Januari Makamba: Kama kuna mtu anataka kutapika kwa sababu kina mama wa vijijini wamepata mitungi ya gesi, basi aende pembeni kutapika

Januari Makamba: Kama kuna mtu anataka kutapika kwa sababu kina mama wa vijijini wamepata mitungi ya gesi, basi aende pembeni kutapika

Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema kama kuna mtu anataka kutapika kwa sababu kina mama wa vijijini wamepata mitungi ya gesi basi aende pembeni kutapika lakini hataacha wala kusimamisha zoezi la kugawa mitungi kwa sababu ni msaada mkubwa kwa akina mama.

"Sasa kama kuna mtu anataka kutapika kwa sababu kina mama wa vijijini wamepata mitungi ya gesi, basi aende pembeni kutapika, lakini maisha yataendelea.Hatutaacha wala kusimama kuigawa kwa sababu ni msaada mkubwa kwa kina mama," amesema January.

CHANZO: Facebook/ Mwananchi Julai 25, 2022
Kipara hana sera
 
Magu alichowazidi mwenzao siasa na propaganda zake zilikuwa relevant kwa wananchi wa kitanzanua...hawa hata kudanganya tu wanashindwa sasa mtu wa kijijini na kutumia gesi wapi na wapi,sina uhakika hata kama huko vijijini kuna mawakala wa kudumu wa hizo gesi.
 
Yaani mtu anatumia hela za walipa kodi kununua mitungi kutoka kwenye biashara ya mtu wake wa karibu; halafu akiulizwa anasema waulizaji wakatapike.

Tena anapiga na picha majiko kayageuza tuone chapa ya ‘taifa gas hiyo si ni promotion ya bure’ anawafanyia.

Hila hawa jamaa wanadharau kweli, atoe hela yake mfukoni kununua hayo majiko hakuna mtu ata angaika nae.

Fisadi mkubwa
 
1. Njoo mniue

2. Mtusifie kama tumefanya vema

3. Mkatapike.

Huyu ni presidential candidate mtarajiwa. Huyu kichwa boga nilivyokuwa namdhania hata sivyo. Kuna kilaza mmoja bungeni akasema ati Harvard material . Pfyuuuu . Mama akiangalia waliofoji vyeti polisi ,apitie na walioiba peper ndani ya baraza labda tutapumua.
 
Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema kama kuna mtu anataka kutapika kwa sababu kina mama wa vijijini wamepata mitungi ya gesi basi aende pembeni kutapika lakini hataacha wala kusimamisha zoezi la kugawa mitungi kwa sababu ni msaada mkubwa kwa akina mama.

"Sasa kama kuna mtu anataka kutapika kwa sababu kina mama wa vijijini wamepata mitungi ya gesi, basi aende pembeni kutapika, lakini maisha yataendelea.Hatutaacha wala kusimama kuigawa kwa sababu ni msaada mkubwa kwa kina mama," amesema January.

CHANZO: Facebook/ Mwananchi Julai 25, 2022
Hahaha ujumbe wameupata akina Voicer, eltwege et al
 
Back
Top Bottom