morphine
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 3,513
- 1,114
Hata mimi ndivyo nilivyoona!Kwa hili anastahili pongezi.
Nadhani unapoteza muda wako kutoa ushauri!Mkuu misimamo yako ya kisiasa inakufanya uonekane mpuuzi by far kuliko unayelazimisha aonekane hivyo. Wakati mwingine busara ikutume kuhifadhi hasira zako dhidi ya Rais hata kama haistahiki kwa kiasi hicho. Ok haya tufanye alikosea na kwa vile hana immune ya kutofanya kosa, wewe unashauri nini ili tukifuate? Chuki zako zinafanya baadhi ya watu wasi concentrate na hoja zako.
Mkuu;Zanzibar huko kuna wazungu wameona bora waendelee kukaa zanzibar kwa kipindi kuliko kurudi kwako kwenye korona.
Unataka kufanana kabisa na mfalme aliyekuwa akiitawala Dunia nyakati hizo za Biblia akiitwa Nebukadreza, naye hakuwahi kuipa nafasi nguvu ya Mungu ktk utawala wake kama unavyoidhihaki wewe,Acha kupotosha watu wewe!
Hakuna aliyewahi kumlaumu Jiwe eti kwa sababu ya kuacha watu waendelee kufanya kazi bali watu walimlaumu kwa mambo kama alivyokuwa anaongea kwa mbwembwe kwamba hawezi kuzuia watalii kuingia nchini, kufuta international flights na huu ujinga wa last week kwamba eti watu waendelee tu kujazana kwenye nyumba za ibada na kwamba COVID-19 haiwezi kufua dafu mbele Damu ya Yesu!
Ni rahisi wa hovyo hovyo tu kama Magufuli ndie anaweza kuaminisha watu eti unaweza kupambana na coronavirus kwa maombi!
Titafuteni pesa na maendeleo ya nchi zetu tuache kunyanyasika.Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanasiasa kutaka Rais Magufuli na serikali yake wafunge mipaka ya nchi na kutoa tamko la kuwataka/kuwalazimisha wananchi wabakie majumbani mwao ili ‘’ kupambana’’ na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 yasisambae nchini.
Mashinikizo yanayotolewa kwa Rais Magufuli unaweza kuyaona niya msingi kama utadhani mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii ni sawa na mazingira ya ''Nchi za Magharibi'' ambazo zinatumia mbinu hii katika kukabiliana na janga la COVID-19.
Nakumbukwa kwenye sherehe ya wafanyakazi mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''Mtu yeyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, na yeye anajua una akili na anajua kuwa niya kipumbavu usipoyakataa anakudharau''.
Ni ukweli kuwa, Mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini yako tofauti sana na mazingira ya nchi za Magharibi na kwa msingi huu, haiwezekani mbinu za kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 yakafanana na nchi hizo.
Mwanasiasa wa Marekani aitwaye Donald Rumsfeld aliwahi kusema, ‘’You go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time.”
Kwa kiswahili ambacho sio sanifu, Donald Ramsfeld alisema, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’.
Kwa mantiki hii, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi la kiuchumi na kijamii alilonalo na sio ambalo baadhi ya wanasiasa wanataka liwepo wakati halipo.
Kwenye suala la kiuchumi, nchi za Magharibi zimeweza kufanikiwa kufunga mipaka na kuwalazimisha wananchi wake wabakie majumbani mwao kwa masaa 24 bila kutoka nje kwa sababu mazingira ya kiuchumi yanaruhusu kufanya hivyo.
Kwa sasa wananchi wote wa nchi hizo pamoja na kwamba hawafanyi kazi lakini serikali imeamua kuwalipa mishahara na pesa za kujikimu na maisha wananchi wake wote mpaka pale watakapoanza kufanya kazi tena. Hata malipo rehani (mortgage) kwa sasa yamebebwa na serikali.
Kwa upande wa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ kama Tanzania, serikali haiwezi kubeba jukumu la kiuchumi kama zilivyofanya nchi za Magharibi kwa sababu haina uwezo huo na kama serikali italazimisha wananchi wake wabakie majumbani basi tutegemee machafuko nchini au familia nyingi kufa kwa njaa hasa zile zinazoishi kwenye maeneo ambayo bila kutoka ‘’nje ya nyumba’’ familia haiwezi kupata chakula cha siku.
Kwa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwamo Tanzania, binadamu anaishi kwa jasho/nguvu zake lakini kwa ‘’nchi za Magharibi’’, binadamu anaweza akaishi bila jasho/nguvu zake bali kwa msaada kutoka serikalini
Tanzania vile vile ni ''lango kuu'' na mkondo wa usafirishaji katika nchi karibu nane ambazo hazina bahari.
Haishangazi kwa sasa tumeanza kuona wananchi wakipigwa risasi katika nchi za Rwanda na Uganda kwa sababu wamekataa kutii amri ya kubakia majumbani mwao kutokana na ukweli kuwa kubaki ndani pia ni kukaribisha kifo kwa njaa. Ni bora watoke nje wakajaribu bahati ya kutafuta chakula kuliko kubaki majumbani mwao. Nadhani baada ya wiki moja hali itakuwa mbaya zaidi.
Huko Kenya, Rais Kenyatta amegundua makosa na kwa sasa amebadili msimamo wake ambapo badala ya amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao kwa saa 24 kwa sasa watafanya hivyo kuanzia majira ya saa 11 za jioni hadi saa 11 alfajiri. Hii mbinu ya Rais Kenyatta inashangaza kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi katika nchi zetu wanakusanyika zaidi mchana kuliko usiku!
Kwenye suala la kijamii, nchi za Magharibi zimefanikiwa kutokana na ukweli kuwa jamii zake zinaishi maisha ya ‘’kipweke’’. Ninaposema kipweke nina maana mazingira ya hali ya baridi na kazi yamewafanya wananchi wawe wanaishi maisha ya kujifungia ndani hata wakitoka kazini. Wenzetu hawana hii dhana ya ‘’kwenda kwenye kijiwe’’ kupiga stories au kwenda kwa ndugu au rafiki bila kutoa taarifa.
Kwa nchi kama Tanzania ambayo mikusanyiko ya kijamii na kifamilia ni sehemu muhimu ya maisha, ni vigumu sana kwa serikali kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wengi kama itatoa amri ya kuwataka wananchi wasifanye hivyo na badala yake wabakie majumbani mwao kwa saa 24.
Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwemo Tanzania haiwezekani kuzitumia kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.
Kama alivyosema Donald Ramsfeld, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’. Kwenye janga hili la COVID-19, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi alilonalo!
Kusifu na kutoa pongezi ni vitu viwili tofauti!1. Kenya na Uganda na wengine hapa Afrika wanapata shida kwa sababu huwezi kutoa amri ya watu kujifungia ndani (lockdown) kwa mwezi mzima bila kuwahakikishia upatikanaji wa mahitaji yao muhimu hasa chakula na mengine...
2. Kiukweli kama serikali za nchi hizi zilitoa amri za namna hii bila kufikiri juu ya haya, walifanya makosa
3. Kwa hapa Tanzania, binafsi nadhani tuendelee kuchukua tahadhari na huu siyo muda wa kuanza kujisifu.
Ukijisifu hivi, utafika wakati utalazimika kuchukua hatua hizihizi na sijui utaweka wapi sura yako....!
Tuendelee kuomba na pengine kikubwa ni ukiona mwenzio ananyolewa, ni bora na wewe ukaanza kujiandaa kutia maji nywele zako...
Kama ni lazima kuwafungia watu ndani kama sehemu ya uponyaji wao, itakazimika iwe hivyo tu bila kujali nini ni nini....!!
Nonsense!La sivyo basi ni chuki tu zinazosumbua moyo wako
Mkuu;Binafsi sijaona kosa la mtoa mada
nafikili wachangiaji wengi wanashindwa kujua hoja hasa ya mada
mtoa mada haconclude kwamba njia aliyoitumua Magufuri ndio sahihi! la hasha!
anachomaanisha ni kwamba njia hii ni sahihi kwa mazingira yetu, kutokana na nguvu ya kiuchumi tuliyonayo
Na isitoshe Corona si tishio sana kwa afrika(nisiulizwe kwanini tafadhari) hivyo kutofanya total lock down haitokua na athari kubwa kama kwa wenzetu
Lakini njia sahihi kwa nchi zenye uchumi mzuri ni Total Lock down kama inavyoshauriwa na wataalamu.
Mkuu hayo ni maelezo ya waziri wa afya huko zanzibar.Mkuu;
Siamini kama ulichoandika hapa ni kweli! Nadhani unatania!
Katika watu wasiomuunga Magufuli kwa mambo yake mengi, mimi ni mmojawapo, ila kwa hili na mengine machache sana namuunga mkono. Sina lolote la kumpinga au kumkosoa kwenye uamuzi wake huu.
Ok!Social distancing
Sikiliza, haya mambo si kama yale ya kuchutama Lumumba na kutoka na shauri .
kwanin tuvae kama madaktari wanaudumia wagonjwa then tukaendelea na shughuli zetu kuliko kujingia ndani.Ni kwa sababu Corona aijawa tatizo Tanzania na tuombe hali iendelee kubaki ivyo.
Wanaotaka watu kubaki majumbani sio kwamba wana hela za mchezo za kugawa isipokuwa hiyo ndio njia pekee ya kupunguza kasi ya ukuaji vinginevyo ingekuwa ni balaa.
Kubakiza watu majumbani ni maamuzi ya kisayansi sio kupenda ukiacha watu waendelee na shughuli kama kawaida mtu mmoja anaweza unga chain ya watu mianne ndani ya mwezi na ukifungia watu mtu mmoja anaweza sababisha chain ya watu 30 ndani ya mwezi unaweza ona tofauti kubwa sana hapo kwenye rate ya maambukizi.
Lengo la hatua hizo ni kuweza ku manage capacity ya utoaji wa huduma za afya ambazo hata kwa kufungia watu bado resources azitoshi kuhudumia wagonjwa ndio maana unaona hotel, sports centre zinageuzwa hospitals, wastaafu wanaitwa kurudi kazini, manesi wa mwaka wa mwisho washaajiliwa bila ya ku graduate na voluntary zaidi ya laki mbili na nusu wanahitajika NHS nchi kama UK.
Ukisema uache mambo yaendelee kama ilivyo ndio kabisa ni death sentence kwa watu wengi kwa sababu watakuwa hawana hiyo capacity ya ku deal na idadi ya wagonjwa kutokana na rate ya maambukizi.
Ndio maana wengine tunaomba hili janga mungu atuepeshuie mbali kama lilivyowakumba wengine maana sijui itakuwaje.
Mkuu;Sikiliza, haya mambo si kama yale ya kuchutama Lumumba na kutoka na shauri .
Hili ni jambo la kisayansi na kijamii, siyo siasa hata kidogo.
Wanaojadili impact ya jambo hili ni hawa
Virologist, Immunologists,Pathologist, Epidemiologist, Biost, Public health experts, infectious disease specialist, social worker kwa uchache. Wengine nje y team hiyo ni Economists.
Hao ndio wanaotoa ushauri wa COVID-19 siyo wanasiasa
Tuache siasa katika maisha ya watu.
Wewe ni kiongozi, huenda unalipwa kwa kusifia na kupongeza, lakini si juu ya maisha ya watanzania.
Hili ni balaa halihitaji mzaha, ona dunia inavyohangaika halafu utafakari upotoshaji wako na umasikini wa nchi yetu.
Mag3 Chige JokaKuu Pascal Mayalla
Angechukua harsha and radicala actions kama Korea
1.Tangaza hali ya dharura nchini (emergency)
2. Funga mipaka kwa muda hadi hali itakapoimarika, ahirisha shughuli za kitalii n.k.
3. Wazawa wanaorudi nyumbani wawe chini ya karantini, serikali igharamie ili kuondoa ukwepaji
4. Funga shughuli za mikusanyiko makanisani, misikitini, vikao vya harusi, michezo n.k.
5. Funga vyuo, shule , makongamano, warsha n.k
6. Hakuna Hoteli za kukusanya watu, ziruhusiwe kwa ''take away'
7. Weka social distancing, na zuia shughuli zisizo za lazima kwa wiki kadhaa.
8.Hakikisha kuna maeneo maalumu pindi hospitali maalumu zitakazidiwa
9. Hakikisha vifaa kwa wahudumu wa afya ili kuwakinga na janga
10. Tayarisha Watumishi wa afya wastaafu kama ''reserve'' ikibidi warudi kazini
11. Unda kamati maalumu itakayotoa taarifa kila siku katika vyombo vya habari kuhusu hali ilivyo nchini na duniani
Sisi bado saana, hatuna mbinu yoyote ya kujikomboa na hili janga kama kweli litavamia kama ilivyo Uchina, Ulaya na US, cha msingi omba Mwenyezi Mungu atuepishie hili janga...Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanasiasa kutaka Rais Magufuli na serikali yake wafunge mipaka ya nchi na kutoa tamko la kuwataka/kuwalazimisha wananchi wabakie majumbani mwao ili ‘’ kupambana’’ na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 yasisambae nchini.
Mashinikizo yanayotolewa kwa Rais Magufuli unaweza kuyaona niya msingi kama utadhani mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii ni sawa na mazingira ya ''Nchi za Magharibi'' ambazo zinatumia mbinu hii katika kukabiliana na janga la COVID-19.
Nakumbukwa kwenye sherehe ya wafanyakazi mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''Mtu yeyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, na yeye anajua una akili na anajua kuwa niya kipumbavu usipoyakataa anakudharau''.
Ni ukweli kuwa, Mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini yako tofauti sana na mazingira ya nchi za Magharibi na kwa msingi huu, haiwezekani mbinu za kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 yakafanana na nchi hizo.
Mwanasiasa wa Marekani aitwaye Donald Rumsfeld aliwahi kusema, ‘’You go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time.”
Kwa kiswahili ambacho sio sanifu, Donald Ramsfeld alisema, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’.
Kwa mantiki hii, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi la kiuchumi na kijamii alilonalo na sio ambalo baadhi ya wanasiasa wanataka liwepo wakati halipo.
Kwenye suala la kiuchumi, nchi za Magharibi zimeweza kufanikiwa kufunga mipaka na kuwalazimisha wananchi wake wabakie majumbani mwao kwa masaa 24 bila kutoka nje kwa sababu mazingira ya kiuchumi yanaruhusu kufanya hivyo.
Kwa sasa wananchi wote wa nchi hizo pamoja na kwamba hawafanyi kazi lakini serikali imeamua kuwalipa mishahara na pesa za kujikimu na maisha wananchi wake wote mpaka pale watakapoanza kufanya kazi tena. Hata malipo rehani (mortgage) kwa sasa yamebebwa na serikali.
Kwa upande wa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ kama Tanzania, serikali haiwezi kubeba jukumu la kiuchumi kama zilivyofanya nchi za Magharibi kwa sababu haina uwezo huo na kama serikali italazimisha wananchi wake wabakie majumbani basi tutegemee machafuko nchini au familia nyingi kufa kwa njaa hasa zile zinazoishi kwenye maeneo ambayo bila kutoka ‘’nje ya nyumba’’ familia haiwezi kupata chakula cha siku.
Kwa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwamo Tanzania, binadamu anaishi kwa jasho/nguvu zake lakini kwa ‘’nchi za Magharibi’’, binadamu anaweza akaishi bila jasho/nguvu zake bali kwa msaada kutoka serikalini
Tanzania vile vile ni ''lango kuu'' na mkondo wa usafirishaji katika nchi karibu nane ambazo hazina bahari.
Haishangazi kwa sasa tumeanza kuona wananchi wakipigwa risasi katika nchi za Rwanda na Uganda kwa sababu wamekataa kutii amri ya kubakia majumbani mwao kutokana na ukweli kuwa kubaki ndani pia ni kukaribisha kifo kwa njaa. Ni bora watoke nje wakajaribu bahati ya kutafuta chakula kuliko kubaki majumbani mwao. Nadhani baada ya wiki moja hali itakuwa mbaya zaidi.
Huko Kenya, Rais Kenyatta amegundua makosa na kwa sasa amebadili msimamo wake ambapo badala ya amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao kwa saa 24 kwa sasa watafanya hivyo kuanzia majira ya saa 11 za jioni hadi saa 11 alfajiri. Hii mbinu ya Rais Kenyatta inashangaza kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi katika nchi zetu wanakusanyika zaidi mchana kuliko usiku!
Kwenye suala la kijamii, nchi za Magharibi zimefanikiwa kutokana na ukweli kuwa jamii zake zinaishi maisha ya ‘’kipweke’’. Ninaposema kipweke nina maana mazingira ya hali ya baridi na kazi yamewafanya wananchi wawe wanaishi maisha ya kujifungia ndani hata wakitoka kazini. Wenzetu hawana hii dhana ya ‘’kwenda kwenye kijiwe’’ kupiga stories au kwenda kwa ndugu au rafiki bila kutoa taarifa.
Kwa nchi kama Tanzania ambayo mikusanyiko ya kijamii na kifamilia ni sehemu muhimu ya maisha, ni vigumu sana kwa serikali kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wengi kama itatoa amri ya kuwataka wananchi wasifanye hivyo na badala yake wabakie majumbani mwao kwa saa 24.
Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwemo Tanzania haiwezekani kuzitumia kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.
Kama alivyosema Donald Ramsfeld, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’. Kwenye janga hili la COVID-19, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi alilonalo!
Karibu sana, sio kwamba JPM hana mapungufu, yeye ni binadamu kama mwanadamu yoyote. Kuna mazuri mengi ambayo ameitendea nchi yetu sio wakati akiwa rais tu, bali hata alipokuwa waziri. Naweza kumlinganisha na marais waliomtangulia kama BWM au JMK na kukiri kwamba hawa wawili wakati wao hasa walipokuwa na madaraka ya juu hawakuwatendea haki Watanzania walio wengi.
Tanzania tulijulikana kama shamba la bibi. Hata nchi mbali mbali walifahamu kwamba Tanzania tumekosa direction. Leo hii wanafahamu sisi sio wale wa kuchezewa tena, adabu na heshima ya nchi yetu imerudi. Hata yule mropokaji mkuu ambaye alikuwa anajigamba ati anaongea na WB amebaki kula matapishi yake maana wazungu coronal virus imewatikisa, hawana wakati wa kuvisikiliza vikaragosi vyao vilivyoshikwa na utapia mlo na kwashakoo. Vimebaki kujibaraguza ati kujifanya kuandika vijimakala ili viwe na ushawishi kwenye uongozi wa serikali hii ..... .. … thubutu!
Tanzania ni taifa huru na wala haiwezi kupelekeshwa na vijikaragosi ambavyo vinafikiria vina turufu kwenye nchi yetu. JPM yupo pale kuhakikisha kwamba nchi yetu ni salama kila wakati iwe mchana usiku na wakati wowote kwa kizazi hiki na kijacho. Aluta Continua.
Mkuu maelezo yangu hayo madogo ndio umeandika maelezo yote hayo? Unaamini maelezo yako haya yanaweza kubadilisha msimamo wangu dhidi ya Magufuli, kwa kuwachafua baadhi ya watu? Nina uwezo wa kutosha wa kuelewa, na msimamo wangu sio wa bahati mbaya.