Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

God bless you brother.
 
Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JPM) yupo sawa. Raia hatuna hata fridge na wenye nazo bado umeme unaweza kuwa tatizo kwa upande wa kuhifadhi chakula cha muda mrefu. Nampongeza sana kwa kuliona hilo.
Huu ndio ukweli halisi ambao kuna watu kwa kuwa wanaishi katika maisha ya ''wananchi wa nchi za magharibi'' wanadhani watanzania wengi wana uwezo wa kuishi bila kutoka nje na kwenda kutafuta chakula cha siku!
 
Kwani serikali ndio imeleta huu ugonjwa? Hivi africa unawafungiaje watu ndani. Huoni utasababisha vifo vya njaa na utapiamlo?
Kama umeelewa uchambuzi huwezi kulaumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani baadhi ya nchi kama Uganda, Rwanda, South Africa na Kenya ambao wametoa amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao wana CAPACITY ya kuwapima, kuwahifadhi na kuwatibu wagonjwa wote wa COVID-19?

Nadhani hujajua hata msingi wa mada yangu!
Hili suala halihitaji watu ku jump into conclusions so early. Toa muda kidogo huu siyo wakati wa kujigamba.
 
Ninakubaliana kwa kiwango kikubwa na angalizo lako!

Ni ukweli kuwa mazingira yetu ya kiuchumi na kijamii hayawezi kuruhusu wananchi wajifungie ndani kwa zaidi ya wiki moja bila kutoka nje.

Kama ulivyosema, mtu hawezi kukubali kuishi ndani akifa polepole wakati akitoka nje atapata chakula ingawa kwa shinda na hatari ya kukamatwa.
 
Nakubaliana nawe kwa kiwango kikubwa!
 
Mzungu anaamini dinosaurs walitoweka kwa sababu miaka zaidi ya million 200 dunia ilitandikwa na comet moja kubwa iliyouwa karibu viumbe vyote ardhini.

Leo kuna watu wameajiriwa kufanya kazi usiku na mchana kuangalia asteroid belt and beyond kama kuna comet kubwa zinazoweza kuja karibu na sayari yetu na wana mipango ya kuifuata huko huko kuipasua miaka kadhaa kabla ya kutufikia.

Ndio tujue huku kufungia watu sio sera ya kubahatisha washakumbana na haya matatizo in the past kupitia ‘spanish flu’, washafanya experiments za simulation kutokana na tabia watu ndani ya jamii zao, washajifunza haya maambukizi yanavyotokea, hatua za kuchukua yakijirudia, wana optional solutions za scenarios mbali mbali kwenye kukabiliana na majanga ya sasa na mengine mbalimbali yanayoweza wakumba (these ppl plan ahead).

Itafika wakati lockdown itakuwa mandotory tu ata kwa Tanzania kukabiliana na virus pamoja na watu mnavyojaribu kujiaminisha; kwa sababu ndio njia pekee health systems zinavyoweza kukabiliana na utoaji wa huduma given their capacity.

Busara ni kushauri watu wenye kuweza kurudi vijijini kwa muda au kuelekea maeneo yenye less population density kuanza kufanya ivyo au kuja na ubunifu mwingine wa kuwalisha watu haswa maeneo ya mjini; hila lockup is inevitable watu wajiandae kabisa kisaikolojia.

Just wait
 
Mkuu umeasi ccm au umeamua kuidharirisha nchi yetu? A Dona county,nchi tajiri wananchi wake wanawezaje kukosa maji Safi ya kunywa? Je hili bandiko lako na yule aliyepiga picha ya mahandaki kwenye Barbara za ngorongoro tofauti ni Nini?
 
Kaka naona unatumia nguvu nying ili tu watu wamlaum magufuli hahahaha endelea bas [emoji1787][emoji1787]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbumbumbu katika ubora wake. Pole mkuu kwa kuwa mbumbumbu wa maisha!
 
Lazima utete ujinga... utatetea hadi suala la serikali kumvua madaraka Dr. Janabi kwa sababu aliongea ukweli kuhusu COVID-19. Na kwavile Janabi ameshatiwa adabu, hakuna daktari hata mmoja atakayeweka wazi ukweli kuhusu janga!
Acha kuleta habari za kuokoteza okoteza kwenye vijiwe vya wajinga wajinga!

Ni lini Dr. Janabi amevuliwa madaraka?

Dr. Janabi anaendelea na kazi zake kama kawaida.

Halafu hakuna aliloongea ambalo linapingana na serikali wakati yeye pia ni sehemu ya serikali na mmoja wa wataalam katika jopo la kushughulikia suala la COVID-19 nchini.
 
Ni haki yako kikatiba!

Hii picha ni tukio la Kenya leo. Hawa wameshukiwa kuvunja amri ya kutembea. Hapa mtu unashangaa si wanaambukizana zaidi kwa kulundikwa hivyo? Ni kweli kabisa. Nchi zetu hizi ambazo ili raia ale ni lazima atoke hizi amri haziwezekana. Na mbaya zaidi ni watu hawatatii na polisi watachukulia kama mradi wao.
 
Mkuu;
Ni kweli Dkt Janabi hajafukuzwa kazi.

Huyo unayemjibu ni kati ya wale wanaokoteza habari kwenye vijiwe vya wajinga wajinga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…