Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Watu waelewe kwamba ugonjwa huu wamafua hauna dawa. Waathirika wakubwa ni wazungu kuliko waswahili, kidogo immunity yetu inatusaidia.
Nadhani tafiti bado zinaendelea!
 
Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanasiasa kutaka Rais Magufuli na serikali yake wafunge mipaka ya nchi na kutoa tamko la kuwataka/kuwalazimisha wananchi wabakie majumbani mwao ili ‘’ kupambana’’ na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 yasisambae nchini.

Mashinikizo yanayotolewa kwa Rais Magufuli unaweza kuyaona niya msingi kama utadhani mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii ni sawa na mazingira ya ''Nchi za Magharibi'' ambazo zinatumia mbinu hii katika kukabiliana na janga la COVID-19.

Nakumbukwa kwenye sherehe ya wafanyakazi mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ''Mtu yeyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu, na yeye anajua una akili na anajua kuwa niya kipumbavu usipoyakataa anakudharau''.

Ni ukweli kuwa, Mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini yako tofauti sana na mazingira ya nchi za Magharibi na kwa msingi huu, haiwezekani mbinu za kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 yakafanana na nchi hizo.

Mwanasiasa wa Marekani aitwaye Donald Rumsfeld aliwahi kusema, ‘’You go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time.”

Kwa kiswahili ambacho sio sanifu, Donald Ramsfeld alisema, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’.

Kwa mantiki hii, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi la kiuchumi na kijamii alilonalo na sio ambalo baadhi ya wanasiasa wanataka liwepo wakati halipo.

Kwenye suala la kiuchumi, nchi za Magharibi zimeweza kufanikiwa kufunga mipaka na kuwalazimisha wananchi wake wabakie majumbani mwao kwa masaa 24 bila kutoka nje kwa sababu mazingira ya kiuchumi yanaruhusu kufanya hivyo.

Kwa sasa wananchi wote wa nchi hizo pamoja na kwamba hawafanyi kazi lakini serikali imeamua kuwalipa mishahara na pesa za kujikimu na maisha wananchi wake wote mpaka pale watakapoanza kufanya kazi tena. Hata malipo rehani (mortgage) kwa sasa yamebebwa na serikali.

Kwa upande wa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ kama Tanzania, serikali haiwezi kubeba jukumu la kiuchumi kama zilivyofanya nchi za Magharibi kwa sababu haina uwezo huo na kama serikali italazimisha wananchi wake wabakie majumbani basi tutegemee machafuko nchini au familia nyingi kufa kwa njaa hasa zile zinazoishi kwenye maeneo ambayo bila kutoka ‘’nje ya nyumba’’ familia haiwezi kupata chakula cha siku.

Kwa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwamo Tanzania, binadamu anaishi kwa jasho/nguvu zake lakini kwa ‘’nchi za Magharibi’’, binadamu anaweza akaishi bila jasho/nguvu zake bali kwa msaada kutoka serikalini.

Tanzania vile vile ni ''lango kuu'' na mkondo wa usafirishaji katika nchi karibu nane ambazo hazina bahari.

Haishangazi kwa sasa tumeanza kuona wananchi wakipigwa risasi katika nchi za Rwanda na Uganda kwa sababu wamekataa kutii amri ya kubakia majumbani mwao kutokana na ukweli kuwa kubaki ndani pia ni kukaribisha kifo kwa njaa. Ni bora watoke nje wakajaribu bahati ya kutafuta chakula kuliko kubaki majumbani mwao. Nadhani baada ya wiki moja hali itakuwa mbaya zaidi.

Huko Kenya, Rais Kenyatta amegundua makosa na kwa sasa amebadili msimamo wake ambapo badala ya amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao kwa saa 24 kwa sasa watafanya hivyo kuanzia majira ya saa 11 za jioni hadi saa 11 alfajiri. Hii mbinu inashangaza!

Kwenye suala la kijamii, nchi za Magharibi zimefanikiwa kutokana na ukweli kuwa jamii zake zinaishi maisha ya ‘’kipweke’’. Ninaposema kipweke nina maana mazingira ya hali ya baridi na kazi yamewafanya wananchi wawe wanaishi maisha ya kujifungia ndani hata wakitoka kazini. Wenzetu hawana hii dhana ya ‘’kwenda kwenye kijiwe’’ kupiga stories au kwenda kwa ndugu au rafiki bila kutoa taarifa.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo mikusanyiko ya kijamii na kifamilia ni sehemu muhimu ya maisha, ni vigumu sana kwa serikali kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wengi kama itatoa amri ya kuwataka wananchi wasifanye hivyo na badala yake wabakie majumbani mwao kwa saa 24.

Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya Tanzania na nchi za ‘’dunia ya tatu’’ haiwezekani kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.

Kama alivyosema Donald Ramsfeld, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’. Kwenye janga hili la COVID-19, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi alilonalo!
uchambuzi kama huu ulitakiwa uwe hotuba kabisa ya rais kwa taifa na dunia big up sana.
 
Rwanda au South Africa wanaweza je? Uganda, Kenya nao je?

China wamefanikiwa kupitia lockdown. Korea kusini nao hivyo hivyo. Kwani siku nyingi mafanikio ya Rwanda na South Africa katika mwezi 1 mbivu na mbichi zitakuwa nje.

Mtatafuta hata kwa tochi za kuhalalisha mipaka kuwa wazi.

Ila fahamuni kitakapo nuka sawa sawa ndipo itajulikana kuwa kufunga mipaka na kwenda lockdown kumbe inawezekana.

Kwa hapo haitakuwa for free itabidi tukumbushane kwa nini tulipuuzia.

Hizi kelele za sasa ngoma bado mbichi, kila mtu ana mdomo. Hata Italy, Spain na USA ilikuwa hivi hivi wakati ngoma ilikuwa bado mbichi. Leo wanajuta kwa kuchelewa mno.
kaa usubili dua la kuku alimpati mwewe..
 
Asante sana mkuu kwa uchambuzi mzuri na wa maana sana.
Nawashangaa hawa waajiriwa wa serikali wanataka nchi iwekwe karantini wakati uchumi utasimama ukisimama kinachofuata ni kupunguza mishahara tu.

Nani kaumia hapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna tatzo mkuu

Kitabibu haikupaswa tuzurure,vifaa tunavyotumia kwa ajili ya hili jambo ni duni
Uangalizi wetu ni dhaifu sana
Labda kibiolojia tuna bahati hayujadhurika


Kumbuka wadau wetu wa kiuchumi ndio waathirka wakubwa,wao kwa wao hawakaribiani sababu ya tahadhari

Wanapoona tunazembea katka hili amini itatupa wakati mgumu kutoka nje na kupokelewa
Majirani tu hawatupokei

Anayoamua kiongozi wetu tunapaswa kuyatafakari mno


Sent using Jamii Forums mobile app
Facts

Na unafikiri watakuelewa mkuu? Ila kwa vile familia ya mwenyekiti imekuwa waanga ndio maana maneno yamepungua
 
Washauri wa mh Rais kwa hili nawapongeza sana. Kweli ya Rwanda na Uganda yanaumiza mno
Baada ya wiki mbili kutakuwa na maasi kutoka kwa wananchi wanaotaka kutoka nje ili wakapate chakula cha siku!
 
Hakuna sehemu nimejigamba!

Hoja ya msingi inabeba swali linalouliza, unawezaje kuwafungia wananchi ndani ya nyumba wakati hawana chakula na wana njaa?
Kitu ambacho pengine kitasaidia, ni kwasababu asilimia kubwa ya wananchi wetu ni vijana wadogo.

Lakini utambuwe kuwa siyo mbinu za mataifa ya magharibi, bali ni maelekezo ya wataalam.
 
Hii picha ni tukio la Kenya leo. Hawa wameshukiwa kuvunja amri ya kutembea. Hapa mtu unashangaa si wanaambukizana zaidi kwa kulundikwa hivyo? Ni kweli kabisa. Nchi zetu hizi ambazo ili raia ale ni lazima atoke hizi amri haziwezekana. Na mbaya zaidi ni watu hawatatii na polisi watachukulia kama mradi wao.
View attachment 1401238
Yaani hata wiki haijapita wananchi wameanza kuonja joto ya maamuzi ya watawala!
 
Magu hakulaumiwa kwa hayo uliyosema bali kalaumiwa kwa mambo kama pale aliposema hawezi kuzuia watalii kuingia nchini! Uzuri ni kwamba, hao watalii wenyewe wana akili na wanafahamu risk iliyopo kwa wao kuendelea kusafiri, na kwahiyo wameamua kujizuia wenyewe huko huko kwao!

Na kwavile ndege nyingi zimesimamisha international flights, hiyo ndo nafuu yenyewe kwetu vinginevyo lau kama airlines na watalii wangekuwa na akili kama za JPM, balaa ambalo lingekuwa limeshatokea tungekuwa tunatafutana hivi sasa!

Zanzibar kwa mfano, wanapokea watalii wengi sana kutoka Italy! Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo Watalii wa Italy wangeendelea kuingia?!

Umeshawahi kujiuliza kingetokea nini endapo wananchi kwenye mataifa yaliyoathirika wangeendelea kumiminika kwa sababu tu Mpiga Ramli mmoja anaamini coronavirus haifui dafu mbele ya ibada?!

Lingine alilolaumiwa JPM ni kauli yake ya majuzi kwamba eti watu waendelee tu kumiminika kwenye nyumba za ibada na kwamba eti COVID-19 haiwezi kuishinda Damu ya Yesu!!

Ni mtu wa ajabu tu ndie anaweza kutetea ujinga kama huu kwa sababu hakuna janga hata moja lililowahi kuzimwa kwa watu kujazana makanisani na misikitini!

And FYI, zipo nchi nyingi tu ambazo zilidhani zingeendelea kuwa salama! Spain kwa mfano, daktari mmoja alifikia hadi kusema ni ngumu sana kwa Spain kupata maambukizo mengi kwa sababu tu walidhani kuto-share mpaka na Italy ingeweza kuwa salama kwao!

Leo hii, it's a matter of time kabla Spain hawajaifunika Italy!!

Hata Trump nae mwanzoni wala hakudhani ingekuwa serious issue kwa US! Leo hii US imeyapiku mataifa yote kwa idaidi ya maambukizi!!

So, endeleeni tu kutetea ujinga kwa sababu ndicho mlichoapa kukifanya!!
Imani yako ndogo
 
Watanzania wengi tunaishi kwa mkopo wa kulipa kesho, Mfano ugali wa leo nimekopa unga kwa mangi nitamlipa kesho..hapo utagundua hata hela ya kula leo sina.

Sasa nikae ndani wiki nzima mtaniua tu.!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mawazo/maisha yako nadhani yana akisi maisha ya Watanzania wengi!
 
MsemaUkweli umesema kweli tupu. Total lockdown pekee kwa Tanzania itauwa watu wengi sana kuliko hiyo corona, na kwa muda mrefu zaidi. Asilimia takribani 80% ya watanzania ni wakulima wadogo wadogo. Na asilimia 20 iliyobaki chakula chao kinatoka kwa hawa wakulima wadogowadogo. Sasa hivi ni kipindi cha masika, kipindi cha kulima. Ukiwa lock down maana yake mwaka huu watanzania wote million 60 hawatakuwa na chakula cho chote. Mifugo yote itakufa na kadhalika. Serikali itawezaje kuwalisha watanzania wote, kwa kipato kipi?

Total lockdown itafanya shughuli zote za kiuchumi ziwe sifuri kwa kipindi chote cha mlipuko huu wa corona ambao hatujui utachukua miezi au miaka mingapi. Maana yake mapato ya serikali (TRA) yatakuwa zero. Hivyo hakutakuwa na mishahara wala kitu cho chote kwa watumishi wa umma wote na hata wale ambao si watumishi wa umma. Yaani hata majeshi yetu ambayo nayo yatakuwa kwenye lock down except a few na wahudumu wa afya watakaokuwa wakitibu wagonjwa wa corona wanaweza nao wakakosa mishahara maana TRA watakuwa hawakusanyi cha kutosha na akiba yetu ndogo haitatosha. Wengi wetu ambao kipato chetu kwa siku ni hand to mouth tutakufa kwa njaa ndani ya siku mbili au tatu tu za total lock down, kitu ambacho hakuna atakayekubali, wote watatoka nje na polisi haitaweza kuwamudu.

Tuendelee kumuomba Mungu atuvushe kwenye hili janga. Tulishavuka na tunaendelea kuvuka majanga mengi tu yaliyoua watu wengi zaidi kuliko hiyi corona hususani kipindupindu, surua, kifua kikuu, ukimwi, utapiamlo, mafuriko, ajali za barabarani nk bila kuwekwa total lockdown. Hata hili tutalivuka bila total lockdown. Hakuna haja ya kuwa na hofu (panic). Huko China ambako population ni watu zaidi ya billion moja ugonjwa huu umeua watu wasiozidi elfu nne tu sawa na asilimia 0.0000001 of the population! Tusiogope, hii changamoto nayo itapita. Hofu na uwoga hupunguza kinga (immunity) ya mwili. Usiiruhusu. Ibada za makanisani na misikitini ni maeneo madhubuti ya kuwaondolea binadamu hofu na uwoga wa dunia hii na kuukabidhi kwa Mola, hivyo ku boost immunity ya binadamu.
Kwa kiwango kikubwa ninakubaliana na mawazo yako!
 
Back
Top Bottom