibongo bongo kumwambia mtu akae ndani siku 14 ni sawa na kumuambia achague kati ya njaa na corona ipi inaua vibaya.. obvious kila mtu ata-take chance yake kitaa kuliko kufa na njaa..

Maana njaa ni 100% inakudedisha bila kuangalia lakini corona unaweza kupona..
Absolutely!
 
Back
Top Bottom