Januari Makamba analaumiwa kwa kosa gani?

Mtumishiwetu

Senior Member
Joined
Jul 13, 2022
Posts
196
Reaction score
346
Naomba watanzania wenzangu mnisaidie jambo moja kila siku nikiamka kwenye mitandao nakutana na mijadala mbalimbali inayomkosoa Januari Makamba lakini mpaka sasa najiuliza Makamba amewafanyia nini watanzania hadi mumchukie kiasi hicho?

Kosa lake ni nini hasa? kama ni Wizara ya Nishati tayari alishaondoka lakini mbona bado mnaendelea kumsakama kijana wa watu amewakosea nini watanzania?
 
January sio kijana
 
Chuki dhidi yake inatokana na namna alivyotimiza majukumu yake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Aliisadia sana CCM kupata ushindi kwenye uchaguzi ule uliosheni hekheka.
Baadhi ya wanasiasa bado bado wana kinyongo naye
 
SSH angemwacha Dr Kalemani tatizo lote la mgao lisingekuwepo. Tatizo limetengenezwa na serikali na waziri asiye makini wala kujali maisha ya Watanzania.

Biashara ngapi zimekufa kutokana na mgao aliouanzisha? Maisha ya Watanzania wengi yameathirika vibaya sana na mgao wake na uongo wake karibu kila siku.

Mara tatizo hakuna repair, mvua, kuchepusha maji, crane, board ya Tanesco, ahadi kibao za uongo.

Ilibidi asifiwe na kupongezwa? Kuna waziri mbovu kuliko huyu Tanzania?
 
Tatizo nyota,JK kabla hajawa rais alikuwa anapendwa tu bila sababu,ila Jk ndio muasisi wa mgawo wa umeme,yeye ndo aliwaleta Dowans,IPTLna Richmond
 
Hana sifa ya kusifiwa
 
Miradi yake aliyoacha tanesco ndio inayotufanya tukose umeme hadi sasa
Umeonaeeeeeee ?
Wakati anaingia pale umeme ulikuwa stable lkn alipoingia akavuruga vuruga mifumo yote ili apige fedha
 
huyo kalemani angekojoa ili mito na mabwawa yajae? tuache kukariri
 
Reactions: Tui
Hakuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…