Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Nadhani unapoteza muda wako kutoa ushauri!

Kuna baadhi ya wachangiaji humu wala usipoteze muda wako kutoa ushauri labda kama huwajui vizuri!
 
Unataka kufanana kabisa na mfalme aliyekuwa akiitawala Dunia nyakati hizo za Biblia akiitwa Nebukadreza, naye hakuwahi kuipa nafasi nguvu ya Mungu ktk utawala wake kama unavyoidhihaki wewe,

Unapopinga mpango mpya huu WA mapambano kuhusu virusi hawa jaribu kuonyesha njia Bora kuliko hiyo ambayo Mh Raisi anaitumia, na uonyeshe kwamba njia yako hiyo ndiyo imessidia Taifa fulani

La sivyo basi ni chuki tu zinazosumbua moyo wako

Waliojifungia tunaambiwa kwamba ndiko vifo vingi na maambukizi mengi yanaendelea, elekeza njia sahihi watakusikia
 
Titafuteni pesa na maendeleo ya nchi zetu tuache kunyanyasika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusifu na kutoa pongezi ni vitu viwili tofauti!

Mimi nimetoa pongezi na sijasifia!
 
Mkuu;
Usihangaike sana na baadhi ya watu wanaosoma kichwa cha habari na kuanza kuandika maoni yao!
 
Katika watu wasiomuunga Magufuli kwa mambo yake mengi, mimi ni mmojawapo, ila kwa hili na mengine machache sana namuunga mkono. Sina lolote la kumpinga au kumkosoa kwenye uamuzi wake huu.

Karibu sana, sio kwamba JPM hana mapungufu, yeye ni binadamu kama mwanadamu yoyote. Kuna mazuri mengi ambayo ameitendea nchi yetu sio wakati akiwa rais tu, bali hata alipokuwa waziri. Naweza kumlinganisha na marais waliomtangulia kama BWM au JMK na kukiri kwamba hawa wawili wakati wao hasa walipokuwa na madaraka ya juu hawakuwatendea haki Watanzania walio wengi.

Tanzania tulijulikana kama shamba la bibi. Hata nchi mbali mbali walifahamu kwamba Tanzania tumekosa direction. Leo hii wanafahamu sisi sio wale wa kuchezewa tena, adabu na heshima ya nchi yetu imerudi. Hata yule mropokaji mkuu ambaye alikuwa anajigamba ati anaongea na WB amebaki kula matapishi yake maana wazungu coronal virus imewatikisa, hawana wakati wa kuvisikiliza vikaragosi vyao vilivyoshikwa na utapia mlo na kwashakoo. Vimebaki kujibaraguza ati kujifanya kuandika vijimakala ili viwe na ushawishi kwenye uongozi wa serikali hii ..... .. … thubutu!

Tanzania ni taifa huru na wala haiwezi kupelekeshwa na vijikaragosi ambavyo vinafikiria vina turufu kwenye nchi yetu. JPM yupo pale kuhakikisha kwamba nchi yetu ni salama kila wakati iwe mchana usiku na wakati wowote kwa kizazi hiki na kijacho. Aluta Continua.
 
Sikiliza, haya mambo si kama yale ya kuchutama Lumumba na kutoka na shauri .

Hili ni jambo la kisayansi na kijamii, siyo siasa hata kidogo.

Wanaojadili impact ya jambo hili ni hawa
Virologist, Immunologists,Pathologist, Epidemiologist, Biost, Public health experts, infectious disease specialist, social worker kwa uchache. Wengine nje y team hiyo ni Economists.

Hao ndio wanaotoa ushauri wa COVID-19 siyo wanasiasa

Tuache siasa katika maisha ya watu.

Wewe ni kiongozi, huenda unalipwa kwa kusifia na kupongeza, lakini si juu ya maisha ya watanzania.

Hili ni balaa halihitaji mzaha, ona dunia inavyohangaika halafu utafakari upotoshaji wako na umasikini wa nchi yetu.

Mag3 Chige JokaKuu Pascal Mayalla
 
kwanin tuvae kama madaktari wanaudumia wagonjwa then tukaendelea na shughuli zetu kuliko kujingia ndani.
 
Mkuu;
Wakati mwingine nikisoma maoni yako huwa ninacheka tu!

Kwa hiyo wewe ulipoandika haya hapa chini ulikuwa ni mmoja wa hao wataalam uliowataja?

Kuna kanuni inasema, ''ukiwa muongo usiwe msahaulifu''

 
Sisi bado saana, hatuna mbinu yoyote ya kujikomboa na hili janga kama kweli litavamia kama ilivyo Uchina, Ulaya na US, cha msingi omba Mwenyezi Mungu atuepishie hili janga...

Hatuna ujanja wowote so far wa kujikinga na hili janga unaoonekana....haya maji ya kunawa ni justification tu.

Gonjwa linalouwa raia 900 kwa siku wanaojitambua likizama hapa sijui nani atamzika mwenzake!!
 

Mkuu maelezo yangu hayo madogo ndio umeandika maelezo yote hayo? Unaamini maelezo yako haya yanaweza kubadilisha msimamo wangu dhidi ya Magufuli, kwa kuwachafua baadhi ya watu? Nina uwezo wa kutosha wa kuelewa, na msimamo wangu sio wa bahati mbaya.
 
Mkuu maelezo yangu hayo madogo ndio umeandika maelezo yote hayo? Unaamini maelezo yako haya yanaweza kubadilisha msimamo wangu dhidi ya Magufuli, kwa kuwachafua baadhi ya watu? Nina uwezo wa kutosha wa kuelewa, na msimamo wangu sio wa bahati mbaya.

Sina hata iota ya kubadili msimamo wako kwa JPM, ''mwanadamu yoyote kajaumbika kabla ya kufa.'' if you know what I mean. Kama post yangu ime-cause offence my apologies.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…