Januari ataja sababu za kusuasua kwa Mradi wa JNHPP

Januari ataja sababu za kusuasua kwa Mradi wa JNHPP

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Waziri wa Nishati, Januari Makamba ametaja sababu za kuchelewa kwa mradi wa Bwawa la Nyerere kuwa ni utendaji mbovu wa Menejimenti ya Tanesco kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

"Tuliamua kubadilisha menejimenti ya Shirika pamoja na Bodi na kuweka menejimenti mpya na bodi ambayo tunaamini inaelewa sayansi ya usimamizi wa miradi na wana uzoefu na uwezo wa kusimamia miradi mikubwa ya aina hii na matokeo tumeyaona tulibadilisha mfumo mzima wa usimamizi wa mradi huu sasa hivi kazi inafanyika kwa saa 24 kasi imeongeka" amesema Makamba.

Makamba alikuwa anatoa taarifa hiyo kwa kundi kubwa la Wahariri wa Vyombo vya Habari aliowapeleka kukagua mradi huo.

CHANZO: ITV Habari Saa 12 asubuhi Julai 9, 2022
 
Hii itakuwa ni sababu ya ngapi ameitoa kuhusu kusuasua kwa ujenzi wa hilo bwawa?

- Crane ya tani 26.

- Ukosefu wa pesa.

- Corona.

- Menejimenti iliyopita.

-

Bila shaka siku sio nyingi itafuatia sababu ya tano.

Naona bora akae kimya tu kazi ifanyike, anavyozidi kuongea ndio anazidi kujiaibisha, hizi siasa zake nyepesi zimepitwa na wakati.
 
Mradi umekiuka sheria za Mazingira za ndani na zile za Kimataifa - hauna baraka !! ni lazima udode.
Duuuu hii nchi no ngumu, naamini ungekuwa China ungenyongwa
 
Back
Top Bottom