Tatizo ukipenda, chongo utaita kengeza
Kila nililotaja hapo juu naweza kukupa mfano
Na kama unafahamiana nae muulize labda kwa jambo moja. Muulize ule mlolongo wote uliomfanya sio tu waziri, pia waziri wa Nishati. Muulize ilikuwaje hadi kupewa kwanza uwaziri, pili wa nishati. Je Samia ndio alimchagulia wizara? Nani walihusika katika kuwa kwake waziri?
Pili muulize ilikuwaje alipopewa uwaziri kina Tito Mwinuka ikabidi waondoke waje kina Maharage Chande. Nani alileta hiyo ajenda? Kama ni yeye alitumia ushawishi gani hadi Raisi akakubali? Nani walimuunga mkono kumshawishi Samia? Nini alichofanya au anachofanya Maharage Chande ambacho Mwinuka hakuwa anafanya? Tanesco imekuwa bora zaidi?
Kwa hiyo kama ni chuki unaziongelea hapa, labda ushauri wako kampe huyo January kwanza, ndio uje kutuambia sisi. Unachukia hadi watu waliokufa na kusema hutaki kufanya kazi na walioteuliwa nao, uko sawa wewe!
Tanesco inaongozwa na aliekuwa mkurugenzi wa Vodacom sijui, Wizara ya nishati inaongozwa na mtu ambae background yake hasa ni kuandika hotuba za Kikwete, kasomea fasihi sijui. Halafu tunapata matokeo madudu kabisa mnasema acheni chuki binafsi. Kuna watu mnafanya utani na nchi hii.
Watu kama January uwepo wao katika baraza la mawaziri na connection zao kwa baba yake na kina Kikwete unamfanya Samia awe kiongozi weak, na hilo Samia anapaswa kulitambua, na nitasema hata mbele yake.